MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
SAKATA LA RADA:Kina Ndugai wataka kina Chenge washitakiwe  Send to a friend
Tuesday, 05 July 2011 21:02

Leon Bahati, Dodoma
TIMU ya wabunge walioenda nchini Uingereza kufuatilia malipo ya rada kwa Serikali ya Tanzania imekabidhi ripoti yake kwa Spika wa Bunge inayopendekeza mambo mawili, ikiwamo kushtakiwa kwa wahusika wa sakata hilo hapa nchini.Timu hiyo ya wabunge wanne ikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ilimkabidhi ripoti hiyo kwa Spika Anne Makinda jana mchana.

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Angellah Kairuki (Viti Maalumu-CCM), Mussa Zungu (Ilala-CCM) na John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP).

Kwa nyakati tofauti, wabunge hao waliwaeleza waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa imegundua madhambi ya kutisha katika sakata la ununuzi wa rada hiyo ya kijeshi yanayoweza kuwatia hatiani wahusika.

Ingawa wajumbe hao hawakuwataja watuhumiwa hao kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), ni mtuhumiwa namba moja na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk Idrisa Rashid.

Wakati wa uchunguzi wa sakata hilo, Kampuni ya SFO ilibaini zaidi ya Dola za Marekani 1.2milioni kwenye akaunti ya Chenge iliyoko katika kisiwa cha Jersey nchini Uingereza. Lakini alipohojiwa na waandishi wa habari, Chenge alisema 'hivi ni vijisenti tu'

"Miongoni mwa mapendekezo yake (ripoti) kwa Serikali ni kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote waliohusika kwenye ufisadi huo," alisema mmoja wa wajumbe wa timu hiyo.   

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa imeweza kufichua mlolongo wa kashfa na njama ambazo zilitengenezwa nchini Uingereza ili kufunika uovu huo ambao ni wizi dhidi ya fedha za Watanzania.  

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, timu hiyo ilisema, mbali na kupendekeza wahusika katika sakata hilo washtakiwe, walitaka pia Bunge na Serikali kushirikiana kwa karibu hadi fedha ambazo Tanzania inazidai kutoka Kampuni ya BAE System, zipatikane.

Cheyo, mmoja wa wajumbe wa timu hiyo, hakuwapo katika mazungjmzo hayo na waandishi wa habari jana.

Wabunge hao walisema katika safari yao wamegundua mengi ikiwa ni pamoja na namna uovu huo wa kifisadi ulivyozimwa ili dunia isifahamu.

Angellah alisema kuwa timu hiyo ya wabunge ilibaini pia kuwa Serikali ya Tanzania ilikuwa imekatazwa na SFO isiwachukulie hatua watuhumiwa wa hapa nchini kwa sababu ingekuwa ni mwingiliano wa kesi mahakamani.

Alisema kwa sasa ambapo tayari mahakama ya Uingereza imetoa hukumu, Tanzania iko huru kuwachukulia hatua wahusika. Pamoja na hali hiyo, alisema nguvu kubwa kwa sasa ielekezwe katika kuiwezesha Tanzania kupata fedha hizo bila mizengwe.

Alisema kama Serikali ya Tanzania inataka kuwashtaki inapaswa kupata pia ushahidi wa SFO ambao waliutumia kuibana BAE hadi ikaamua irejeshe fedha zote.

Kuhusu uwezekano wa kuwaunganisha maofisa wa BAE kwenye kesi hiyo, Ndugai alisema kuwa tatizo ni kwamba waliohusika kwenye mpango huo tayari wameondolewa kwenye kampuni hiyo.

Zungu alisema mkakati wao ni kwamba iwapo kampuni ya BAE haitatoa fedha hizo hadi Desemba mwaka huu, Serikali ya Tanzania ifungue upya mashtaka nchini Uingereza.

Kwa upande wake, Ndugai alianza kwa kuelezea lilikoanzia sakata hilo, akisema: "kama mnavyojua Desemba 20 mwaka jana mahakama nchini Uingereza ilitoa hukumu ambayo iliiadhibu kampuni ya BAE kulipa fidia ya paundi 29 milioni kwa Tanzania."

Alisema Kampuni ya Kuchunguza Rushwa kubwa kubwa nchini Uingereza ya (SFO) ndiyo iliyofungua mahakamani kesi hiyo.   Ndugai alisema kwa kuwa BAE ilibaini kuwa shtaka hilo lilikuwa ni zito na lingeweza kuharibu sifa ya kampuni hiyo duniani, walifanya mpango wa kesi hiyo kuzungumzwa nje ya mahakama na kufanikiwa.

Wakiwa nje ya mahakama, Ndugai alisema BAE walitengeneza mkataba na kusema kwamba watarejesha fedha zote ambazo Tanzania ilinunulia rada hiyo pamoja na fidia.   

"Yaani walifanya kana kwamba rada hiyo Tanzania imepewa bure. Maana walinunua kwa pauni 28 milioni na sasa wanatoa pauni 29.3 milioni," alisema Ndugai. Alifafanua kuwa mkataba huo ulikuwa ni wa kufunika aibu na uliandikwa na mwanasheria wa BAE huku ukieleza kuwa fedha hizo zitatolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili yatoe huduma za kijamii.

Alisema hata kabla kesi hiyo haijaenda mahakamani, walitoa mapendekezo ya fidia itakayopatikana iletwe nchini ili kununua madawati na kujenga nyumba za walimu kwa kuwa waathirika ni Watanzania.

Baada ya makubaliano hayo ya nje ya mahakama, Ndugai alisema SFO na BAE walikubaliana kesi iliyoko mahakamani ijulikane kuwa ni ya kosa la kushindwa kuweka vizuri kumbukumbu.   

Alisema SFO na BAE wakaingia mkataba wa kufunga faili la uchunguzi kuhusu kashfa hiyo ikiwa na maana kwamba uozo uliofanyika hautatolewa kwa namna yoyote kwa chombo chochote.   

Ndugai alizidi kueleza kuwa hii ni njama kati ya SFO na BAE ya kutotaka madhambi yaliyofanywa katika ununuzi huo wa rada yasiwekwe hadharani na dunia ikafahamu.   

Hata hivyo, Ndugai alisema kamati yake imegundua ujanja huo na kwamba kitendo cha kusema fedha hizo ziende kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kuisaidia jamii, ni njia ya kuzitumia wao wenyewe.

"Wao wanataka ionekane BAE wametoa msaada halafu wafanye safari za kuja nchini kwa ndege na walipane posho halafu mwisho wa siku fedha nyingi watatumia wao," alilalamika Ndugai.
 
Ndugai alisema fedha hizo zitolewe kwa Serikali ya Tanzania na zisimamiwe na Bunge katika kutengeneza madawati na nyumba za walimu na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) aweze kuzikagua.   

"Zikitolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, CAG hataweza kuzikagua na hata matumizi yake yakipindishwa hakuna namna ya kuwabana wahusika," alisema Ndugai.   

Akizungumzia kuhusu safari yao ya Uingereza, Zungu alisema walichogundua ni kwamba BAE ilifanya mchezo mchafu kuanzia ununuzi wa rada hadi kuficha madhambi yake kwa kutaka kesi izungumzwe nje ya mahakama.


Taarifa zao kuvuja
Alilalamika  kuwa hata baadhi ya wabunge wa upinzani waliozungumzia suala hilo juzi, ilitokana na kuvuja kwa taarifa za ripoti yao.   

Hakumtaja mbunge huyo wa upinzani, lakini John Mnyika ndiye aliyeliambia Bunge kuwa fedha hizo zisipelekwe serikalini kwa sababu walishindwa kuzisimamia na wala hawakuomba washirikishwe kwenye kesi hiyo.   

Zungu alilalamika kuwa miongoni mwa lawama dhidi ya SFO ni kutoshirikisha Tanzania kwenye kesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa iliwasiliana na Takukuru ili kupata ushahidi ambao uliisaidia kuibana BAE.
 

Lakini akamsifu Jaji aliyeamua kesi hiyo kwa sababu alisisitiza kuwa dhuluma hiyo ilikuwa ni dhidi ya wananchi wa Tanzania hivyo lazima fedha hizo zipelekwe moja kwa moja kwa manufaa ya waathirika hao.  

Zungu alisema kuwa Jaji aliamua itozwe fidia ndogo ya paundi 500,000 katika fedha hizo ili zigharimie kesi hiyo.

Zungu alionya kuwa kama mshikamano hautakuwapo katika suala hilo, BAE itatumia fedha za Watanzania na kujigamba imetoa msaada.

Alisema katika Bunge la Uingereza, Tanzania inasifiwa kuwa imekuwa ikitumia vizuri fedha za misaada na wanaridhika iendelee kupewa misaada.   

"Sasa kitendo cha kutoa fedha hizi, zilizotoka mikononi mwa Serikali ziende kwa asasi za kiraia kwa madai kwamba hazitatumika vizuri ni udhalilishaji mkubwa," alieleza Zungu.

Alisema kamati hiyo ilipanga kukutana na Mkurugenzi wa SFO, Richard Agaman, lakini alikataa huku akisema yuko tayari kuwasiliana na balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Zungu alisema balozi huyo alisema mkurugenzi huyo wa SFO aliomba radhi kwa kutoshirikisha Serikali ya Tanzania kwenye kesi hiyo.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 07 July 2011 00:20
 

Comments 

 
0 #83 2011-07-06 22:54
Jamani tunachotakiwa kufanya ni kuwaelimisha watanzania kwa ujumla wao
kuwa TANZANIA BILA CCM inawezekana.Ndani ya ccm kuna mambo mengi machafu(YANANUK A).Aduinamba wa Nchi hii ni CCM na SERIKALI YAKE
Quote
 
 
0 #82 2011-07-06 22:36
Serikali tuliyonayo imeishiwa aibu yaani mwizi kaiba kakamatwa na kizibiti,kwa kuwa tabia yao ni kulindana wanadai bado wanafanya upelelezi kwa kuwa tu wamekula wote. kwanza ni waporaji wa haki ya wananchi la sivyo Chenge na genge lake wangekuwa tayari wameshughulikiw a. Hatuna Serikali ya Wananchi ila yao wanolindana.
Quote
 
 
0 #81 2011-07-06 22:08
Fedha(change) za radar zipelekwe NGO au Sudan Kusini kwani TZ imeshindwa kukubali kuwa ufisadi ulitumika ndiyo maana wahusika mpaka leo ni waheshimiwa katika bunge la Tanzania. BAE (na UK kwa vingine) wako sahihi.
Quote
 
 
0 #80 2011-07-06 20:50
WAZIRI CHIKAWE ALIPEWA MGAWO WA RUSHWA YA RADA NDIO MAANA ANITETEA SANA IL KUSUDI WASIJE WAKASULUBIWA ,YEYE PAMOJA RAFIKI ZAKE AKINA CHENGE NA KIKWETE.
KUMBUKA KUWA ENDAPO KAMA CHENGE ATASULUBIWA MSALABANI HATA KIKWETE NAYE HAPONI KWANI YEYE ALIKUWA WAZRI WA MAMBO YA NJE KWA HIYO ANALIJUA SAFI SAKATA LOTE LILIVYO PIA ALIPATA MGAWO KTK UNUNUZI WA ILE RADA,NDIO PESA ALIYOFANYIA KAMPENI YA URAIS MWAKA 2005,KWA HIYO LAZIMA WAMTETEE CHENGE
Quote
 
 
0 #79 2011-07-06 20:37
Quoting Alexander:
Wewe Ahmed00 na Beano, Mnajifanya mna uchungu sana na nchi hii, Mnajifanya wazaleeeeendo! hamna lolote ni walewale tu, Mnaipamba sana Chagga Dev. Manifeto. Nendeni huko mkapewa ubunge wa viti maalumu mpate sitting allowances, mzigomee kwa kutafuta umaarufu.

And you?
Quote
 
 
+1 #78 2011-07-06 20:36
Quoting Mohammed tolawaka:
BAE ni wezi wajanja... wameshatakatifi wa sasa wanataka wazichukue kiujanjaujanja... Hapo hapana

"Wao wanataka ionekane BAE wametoa msaada halafu wafanye safari za kuja nchini kwa ndege na walipane posho halafu mwisho wa siku fedha nyingi watatumia wao," alilalamika Ndugai.
YAANI WEWE UPO KAMA DUME LA NJIWA, UMESIKIA NDUNGA IIII KASEMA HIVYO NA WEWE UMEMSAPOTI UONEKANE NAWE UMESEMA. HUO UNAITWA USEEEEEEEEEE NGE WA MCHICHA WA MIIBA UKIENDA VIBAYA UNAKUCHOMA UKIENDA VZR UNAUCHUMA UTAUPIKA NA TUI LA NAZI UTAWEKA. YAANI CCCM WAMESHAJUA KWAMBA WAZUNGU NA WAO WATAGAWANAA POSHO SHINGO ZIMEWAKAKAMAA WANAONA ULAJI UNAWATOKA WA SE NGE SANA NYIE NA NYUMBA NDOGO ZENU.
Quote
 
 
0 #77 2011-07-06 20:12
Quoting Alexander:
Wewe Ahmed00 na Beano, Mnajifanya mna uchungu sana na nchi hii, Mnajifanya wazaleeeeendo! hamna lolote ni walewale tu, Mnaipamba sana Chagga Dev. Manifeto. Nendeni huko mkapewa ubunge wa viti maalumu mpate sitting allowances, mzigomee kwa kutafuta umaarufu.

you sounds like a little baby
Quote
 
 
0 #76 2011-07-06 19:52
Hi serikali ya kikwete imebakia kama ndoto za alnacha.kila kukicha kuna brand new story huwezi kuamini kama ni serikali iliyoingia kwa mbwembwe.Hatuna imani na kikwete-please ondoka umeshindwa.hatuana bunge,hatuana raisi wala mahakama mihimili yote iko ICU.
Quote
 
 
+1 #75 2011-07-06 18:38
WAZIRI CHIKAWE HUWEZI KUSEMA TU KUWA CHENGE HAUSIKI KWA KUWA NCHI HII INAONGOZWA KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA MNAVYODAI BASI IACHIE MAHAKAMA NDIYO ITAMKE KUWA HAUSIKI NA SIYO WEWE KUJIFANYA NDIO MAHAKAMA NAKUBALIANA NA WOTE WANAOSEMA KUWA HAPA ANAYELINDWA SIYO CHENGE TU BALI MKAPA NA GENGE LAKE.
Quote
 
 
0 #74 2011-07-06 17:24
Kwa ni ninavojua Chenge atakuwa amezimalizia kwa totoz! Mzee wa vijisenti nuksi! usu[NENO BAYA] wake hauchagui weupe au weusi, yeye kila sketi twende tu! Halafu jamani misu[NENO BAYA] mijing a! Angalia hili la CHADEMA (Si BUDA!) linavyobwata hovyo! Eti ngosha anajifanya anajua kiswahili kuliko Shaaban Robert! Ushamb atu! Akili imedumazwa na kuchambua pamba chafu! Nyerere aliibaini mapema hakuipa nafasi; ilikuwa inadai yenyewe almasi, dhahabu na pamba ni zao! Eti Lake Victoria ni yao! Mzee wa Butiama aliwafinyanga wakakoma ubishi! Wao na treni, treni na wao mpaka waliposalimu amri!
Quote
 
 
+1 #73 2011-07-06 17:14
Kina Ndugai acheni kutuzuga! Huy Zungu si ndo wenyewe mandai anauza dawa za kulevya? He! Fisi kapewa sufuria ya pilao apike si maharusi watalala njaa! Kuongozana na mtuhumiwa wa madawa ya kulevya kumevunja sifa ya hiyo timu iliyokwenda huko! Halafu Chenge si mko naye mjengoni miaka nenda miaka rudi? Mbona hamumtimui ili tujue mna uchungu wa kweli? Ndio kwanza mkikutana nae mnajipendekeza pendekeza! Angalia mzee mapesa kawakacha maana huyo ni ngosha mwenzie! hataki hata kumzungumzia! Kabana kimyaa mzee wa minoti! naye jambawaz i kama chenge! Kwanza ofisi ya chama kahamisha nyumbani kwake au bado ipo pale sitting room!? Ndugai, pesa hamtapewa ng'o kwani hamkubani kuwa hukumu haijasema ni fidia? Hiyo ni hisani tu a BAE na wanaweza kumpa yeyote wakishakubalian a na SFO! Danganyanyeni! Mpende msipende zitaenda NGOs! Eti zitatumika vibaya na hakuna jinsi ya kuadabisha! sasa huko kwenye uadabishwaji zilitumika vizuri? Mbona hawajadabishana hali sasa ndo mnataka waadabishwe?! Acha zikaliwe na NGOs kwani nao ni watanzania masikini! Angalau masikini wa NGO watanufaika kuliko nyie nya ng'au! Faflukti kaput!
Quote
 
 
0 #72 2011-07-06 16:33
Jamani nawaombeni sana wana ccm wenzangu tuwe na uchungu na nchi yetu,hasa wabunge kwanini kila kitu NDIYOOOOO,wengi ne ni bendera fuata upepo,mnaitetea serikali hata kwenye uozo.nawewe spika siyo kupitisha kila hoja,sijawahi kukusikia ukiwapa nafasi kwa wanao sema siyoooo.unatumia kipimo gani?
Quote
 
 
+1 #71 2011-07-06 16:29
wabunge wa ccm ni kama mwanamke anayemuogopa mumewe akisikia mume wake kaongea anaitikia hata kama hajitwa wanatabia za kike za woga wanaona wakisema wa[NENO BAYA]sa mlo haiwezekani wewe mbuge unalalamika jimbo lako lina njaaa shida ya umeme ajira halafu mwishoni unaunga hoja huo ni u[NENO BAYA] unadhani watanzania ni [NENO BAYA] kiasi hicho na ngojeni murudi this time mtajuta kuzaliwa muulizeni masha na diallo watawaambia nini kiliwakuta.acheni ubwanyenye mlichobakiza tu ni kuinamishwa na hao ambao mnawaogopa kwa mmekalishwa hapo kazi ni kuitikia ndiooooooo halafu kina chenge ,lowassa,rostam na baba ridhiwani wanapiga deal mnabaki kupiga makofi hamuoni mnadhalilishwa majibaba mazima yamekwenda bungeni kupigia wanaume wenzao makofi na kuwatetea walifilisi hili taifa.tafakari
Quote
 
 
+2 #70 2011-07-06 16:21
wajameni huuu ni mchezo wa kuigiza kama bunge lao la ngonjera,tume zilizoundwa tokea mimi nimekuwa na akili mpaka leo hii ni nyingi mno. tumeunda tume ya kudai pesa ambazo viongozi wetu wenyewe wamehusika kuzipiga na pesa zinaendelea kupotea tu watanzania wana maisha magumu lakini wanaojali katika hilo bunge ni wachache sana. waliobaki hasa hao wa kijani wasiojua nini wafanyalo hapo bungeni ndo wanaoliteketeza hili taifa .wahusika hata mmoja hakuna aliyefikishwa mahakamani wanacheza mchezo wakuigiza kwa kuona watanzania wote ni [NENO BAYA] ila iko siku tuuu wasipolipa wao watalipa watoto wao hata wajukuu.mmesikia ya mwanza leoooooo mambo yameanzaaaaaaa
Quote
 
 
0 #69 2011-07-06 16:11
Hata mseme mimi nimekula mapesa na vijisent senti nivyakununua vipodozi tu..hahaaaaaaaa
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner