
| Wabunge 143 hawachaguliki uchaguzi 2010 | Send to a friend |
| Tuesday, 27 April 2010 23:32 |
Said PowaWABUNGE 143 kati ya 232 wanaotoka katika majimbo ya uchaguzi hawachaguliki, hivyo ni vigumu kurejea bungeni baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet). Utafiti wa taasisi hiyo iliyo chini ya Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam unaonyesha asilimia 61.7 ya wabunge wa bunge la sasa hawatachaguliwa tena. Wakijibu swali lililoulizwa katika utafiti huo kuhusu uchaguzi mkuu ujao kama watachagua mbunge wao aliyepo sasa, asilimia 39.3 ya wananchi ndio waliosema watachagua mbunge wa sasa, wakati asilimia 61.7 ya wote waliyohojiwa walisema hawatamchagua mbunge wa sasa. Utafiti huo ambao ulifanywa kwa ajili ya kutafuta maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi mkuu ujao, ulishirkisha wilaya 52 na kuhoji watu 2600 ikiwa ni watu 50 kutoka kila wilaya. Akisoma matokeo ya utafiti huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk Bernadeta Killian alisema kuwa waliyohojiwa pia walikuwa na maoni tofauti. Alisema asilimia 38.3 walisema watachagua mgombea mwingine wa chama chake, asilimia 8.7walisema watachagua mgombea wa chama kingine, asilimia12.4 walisema hawajaamua bado na asilimia 2.9 walitoa majibu mengine tofauti. Kutokana na hali hiyo, mtafiti huyo wa Redet alisema kuwa karibu asilimia 62 ya wabunge wa sasa hawatachaguliwa tena majimboni mwao. Utafiti huo pia unaonyesha kuwa Rais Kikwete na chama chake cha CCM wanaendelea kushika nafasi ya juu kutokana na maoni ya wananchi hivyo kuashiria kuwa CCM itarejesha wabunge wengi na mgombea huyo wa urais atashinda kwa kishindo. Kwa mujibu wa utafiti huo, waliohojiwa walitakiwa kutoa maoni yao katika swali lililoulizwa kuwa mwezi Oktoba mwaka huu utafanyika Uchaguzi Mkuu, "kama uchaguzi huo ungefanyika leo wewe ungemchagua mgombea wa chama gani?" Asilimia 77.2 (1997) ya waliohojiwa walisema watamchagua mgombea wa urais wa CCM, asilimia 9.2 (237) ikisema itamchagua mgombea wa CUF, asilimia 4.2 (109) mgombea wa Chadema, wakati asilimia 8.7 walisema bado hawajaamua ni mgombea wa chama gani watampigia kura. Kwa upande wa wabunge, inaonyesha CCM itapata upinzani mkali katika baadhi ya maeneo kwa kuwa utafiti huo unaonyesha asilimia kushuka ikilinganishwa na ya urais. Asilimia 68 ya waliohojiwa walisema watachagua mgombea ubunge wa chama hicho. Asilimia 10.2 watachagua mgombea CUF na asilimia 8.6 watachagua mgombea wa Chadema wakati vyama vingine vikitajwa kwa idadi ndogo sana na matokeo hayo yamekuwa yakijirudia kwa asilimia hizo hata kwa madiwani. Kuhusu uchaguzi wa urais, wahojiwa walitakiwa kumtaja mtu mmoja ambaye wangependa awe rais. Rais wa sasa, Jakaya Mrisho Kikwete ameendelea kuwabwanga wengine waliotajwa kwa kujikusanyia asilimia 66.9. Kikwete amefuatiwa kwa mbali na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata asilimia 6.7, Freeman Mbowe (3.1) na Dk. Asha Rose Migiro asilimia 0.7. Wengine ni Salim Ahmed Salim asilimia 0.7, Dk Willibrod Slaa asilimia 0.6, Zitto Kabwe asilimia 0.6, Seif Sharrif Hamad asilimia 0.5, Dk. Ghalib Bilali asilimia 0.5 na Balozi Ali Karume 0.3. Aidha, utafiti huo ulihoji kuhusu utendaji kazi wa Rais Kikwete katika kipindi cha miaka mitano na kuonyesha kuwa asilimia 49 ya waliyohojiwa wanaridhishwa sana na utendaji wake, asilimia 36.5 wanaridhishwa kiasi wakati wasioridhika kabisa ni asilimia 13.1 na wasiojua kitu kuhusu suala hilo ni asilimia 1.1 Takwimu hizi zikilinganishwa na tafiti zilizopita za Redet inaonekana kiwango cha kuridhika na utendaji kazi wa Rais Kikwete miongoni mwa wananchi kimeanza kupanda. Oktoba 2009 ilikuwa asilimia 67.4, Oktoba 2007 ilikuwa asilimia 44.4, Novemba 2008 ilikuwa asilimia 39.5 na Machi 2010 ilikuwa asilimia 49.3. Kuhusu imani ya wananchi kuhusu utendaji kazi wa viongozi na serikali, utafiti huo unaonyesha kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewabwaga viongozi wengine akiwemo Rais Kikwete. Kwa mijibu wa utafiti huo, Pinda anaongoza kwa asilimia 61.2 , akifuatiwa na Rais Kikwete mwenye asilimia 58.8 (1528). Wengine ni Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein aliyepata asilimia 46.8, mawaziri (25.7) madiwani (44.5) na wabunge ni 38.7 . |
| Last Updated on Thursday, 29 April 2010 13:14 |



Said Powa











Comments
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
MAJIBU KAMA HAYO YATAKUWA YANAMWELIMISHA MPIGA KURA ILI AWEZE KUTUMIA VIZURI ZAIDI FURSA YAKE KATIKA KUCHAGUA KIONGOZI BORA NA NIKUIMARISHA DEMOKRASIA HAPA TANZANIA.REDET ISHIRIKISHE WATAALAMU WENGI ZAIDI KATOKA FANI MBALI MBALI NA WAPEWE UWEZO ZAIDI WA KUWAWEZESHA KUBORESHA TAFITI ZAO ILI ZITO MAJIBU YANAYOONYESHA VIONGOZI WATARAJIWA WANAVYOTOFAU[NE NO BAYA] KATIKA VIGEZO MUHIMU VYA KIONGOZI BORA.
MAJIBU WALIOTOA HAPA HATUSAIDII KATIKA HILO.
Pamoja na kusomeshwa shule ya English medium bado hujui English! Grammer hiyo PTU! andika kiswahili tu ijulikane moja! Bird Brains!
KADRI SIKU ZINAVYOKWENDA:
1. Demokrasia inaimarika au inapungua;
2. Ubora wa maisha unaongezeka au
unapungua
3. Ubadhirifi na uizi wa mali za uma
unaongezeka au unapungua
4. Ubora wa viongozi wa kisiasa na
kiserikali unaongezeka au unapungua
Kwenye mazingira tuliyo nayo kwa sasa ambapo kuna demokrasia ya chama kimoja tawala kinachosindikiz wa na utitiri mkubwa wa vyama vidogovidogo visivyokuwa na uwezo, kuruhusu mgombea binafsi kungeimarasha demokrasia au hapana.
nawapongeza mwananchi kwa website yenu mpya na hasa ktk ukurasa huu wa maoni sasa hivi upo fair maana nilishaanza kupoteza imani na nyie, maoni yalikuwa yanawekwa ya baadhi ya watu wanaojulikana utakuta mtu mmoja kurasa moja maoni 5 wengine kapuni,mimi nilishaacha kutuma maoni kwenu kama nilivyokoma kwenye blogu fulani.TUNAWAAMINI KAZI NJEMA!
Utafiti huu ni njia ya kupikia matokeo. Watafanya kila njia kufix matokeo haya na ya uchaguzi. Uchaguzi ukiwa huru na haki CCM itapata wabunge chini ya 50% na Kama JK atashinda basi hatavuka 55% ya kura zote, huko Zanzibar CCM ndiyo watashindwa kabisa.
REDET Imepoteza credibility katika research zake biased wanachofanya ni kuganga njaa ili serikali ya CCM iendelee kuwapatia fedha za walipa kodi waendelee kudanganya umma wa watanzani