
| Bunge latoa masharti kupokea shangingi la Mbowe | Send to a friend |
| Wednesday, 22 June 2011 22:58 |
|
LAMTAKA AACHE KILA KITU ALICHOPEWA, MTIKILA AMUUNGA MKONO "Haya ni mambo ya kisiasa na sisi kama watendaji hatutaki kujiingiza kwenye siasa. Lakini niseme tu kwamba, lile gari hakupewa kufanyia shughuli za kisiasa ni la Serikali kwa ajili ya kazi zake kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni," alisema Joel na kuongeza: Joel alisema moja ya masharti aliyopewa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kupokea gari la Serikali, dereva na kuwekewa mafuta kwenye gari hilo wakati wa shughuli za Bunge. "Sasa pamoja na kupewa gari, Ofisi ya Bunge pia inawajibika kisheria kumpa kiongozi huyo nyumba mbili; Dar es Salaam na Dodoma na mlinzi wa kulinda usalama wake wa kila siku," alisema Joel.Aliendelea,"Sasa akisema gari sitaki, huu ni utashi wake, lakini kwa nini akatae gari tu wakati kuna huduma zingine anazopewa?" Juzi baada ya kupitishwa Bajeti ya Serikali, Kambi ya Upinzani ilitangaza mgogoro na Bunge wa kutochukua posho za vikao vya Bunge kuanzia jana. Lakini hili lingefanyika baada ya kuwasilisha taarifa rasmi bungeni jana. Hata hivyo, wakati kambi hiyo ikitoa msimamo huo wa pamoja, Mbowe alitangaza kuacha kutumia gari alililopewa na Serikali, dereva na mafuta kama sehemu ya kuonyesha kutoridhishwa na hatua ya Serikali kudharau mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na kambi hiyo kuiboresha bajeti. "Tumewaita hapa kueleza msimamo wetu kama Kambi ya Upinzani baada ya Serikali kuyakataa baadhi ya mapendekezo yetu. Serikali haikukubaliani nasi kuondoa sitting allowances (posho ya vikao),"alisema Mbowe na kuongeza: "Sisi tunaamini kuwa viongozi wanaopaswa kusafirishwa kwa ndege katika daraja la kwanza ni Rais na mke wake, Makamu wa Rais na mkewe, Waziri Mkuu na mke wake, Spika wa Bunge na mwenza wake. Halafu mawaziri wanapaswa kusafiri kwa daraja la kawaida na wabunge wote," Barua ya Chadema haijafika Ofisi za Bunge "Siwezi kufanya kazi kwa taarifa za vyombo vya habari. Mbowe hajanipa gari wala sijapata barua ya wabunge kukataa posho. Mambo hayo yapo kisheria muulizeni (Mbowe) kanipa lini gari hilo?"alihoji Bunge kuendelea kuwalipa posho Aliendelea"Mbunge anapewa posho kama sharti namba 3. Sasa kusitisha posho hizo ni mlolongo mrefu ambao hauwezi kufanyika kwa haraka kiasi hicho. Kinachoweza kufanyika, ni kila mbunge anayetaka kutochukua posho kuniandikia barua na sio kama kambi kwa sababu posho hizo ni za mbunge." Akishaniandikia barua, alisema " Kuna njia mbili; moja ni mimi kumpa posho yake halafu yeye airudishe serikalini au mimi niikatie risiti halafu niirudishe serikalini, lakini haiwezi kupelekwa kwingine kokote zaidi ya kuwapa wabunge wenyewe." Joel alipuuza madai ya kambi hiyo kutaka kuwe na fomu mbili bungeni; kulipana posho bungeni na fomu ya mahudhurio ili wao wasaini fomu ya mahudhurio tu, wasipewe posho hizo, akisema "Fomu iliyopo ni ya mahudhurio, wanataka fomu gani sasa? Lissu adai Mbowe alirejesha shangingi … apongezwa kwa kurudisha shangingi “ Uingereza nchi tajiri, lakini mawaziri wake wanatembelea vigari vidogo vinaitwa Austin, lakini sisi na umaskini wetu mawaziri wanatembelea magari ya kifahari,” alisema Mtikila na kuongeza. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Dk Benson Bana alisema, Mbowe ana hoja ambayo inapaswa kuungwa mkono na watu wengi wenye kuitakia mema nchi hii. Naye Shaaban Mtawa, fundi wa magari wa Kinondoni jijini alisema kitendo cha Mbowe kurudisha gari hilo kimemfurahisha na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano huo. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kinachofanywa na Mbowe ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumpatia umaarufu. “Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amepewa gari kwa ajili ya kazi hiyo, anarudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angefanya hivyo?,” alihoji Mtatiro. |
| Last Updated on Thursday, 23 June 2011 23:38 |



Kizitto Noya, Dodoma na Raymond Kaminyoge, Dar











Comments
Hata hivyo nakushukuru kwa kueleza kuwa baadhi yetu waTZ tunamalezi yasiyotusaidia kujua hoja ipi ni hoja ya nguvu na ipi ni ya nguvu ya hoja!!
Mbona hawa viongozi wanongozwa na jaziba na mjungu kama huyo spika ni roboti tu hakuna nachofnya hapo zaidi ya kufanya anachoambiwa na wazee.
Paka tuanze kujilipua wenyewenywe ndio mtaona tumechoka u[NENO BAYA] wa wenu mafisadi
Shida ya watu wengi kama wewe ni malezi. Malezi yetu waafrika yanatuongoza ktk manung'uniko na malalamiko pasipo kuwa na matendo. Sikuelewi unaposema kuwa kazi ya upinzani ni kutoa bajeti mbadala na kukaa kimya kusubiri uchaguzi ujao. Angalia mabunge ya wenzetu jinsi nguvu ya upinzani inavyochochea maendeleo. Bila kutumia nguvu ya umma hiii hali ya viongozi kuwa walaji wa fedha za umma haitamalizwa kwa majadiliano. Kuna mambo ambayo hayawezi na hayatakiwi kusubiri uchaguzi.