
| Serikali yatoa Sh30 bn utafiti wa Sayansi | Send to a friend |
| Tuesday, 19 April 2011 09:22 |
|
Elizabeth Ernest Fedha hizo zimetolewa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia na Mawasiliano kupitia mfuko wa Utafiti na Maendeleo ambao utawasaidia wanafunzi wa fani ya ICT . Akizungumza kwenye wiki ya Maonyesho ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT), kuadhimisha miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana, Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Charles Kitwanga, alisema wizara yake inahitaji tafiti nyingi zinazohusu mawasiliano. “Mimi natoa wito kwenu wanafunzi mchangamkie hizi fedha za utafiti na mkazifanyie kazi ili tuweze kupata wataalamu wengi zaidi kwenye mawasiliano,” alisema. Kitwanga alisema CoICT, bado ni chuo kipya kina kozi mbalimbali za mawasiliano zitakazosaidia kuhamasisha mawasiliano kwa dunia nzima. Aliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutumia ujuzi wa taaluma yao kujiajiri na kuwaajiri wengine, sio kusubiri kuajiriwa ili kuongeza tija na ufanisi wa kile walichojifunza. |















Comments