MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Waliofariki dunia Loliondo wafikia 78  Send to a friend
Monday, 04 April 2011 22:40

Neville Meena na Mussa Juma, Samunge
IDADI ya watu waliopoteza maisha wakienda kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila katika Kijiji cha Samunge, Loliondo Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha imefikia 78.Habari ambazo Mwananchi limezipata na kuthibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Dominick Lusasi jana zinasema idadi ya vifo hivyo ni ile iliyorekodiwa kuanzia Machi 11, mwaka huu.

"Kati ya Machi 11, mwaka huu tulipoanza kuchukua rekodi za waliokufa na Machi 29, watu 74 walikuwa wamethibitishwa kufariki dunia, lakini hivi karibuni nilipata taarifa kwamba watu wengine wanne wamefariki," alisema Lusasi.

Hata hivyo, idadi hiyo inaweza kuwa ndogo kuliko uhalisia kwani upo uwezekano mkubwa kwamba wapo waliofariki dunia na vifo vyao havikurekodiwa tangu watu walipoanza kufurika Samunge mwishoni wa Januari ,mwaka huu hadi Machi 11, 2011 utunzaji wa kumbukumbu ulipoanza.

Kwa mujibu wa uongozi wa Kijiji cha Samunge, watu 19 wamelazimika kuzikwa kijijini hapo kutokana na ama maiti kukosa ndugu au ndugu kutokuwa na uwezo wa kusafirisha maiti hivyo kuomba msaada wa Serikali.
 
Majina ya waliofariki Miongoni mwa waliopoteza maisha ni mke wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mama Parceko Vincent Kone (55), watoto saba akiwamo mtoto wa miaka miwili, Bokye Mwilenyi Magoli, mkazi wa Kyang'ombe, Wilaya ya Rorya, mkoani Mara aliyefariki dunia Machi 25, 2011 sambamba na wagonjwa wengine 10 waliofariki dunia siku hiyohiyo.

 Taarifa ya Idara ya Afya ya Halmashauri ya Ngorongoro inawataja watoto wengine waliofariki dunia wakiwa Loliondo kuwa ni Fatma Hussein (5), mkazi wa Msambi - Kileche, Mwanga, Kilimanjaro; Athumani Omari (7), mkazi wa Ntiko, Singida; Tumaini Samson (10), mkazi wa Sengerema, Mwanza; Lesian Yuton (12) mkazi wa Dodoma Mjini na Jescar John (16) wa Dar es Salaam.

Mtoto mwingine aliyefariki dunia ni raia wa Kenya, Maximilian Shuku (12), mkazi wa Narok na raia mwingine wa nchi hiyo, Nori Makati (46) ambaye ni mkazi wa Usupuko.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, siku inayoongoza kwa vifo vingi ni Machi 24, 2011 ambayo watu 15 walipoteza maisha, ikifuatiwa na Machi 25 ambayo ilishuhudia wagonjwa kumi na moja wakifariki dunia hivyo kufanya jumla ya waliopoteza maisha kwa siku hizo mbili tu kufikia 26.

Majina ya watu wengine waliofariki dunia, umri na wanakotoka katika mabano ni Hassan Ally Tarimo (38- Moshi Mjini), Agness Costantine (43-Singida Mjini), Alex Godii (45 - Mererani, Manyara), Masinyari Nuhu (80 - Engaruka, Monduli), Daudi Shanu (31 -Moshi), na Holo
Nigha (40 - Kishapu, Shinyanga).

Wengine ni Grace Somi (59 -Moshi Mjini), Eva Sumaye (65 - Lekamba, Arusha), Hadija Wambura (30 - Tarime, Mara), Juma Ally (45 - Tanga), Fatuma Shaban (54 - Ngara, Kagera), Mrs Moshi (60 - Msagara, Moshi), Donald Msele (47 - Misungwi, Mwanza) na Mama Ndossi (70 - Bomang'ombe, Moshi). Wengine ni Okonbo Oguyi (78 - Musoma Vijijini), Stella Hagai (43 - Dar es Salaam), Diana Munisi (20 -Hai, Moshi), Flora Assenga (42 - Chumbageni, Tanga), Steward Mgosingwa (86 -Muheza, Tanga), Shanuel Mushi (22 - Lyamungo, Hai), Penina Wiga (38 - Shirati, Rorya) na Mwajuma Ramadhani (72 - Dodoma Mjini).

 Margaret (35 - Rorya, Mara), Eliashenya Bilingi (78 - Meru), Steven Haule (53-Majengo, Tabora), Mary Sindani (38 - Manyoni, Singida), Ngangi Nana (70-Milima Meru), Kabula Kazungu (24 - Nyanguge, Magu), Elizabeth Emmanuel (74 - Arusha) na Jaston Kusoma (35 - Katesh).

 Norbert Kudome (33 - Moshi), Philipo Jalo (35 - Mwanza), Stella Mwanyemba (42 -Busali, Kyela), Haikaeli Msocha (62 -Mlalo, Lushoto), Joy Rose (36 - Msanga, Chamwino), Hamis Kazyoba (70 - Kahama, Shinyanga), Mjaledi Munka (65 - Makete, Iringa), Esther Rutainyu (49 - Biharamulo) na Mwanahamis Rajabu (32 - Tabora Mjini).
Katika orodha hiyo pia wamo, Mwanaisha Isaka (70 - Dodoma Mjini), Rehema Sadalla (30 - Kiteto, Manyara), Emmanuel Napengwa (68 - Ilala, Dar es Salaam), Amina Kimweri (62 - Makanara, Korogwe), Butondo Mbuje (26 - Manyoni, Singida), Elise Mandari (76 - Mamba Kusini, Moshi), Jonathan Mnyiremi (Sorya, Manyoni) na Elisaria Urio (50 - King'ori Arumeru).

Wengine ni Shafu Muya (30 -Korongoni, Moshi), Paschal Shaghembe (47 - Geita Mjini), Bertha Muro (78-Machame, Hai), Lucas Machimo (56 - Ugogoni, Korogwe), Magdalena Kalole (35- Kimara, Dar es Salaam), Charya Mashishi (45 - Usanga, Maswa), Josephine Robert (34-Murukurazo, Ngara), Asha Nkinda (65 -Tanga Mjini) na Lyidia Msuya (78 - Kimara, Dar es Salaam).

 Wagonjwa wengine waliofariki ni Paulina Portea (65 - Ganako, Karatu), Alemwene Mwakatobe (69 - Mwanjelwa, Mbeya), Marieta Mandwa (56 - Shinyanga), Masalu Nhelegani (65-Nyangokolo, Bariadi), Emmanuel Mang'arai (56 - Arusha), Amina Chuwa (86 - Uru, Moshi), Eliadi Mariki (40 - Mwika, Moshi Vijijini) na Mmoja Juma (25 - Bukumbi, Tabora).

 Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwananchi lilishuhudia baadhi ya watu katika Kijiji cha Samunge wakiwa wamebeba maiti ya mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Rukia Rajab, Mkazi wa Kondoa wakati majina ya watu wengine wanne waliofariki dunia bado hayajatambuliwa.Kadhalika, mmoja wa maiti ambazo majina yake hayakutambuliwa alifahamika kuwa ni mkazi wa Biharamulo, mkoani Kagera.
 
Sababu za vifo
Lusasi alisema kwa mujibu wa taarifa za madaktari, vifo vingi vimesababishwa na magonjwa ya kisukari, pumu na shinikizo la damu. "Wagonjwa wengine walikuwa wakifika Samunge unamwangalia na kumwona kuwa huyu alikuwa amewekewa drip, lakini yuko pale akiwa kwenye foleni akisubiri kwenda kwa Mchungaji kunywa dawa," alisema Lusasi na kuongeza:

"Sasa katika hali hiyo kama mgonjwa ni wa kisukari, wengi walipoteza maisha kwani hata vyakula walivyokuwa wakila pengine havikuwa vikikidhi matakwa ya ugonjwa husika."Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, waliimarisha huduma za afya katika Zahanati ya Kijiji cha Samunge kwa kuongeza watumishi wa afya na dawa za magonjwa hayo lakini akasema watu walikuwa hawajitokezi hadi pale hali zao zilipozidi kuwa mbaya.

Alisema zahanati hiyo pia imekuwa ikipewa mgawo mkubwa wa dawa nyingine kutokana na kuongezeka kwa mahitaji na idadi ya wagonjwa kuongezeka.Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa siku kadhaa umebaini kuwa baadhi ya wagonjwa walichukua dawa za siku chache wakitaraji kwamba wangetumia muda mfupi kupata kikombe cha Babu, lakini kinyume chake walijikuta wakikaa kwenye foleni kwa muda wa kati ya siku saba na kumi na moja.

Kutokana na kuwapo kwa dalili za tiba ya Mchungaji Mwasapila kuendelea kwa muda mrefu, Lusasi alisema Halmashauri ya Ngorongoro inakusudia kujenga chumba kidogo cha kuhifadhia maiti katika Zahanati ya Samunge ili kukabiliana na tatizo la maiti kuzikwa kabla ya ndugu zao kufika kuwachukua.

Alisema sababu nyingine iliyochangia vifo hivyo ni kuzibwa kwa barabara kiasi kwamba gari la wagonjwa lililopelekwa na halmashauri kushindwa kuwasadia wale waliokuwa wamezidiwa."Gari lile mara kadhaa lilijaribu kupenya, lakini lilishindwa kutokana na watu kukataa kulipa nafasi, tulijaribu kila njia, kuweka mabango kwenye gari, kuweka bendera na hata kutumia kipaza sauti kutangaza lakini ilishindikana," alisema Lusasi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Tuesday, 05 April 2011 23:57
 
Comments 

0 #38 2011-04-06 19:21
Watu wajitahidi kutoa maoni kwa ustaarabu.
Quote
 
0 #37 2011-04-06 16:26
Mimi nasikitika sana kwani ndugu yangu kapotea tangu tarehe 17 mwezi wa tatu .Alienda na mke wake kwa babu lakini mke karudi peke yake bila mume ,Je kafariki au la!! mbona jina lake hapa alipo? yeye ni mkazi wa Majengo Moshi ana umri wa miaka 52 mwanaume.Jamani naomb amsaada wenu.Kama kafariki tujue au katupwa msituni???
Asanteni
Mwanamchi
Mama Minja V
Quote
 
+1 #36 2011-04-06 00:33
Mwacheni babu
Quote
 
+1 #35 2011-04-05 21:36
Tujulisheni pia watu wanaokufa kwenye hospitali kubwa zinazohudumia wagonjwa wengi kama vile muhimbili katika kipindi cha mwezi mmoja. Hiyo itasaidia watu kuelewa kuwa wagonjwa kufia hospitalini siyo ajabu. Bila hivyo mtakuwa hamjamtendea haki babu maana watu watachukulia kuwa huduma ya babu inasababisha watu kufariki.
Quote
 
0 #34 2011-04-05 21:09
kwamba amepona baada ya kunywa dawa ya babu? e! shetani anavitukoQuoting Rehema:
Quoting Shuhuda:
Quoting kipara:
lawama zote ziende kwa serikali ambayo kwa kiasi fulani inachangia katika hili.kila kukicha vigogo wa serikali wanakimbila huko kwa huyu kibabu jambo linaloashiria kwamba wanaamini hizi dawa za kishetani na kuwafanya wananchi wa kawaida hasa vijijini kuwa na imani zaidi ya kutibu maradhi yao sugu.hivi sasa wako wananchi wengi wameshapoteza mali zao kwa kuziuza ili wapate safari ya kwenda kwa kibabu na matokeo yake majumba na mashamba na mifugo vimeenda na magonjwa bado yako pale pale.nathubutu kusema tiba ya BABU ni usanii wa hali ya juu unaopigiwa debe na baadhi ya wanasiasa kwa faida yao wakishirikiana na wenye magari ya abiria.
lANA YA BWANA IWAFIKIE WALE WANAOWATAPALI WANYONGE

Nadhani wewe ndiye tapeli wa kwanza. Watu tumepona halafu wewe unaleta maneno yasiyokuwa na uthibisho. Pole yako unayedumaa na fikra zako potofu. Hata hivyo siyo lazima kila mtu aamini. Waache wenye imani kama yangu wakapate dawa na wapone kama mimi.

Pole wewe kupona kwako utashangaa mapepo ulienda kuchukua kwa huyo babu utashangaa shetani hakupi kitu bure,akikupa kimoja anachukua mia moja.Anayeponya ni yesu tu sio babu,umwamini Yesu usimwamini babu.
Quote
 
-1 #33 2011-04-05 20:10

-4 #32 2011-04-05 17:23
SOLAR LIGHT, SMALL PANEL WITH FOUR LIGHTS AND 2MOBILE Chargers, IDEA FOR VILLAGERS,STUDE NTS TO STUDY PEACEFULLY IN THE NIGHT, AND SMALLER RETAILERS DEALING IN THE PLACE OF LESS POWER IN ORDER TO INCREASE MORE MONEY.
CONTACT ME 4 BULK AND SMALL QUANTITY ORDER tahir_day@yahoo .com
Quote
 
-1 #31 2011-04-05 16:48
Quoting kipara:
lawama zote ziende kwa serikali ambayo kwa kiasi fulani inachangia katika hili.kila kukicha vigogo wa serikali wanakimbila huko kwa huyu kibabu jambo linaloashiria kwamba wanaamini hizi dawa za kishetani na kuwafanya wananchi wa kawaida hasa vijijini kuwa na imani zaidi ya kutibu maradhi yao sugu.hivi sasa wako wananchi wengi wameshapoteza mali zao kwa kuziuza ili wapate safari ya kwenda kwa kibabu na matokeo yake majumba na mashamba na mifugo vimeenda na magonjwa bado yako pale pale.nathubutu kusema tiba ya BABU ni usanii wa hali ya juu unaopigiwa debe na baadhi ya wanasiasa kwa faida yao wakishirikiana na wenye magari ya abiria.
lANA YA BWANA IWAFIKIE WALE WANAOWATAPALI WANYONGE

Nadhani wewe ndiye tapeli wa kwanza. Watu tumepona halafu wewe unaleta maneno yasiyokuwa na uthibisho. Pole yako unayedumaa na fikra zako potofu. Hata hivyo siyo lazima kila mtu aamini. Waache wenye imani kama yangu wakapate dawa na wapone kama mimi.
Quote
 
-1 #30 2011-04-05 16:43
Quoting jameyla:
kuna waliokufa weeengi baada ya kunywa dawa hiyo teyna wengi wa kisukari kwani waliaamini watapona na kuacha matibabu yao ya kila siku sasa huyo mtu aliyopewa maono na mungu yako wapi anaangamiza watu bila haya na hela anakusanya kwa nini hayo mamilioni asijenge yeye barabara na mahali pa kuhifadhia maiti anaomba msaada wa serikali wa nini????hayo mamilioni yameenda wapi mmmh haka kamchezo,,,,ato e hayo mamilioni yote kabla hajakimbia...

Tatizo Lako umekulupuka bila kujua unachangia nini.
Quote
 
+2 #29 2011-04-05 15:43
kuna waliokufa weeengi baada ya kunywa dawa hiyo teyna wengi wa kisukari kwani waliaamini watapona na kuacha matibabu yao ya kila siku sasa huyo mtu aliyopewa maono na mungu yako wapi anaangamiza watu bila haya na hela anakusanya kwa nini hayo mamilioni asijenge yeye barabara na mahali pa kuhifadhia maiti anaomba msaada wa serikali wa nini????hayo mamilioni yameenda wapi mmmh haka kamchezo,,,,ato e hayo mamilioni yote kabla hajakimbia...
Quote
 
0 #28 2011-04-05 15:29
wote mnaomsema vibaya babu hhamjaumwa subirini yawapate mtamjua babu ni nani na kwanini watu wanakwenda huko.imani yako kwa kila jambo itakuponya najua kwa jambo hili wapingaji wengi ni watu wa Makanisa na sababu zinaeleweka,wen ye maduka ya dawa na zahanati.kama huumwi waache wenye imani ya kupona huko kama ni kufa wangapi wanakufa hapo muhimbili au Bugando kwenye mabingwa,kama kwenda kule ni dhambi hiyo dhambi haitahama na kuja kwako kila mtu atahesabiwa kadili ya matendo yake.
Quote
 
0 #27 2011-04-05 14:48
lawama zote ziende kwa serikali ambayo kwa kiasi fulani inachangia katika hili.kila kukicha vigogo wa serikali wanakimbila huko kwa huyu kibabu jambo linaloashiria kwamba wanaamini hizi dawa za kishetani na kuwafanya wananchi wa kawaida hasa vijijini kuwa na imani zaidi ya kutibu maradhi yao sugu.hivi sasa wako wananchi wengi wameshapoteza mali zao kwa kuziuza ili wapate safari ya kwenda kwa kibabu na matokeo yake majumba na mashamba na mifugo vimeenda na magonjwa bado yako pale pale.nathubutu kusema tiba ya BABU ni usanii wa hali ya juu unaopigiwa debe na baadhi ya wanasiasa kwa faida yao wakishirikiana na wenye magari ya abiria.
lANA YA BWANA IWAFIKIE WALE WANAOWATAPALI WANYONGE
Quote
 
0 #26 2011-04-05 13:47
unajua serikali nayo inachukua nafasi ya[NENO BAYA]liza sisi tunaopeleka magari loliondo. watu wanaumwa tunatoa magari yetu ya utalii kupeleka watu loliondo, magari ya utalii tayari yameshalipiwa COMESA KWA MWAKA MZIMA inakuwaje tena tunaambiwa tulipe komesa nyingine? huo kwamba hii si halali?
Quote
 
0 #25 2011-04-05 13:41
Usiseme serikali haihusiki, serikali ni watu na watu wenyewe ndiyo sisi. serikali inayobudi kufuatilia, kujua na kusaidia pale wananchi wanapohitaji msaada wowote. serikali haiwezi kuona wananchi wengi kiasi hicho wanakufa au wanapata shida alafu inyamaze kimya haiwezekani kabisa. Lazima kwa babu kutakuwa ni msaada mkubwa sana na ndiyo maana wananchi wengi mno wanaelekea huko. Babu ni Mungu amemteua kwaajili ya watu wake. haijalishi
Quote
 
+1 #24 2011-04-05 13:32
Quoting resu:
TUSIITUPIE LAWAMA SERIKALI KWA VIFO VYA WATU HUKO LOLIONDO,KWANI HAIKUWALAZIMISH A.KUNA WENGINE WAMEZIACHA HATA HUDUMA ZA SERIKALI HOSPITALINI NA KWENDA KWA HUYO BABU WENU.BADO TUIPONGEZE KWA KUKUBALI KUWEKA HUDUMA KADHAA HUKO LOLIONDO.KWA SABABU HIYO TIBA NI MKATABA KATI YA BABU NA WAGONJWA,KWA HIYO NI BABU MWENYEWE ALIETAKIWA AYAWEKE MAZINGIRA YAKE SALAMA KWA WATEJA WAKE.HIVI HATUONI HOSPITALI ZA WATU BINAFSI?

Suala si kulazimisha au kwenda kwa hiari.Hata kwenye huduma za kawaida hakuna sheria inayolazimisha mtu kwenda hospitali kutibiwa,au hujui.Kinachofanyika elimu inatolewa ili mtu afanye uamuzi[informed choice],ila huduma itakayotolewa iwe salama na kuthibitishwa na serikali.Tiba ya babu ni kinyume kabisa na sheria yoyote hapa nchini.Hata kama viongozi wote watakwenda huko,bado haihalalishi tiba hiyo.SHERIA IMEVUNJWA.Babu anafanya biashara isiyo halali.Yale mamilioni yake,kodi ya serikali ni sh ngapi?Wafanyakazi wake wako kwenye shirika gani la huduma za jamii?Hata Yesu alilipa kodi!Babu alindwe asije akapotea ghafla kama Balali,ili tuone mwisho wake.
Quote
 
Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!

Banner
Banner