MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Fumua fumua CCM, Makamba na Sekretarieti wajiuzulu  Send to a friend
Sunday, 10 April 2011 06:39

Waandishi wetu, Dodoma
MABADILIKO makubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yamefanyika baada ya wajumbe wa sekretarieti ya chama hicho kujiuzulu.

Kutokana na hali hiyo, huenda Kamati Kuu nayo ikajiuzulu na kubakiwa na Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge, Anna Makinda ambao wanaingia kwa nafasi zao na John Malecela ambaye ni Mjumbe wa Kudumu.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokutana mjini Dodoma jana, zinaeleza kuwa hatua hiyo inatokana na mgawanyiko uliokikumba chama hicho.

Hatua hiyo ya kujiuzulu kwa wajumbe wa nafasi  nyeti ya chama hicho, inakuja miezi mwili baada ya Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete kueleza wazi kuwa chama kinahitaji kujivua gamba ili kiweze kurejesha heshima yake.

Akihutubia kilele cha maadhimisho ya siku ya kuzaliwa CCM, mjini Dodoma Februari 5 mwaka huu, Rais Kikwete alisema chama hicho kinahitaji mabadiliko makubwa kiweze kurejesha hadhi yake.

Wajumbe waliojiuzulu ni Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba ambaye ni mwenyekiti, manaibu makatibu wakuu wa CCM Bara na Visiwani, George Mkuchika na Saleh Ramadhan Feruzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati.

Wengine ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makala, Katibu wa Mipango, Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata jana usiku zilieleza kwamba Makamba aliwasilisha barua yake kwa kuiweka kwenye meza ya mwenyekiti kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Taarifa hizo zinasema kuwa baada ya kuwasilisha barua hiyo, Makamba aliomba ruhusa ya kuondoka kwa maelezo kuwa amepata msiba nyumbani kwao Tanga.

Hata hivyo, wajumbe wa kamati hiyo walikataa kutokana na umuhimu wake kwenye kikao hicho,  hivyo wakamweleza kuwa atume mwakilishi kwenye msiba.

Habari zaidi zinasema, Makamba amemtuma mwanaye, Januari Makamba ambaye ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga kwenda kumwakilisha kwenye msiba huo.

Awali wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), waliendelea kuvutana na kusababisha kuahirishwa kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichokuwa kianze jana.

Kikao cha CC ambacho kilianza juzi jioni kilitarajiwa kumalizika usiku wa siku hiyo na jana kilikuwa kifanyike kikao cha NEC, ajenda kuu ikiwa ni kujadili tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo, Kamati Kuu iliyoanza kikao saa 10 jioni juzi, iliahirisha kikao chake saa 1:00 usiku na kurejea tena saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, bila kumaliza kupanga ajenda za NEC.

Wajumbe wa NEC walianza kukusanyika asubuhi jana katika Makao Makuu ya CCM, baadaye walitakiwa kurudi tena saa 7:00 mchana,  lakini waliporejea walitakiwa kurudi tena saa 10:00 jioni, pia walitakiwa kurejea leo saa 3:00 asubuhi.

Kuahirishwa kwa kikao cha NEC, kulidaiwa kuwa kumetokana na CC kutomaliza kuandaa ajenda za kikao hicho.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa hatua ya kuahirishwa kwa kikao hicho ilitokana na kuwepo kwa mvutano mkali kati ya wajumbe wa CC, wakitaka baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wajiuzulu ili kukinusuru chama kutokana na tuhuma mbalimbali kinazobebeshwa na kuharibu taswira yake.

Kundi hilo linadai pia kuwa kama wajumbe hao watatoswa watakuwa wamewanyima Chadema ajenda mbele ya wananchi, lakini kundi jingine linalowaunga mkono likipinga mapendekezo hayo.

Baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa CCM, wanaunga mkono kundi hilo la watuhumiwa lilikuwa likikutana kwenye hoteli moja, wakihaha kuhakikisha ajenda hiyo inazimwa.

Katika mkutano huo, inadaiwa ajenda nyingine iliyokuwa na mvutano zaidi ni ya Muswada wa Sheria ya Kubadilisha Katiba wa 2011 ambapo katika kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema pia alihudhuria.

Wanaotajwa kurithi nafasi ya Makamba ni, Balozi wa Tanzania nchini Russia, Jaka Mwambi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kanali Abdulrahman Kinana, ambaye anadaiwa anaweza kukinusuru chama hicho na mgawanyiko uliopo, anadaiwa kukataa nafasi hiyo baada ya kuombwa na mwenyekiti. Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa amekubali kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Mwingine anayetajwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira, lakini anahukumiwa na historia yake ya kuhama chama hicho kwenda NCCR-Mageuzi mwaka 1995.

Kikao hicho kinadaiwa pia kujadili matamshi ya kejeli na matusi yaliyotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) dhidi ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kuwa yanakigharimu chama.

“Kama kuna kitu kimetugharimu kichama ni kauli za UVCCM, huwezi ukabeza mchango wa Frederick Sumaye. Huyu amelitumikia taifa na chama kwa muda wa mrefu,” kilisema chanzo chetu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema ngoma bado ni nzito na kuwataka wajumbe wa Nec kuwapo kwa ajili ya kikao leo saa 5:00 asubuhi.

Hata hivyo, Chiligati alikataa kutaja ajenda zilizokuwa zikijadiliwa kupelekwa NEC na kuahidi kuzitaja kwa waandishi wa habari leo saa 3:00 asubuhi.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Monday, 11 April 2011 00:08
 

Comments 

 
0 #73 2011-04-11 08:28
[*]ccm mko hatarini si mlijifanya mnajua kila kitu leo vipi?hiyo ya kujiuzulu kwa makamba siyo jibu mnachotakiwa kufanya ni mbona hata mkulo alisema kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake huyo naye ni wa ccm achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kauli ya maudhi kwa watanzania.pia uvccm na wao wajiuzulu.
Quote
 
 
0 #72 2011-04-11 00:14
KUBADILI STYLE YA KUCHEZA KWA MSANII ALIYEKAA JUKWAANI KWA MDA MREFU NA KUSHINDWA KUMFURAHISHA MTAZAMAJI ALIYELIPA KIINGILIO NI MARA CHACHE SANA KUTABADILI MTAZAMO WA MTAZAMAJI ALIYEKWISHA MTAFSIRI MSANII HUYO KAMA ALIYECHUJA KISANII!! KUJIUZULU KWA KAKAMBA HAKUNISAIDII KUUBADILISHA MTAZAMO WANGU JUU YA CCM ILIYOSHINDWA KUNITUMIKIA BALI INANIFANYA NITHIBITISHE MTAZAMO WANGU KUWA CCM NI CHAMA KILICHOPOTEZA MWELEKEO!! KWELI CHADEMA WAMEIADHIBU CCM BILA WAO PENGINE CCM ISINGEONEKANA KUWA NA MAPUNGUFU NA KILA KITU KINGEONEKANA KUWA SAWA! SWALI LA KUJIULIZA... BAADA YA MAKAMBA NA WENZAKE KUJIUZULU,, NINI KINAFUATA?
Quote
 
 
0 #71 2011-04-11 00:08
Bwana Jones uliyoandikayote yako sahihi, tatizo zima liko kwa wapigakura wasiojua kusoma nakuandika, ni vema kuhakikisha upigaji wa kura ni rahisi kiasi kwamba mtu atachagua mwenyewe mtu wake bila msaada wa mtu.
Pili kama utaratibu ni huo huo uliotangulia Rais kuteua tume a uchaguzi na matokeo kutohojiwa, basi safari bado ndefu sana, wataendelea kutumia udhaiufu wa taratribu kubaki madarakani hata kama kubaki kwao madarakani kutawakera wananchi kiasi gani.
Kwa kifupi CCM wamegeuza ufisadi kuwa ni dini, wanaamini bila kulinda ufisadi hakuna uhai.
Quote
 
 
0 #70 2011-04-10 23:33
NDIYO,HUYO JANGA LA KISIASA AMEFANYA VIZURI KUWAJIBIKA.
Quote
 
 
0 #69 2011-04-10 23:13
Bado kikwete ajiuzuulu kwani naye yupo kwenye kamati kuu. Igeni kule bondeni kwa MANDELA.
Quote
 
 
0 #68 2011-04-10 22:54
nazi kachagua mwenyewe, chuzi limeharibika akimwaga mboga sie twazidi teseka na njaa. kisha mwamsifu. ngoja zije nazi nyingine mbovu hadi tufe njaa ndo mtajua kosa ni la mchagua nazi
Quote
 
 
0 #67 2011-04-10 22:37
Michuzi blog inachakachua maoni yetu sisi wananchi.
Quote
 
 
-4 #66 2011-04-10 20:35
Hongera Kikwete! Hongera sana Raisi wetu. Wewe ndie uliye na moyo wa Gobachevu. Kulikuwa na watenda Dhambi ndani ya chama na walifikia pahara pa kutisha.Nakuomba Raisi Ruhusu katiba yenye Uhuru a mahakamkuu na Bunge liwe huru. Hapo utakuwa umeua sungura sita kwa risasi moja. Fukuza wajumbe wote katika house of Congress na CC wenye dhambi na usiwaonee haya, Pili weka wasomi sasa walifuzu vyuo vinavyoeleweka ili upate chama kinachojenga uchumi na sio siasa safiiii. Najua una kazi kubwa lakini mungu yupo nawe na atakulinda.
Quote
 
 
+5 #65 2011-04-10 20:29
Sumaye katumikia taifa na chama muda mrefu lakini hana historia ya kutatua matatizo ya wananchi kama sokoine au Lyatonga. Alikaa pale laibon kwa miaka kumi na hakuthubu kamwe hata siku moja kutatua tatizo laforeign barabara ya ali hassan mwinyi. Hivyo kumfanya wa maana katika CC ni kosa kubwa sana sana. Cha maana alichofanyia taifa hakijulikani!
Quote
 
 
+5 #64 2011-04-10 20:13
Zakia Meghji yule Fisadi wa EPA? Kweli nyoka akijivua gamba kamwe hatogeuka kuwa mjusi.
Mafisadi + CCM = mafisadi nyoka
Quote
 
 
+1 #63 2011-04-10 19:59
afadhali ccm wameonyesha kuanza kujitambua kiukweli kulikua na haja ya kujiuzulu ili kurudsha heshma ya chama na kuweka watu wenye uelewa na kujitambua co kujibujibu 2 ka makamba
Quote
 
 
0 #62 2011-04-10 19:48
Baada ya Makamba kujiuzulu na genge lake, Labda Uhuni utapungua CCM.
Quote
 
 
+1 #61 2011-04-10 19:20
Any responsible leader should take resiponsibiliti es incase he/she is no longer infuential to the society concern.Makamba should check the state of moving wind.
Quote
 
 
+10 #60 2011-04-10 19:03
R.I.P-CHAMA CHA MAFISADI, aka CCM, Dont forget to Prepare your shameless face once you meet Nyerere, Karume and Sokoine at the resting room....AMENIIIIIIIIIII I....
Quote
 
 
+4 #59 2011-04-10 18:53
NILIKWISHA KUSEMA NA NINARUDIA KWA HAYO MFANYAYO CCM, MZIMU WA.... HAUTA WAONEA HURIMA HATA KIDOGO. MI NADHANI WATANZANIA TUAMKE SASA, HATA KAMA NI KULA BASI WALE NA WENGINE. KWANI CCM WAMESHAKULA VYA KUTOSHA. LA MSINGI TULILIE KATIBA ILIYO IMARA KWANI TUKIWA NA KATIBA IMARA, HATA HAO WENGINE TUTAKAOWACHAGUA TUTAWABANA KISHERIA. KULIKO HALI ILIVYO SASA. YATARUDI YALE YALE YA SIKU ZOTE.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner