
| Rostam, Mkapa kuungana kampeni za CCM Igunga | Send to a friend |
| Tuesday, 30 August 2011 22:02 |
|
ALIYEKUWA Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ni miongoni mwa makada watakaotumiwa na CCM katika kampeni za kumsaka mrithi wake katika jimbo hilo.Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) kilichokutana juzi, Ikulu Dar es Salaam zinasema Rostam amepangwa kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za CCM zitakaofanywa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Septemba 10, mwaka huu."Labda ratiba ibadilike, lakini ni kweli Rostam amepangwa kwamba ataambatana na Mzee Mkapa kwenda Igunga na yeye atabaki huko kama wiki moja hivi kusaidia kampeni hizo," alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu hiyo ya CCM. Mjumbe huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema Rostam amepangiwa kwenda Igunga mara tatu: "Baada ya hapo atarudi tena katikati ya kampeni na pia atarudi tena wakati wa hitimisho." Uamuzi wa CCM kumtumia Rostam katika kampeni zake za Igunga unatafsiriwa kuwa hatua ya kutafuta kuungwa mkono na wakazi wa jimbo hilo ambao "walikasirishwa" na kitendo cha mbunge wao huyo kujiuzulu kwa kile alichokiita "siasa chafu." CCM kinakabiliwa na makovu huko Igunga yaliyotokana na kujiuzulu kwa Rostam ambaye wakati akitangaza kujiuzulu alitamka bayana kwamba uamuzi wake huo ulitokana pamoja na mambo mengine, wanasiasa uchwara wanaoendesha siasa za kupakana matope baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kutangaza mpango wa kujivua gamba. “Nimepata msukumo wa kuamua kuachia nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama, nikianzia na ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nikiuwakilisha Mkoa wa Tabora na hii ya ubunge wa Igunga ambazo kama si kwa baraka za chama changu, nisingelikuwa nazo," alisema Rostam siku alipotangaza kujiuzulu na kuongeza: “Napenda kuliweka hili sawasawa. Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM, haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu." Rostam sasa anatarajiwa kushiriki kampeni hizo, akimpigia debe mgombea wa CCM, Dk Dalaly Peter Kafumu aliyepitishwa na CC ya chama hicho juzi. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu ushiriki wa Rostamu katika kampeni za Igunga alisema: “Rostam ni mwanachama wa CCM na chama kimetoa mwaliko kwa wanachama wake kushiriki kampeni hizi, hivyo hilo labda ajibu mwenyewe lakini kama mwanachama ana haki ya kushiriki.” “Labda niseme hivi, ukiachilia mbali watu kama Mzee Mkapa ambaye atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi, hatukupeleka mwaliko kwa mtu mmoja mmoja, ila tuliwaalika wanachama wetu kusaidia kampeni hizi, kwa hiyo Rostam akiwa mwana CCM ana haki ya kukipigia kampeni chama chake.” Nape pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), John Chiligati walitajwa na Rostam wakati akijiuzulu kwamba ndiyo waliopotosha dhana ya kujivua gamba kinyume cha uamuzi wa NEC. “Walisikika wakitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuwa imefikia uamuzi wa kuwapa siku 90 wale walioitwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama kujitoa katika nafasi zao za uongozi vinginevyo watafukuzwa na chama," alisema Rostam. Hata hivyo, Rostam hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwani alipopigiwa simu yake ya kiganjani hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi alijibu kwa kifupi: “in a meeting, baadaye” akimaanisha kwamba alikuwa kwenye mkutano. Juzi, Nape akitangaza uteuzi wa Dk Kafumua alisema: “Katika kufanikisha kampeni za CCM wanachama waliowania kuteuliwa katika nafasi hiyo wameahidi kuwa watashiriki kikamilifu katika kampeni hizo.” Alisema hata wagombea wengine wa chama hicho katika kura za maoni wameahidi kuwa watamuunga mkono Dk Kafumu ambaye aliibuka mshindi kwa kupata kura 588. Hao ni pamoja na aliyemfuatia kwa karibu, Jafari Omari aliyepata 193 na Shams Brahamu aliyepata kura 38. Katika uchauguzi huo wanachama 13 wa CCM waliomba nafasi hiyo. Nape alisema CCM kitashinda kwa kuwa kina mizizi imara iliyojikita katika vitongoji vyote vya jimbo hilo, tofauti na vyama vya upinzani... “CCM ipo Igunga wakati wote (wa uchaguzi na usio wa uchaguzi). Vyama vya upinzani huonekana kule wakati wa uchaguzi.” CCM waunda timu nne Katika kuhakikisha kinashinda uchaguzi huo mdogo, CCM Wilaya ya Igunga kimeunda timu nne maalumu, ikiwamo ya wafanyabiashara maarufu watakaohakikisha kwamba mgombea wa chama hicho, Dk Kafumu anashinda. Hatua ya kuunda timu hizo inatokana na chama hicho ngazi ya taifa kutangaza kuwa majukumu yote ya kupanga na kuendesha kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu, zitasimamiwa na CCM Wilaya ya Igunga. Katibu wa CCM Wilaya ya Igunga, Neema Adam alisema jana kuwa tayari wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya vyama vitano vya upinzani vilivyosimamisha wagombea. "Kimsingi uchaguzi unasimamiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya. Hivyo wajumbe wote wa kamati hiyo wataratibu shughuli zote za kampeni," alisema Neema lakini akidokeza kuwa kamati hiyo itasaidiana na timu nyingine tatu. "Mbali na kamati hiyo, wafanyabiashara maarufu 20 hapa Igunga, wameunda timu itakayosaidiana na wanachama wa CCM kufanikisha kampeni hizo. Vilevile kila tarafa ina timu ya watu wanne na kila kata watu 10. Kwa hivyo ukiangalia utaona kuwa tumejipanga vizuri katika kuhakikisha tunapata ushindi." Wagombe wengine ni Joseph Kashindye wa Chadema, Moses Edward (TLP) na John Maguma wa SAU na Leonard Mahona wa CUF. Uchukuaji fomu ulimeanza Agosti 24 na unatarajiwa kukamilika Septemba 6, mwaka huu. CUF nayo yatamba Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema wamejipanga kikamilifu kukabiliana na CCM kwenye kampeni zijazo.Alisema wakati wa kampeni chama chake kitalipua siri zilizofichuka dhidi ya kiongozi yeyote wa CCM atakayefika Igunga, akiwamo Rais Mstaafu, Mkapa. Katika kampeni hizo, Mtatiro alisema wataweka hadharani sababu ambazo wapiga kura wanapaswa kuzizingatia na kutoichagua CCM na badala yake kumchagua mgombea wa CUF. Alisisitiza kuwa CCM wajiandae kukabiliana na maswali mengi ambayo watashindwa kuyajibu mbele ya wakazi wa Igunga. |
| Last Updated on Thursday, 01 September 2011 00:05 |















Comments
nimeamua kutumia siku kuu ya leo kwenda bagamoyo kupata upepo wa bahari ya hindi. nimeogelea na kufaidi breezes. siyo siri nimepunguza msongo kichwani!
bahari ni rasilimali yetu! tuitumie angalau siku mojamoja. panapo majaliwa vile nimerefresh mind kuanzia kesho nitachangia kwa ueledi, ufasaha, ukweli, uhakika, uwazi, uzalendo bila kusahau uono wa mbali!
alamsiki!
Nafikiri tutabishana mpaka Asubuhi bila kufahamiana, ni kitu akiwezeni kabisa Qatari kutuma ndege bila idhini ya wahusika nakama hivyo ina maana hata JK anaweza kubebwa ikuru bila watu kujuwa keti ujuwe kabla ya ndege kutuwa kuna mambo mengi kufataiwa vibari na usalama wahiyo ndege kutua. kwahapo inaonekana wazi wewe unachuki zako binafsi.
Tunafahamu na kila mtu anafahamu Tanzania ina rasimali nyingi sana lakini faida nini wakati budget ya kutembeza kopo na watu wake duni.
Kitu cha msingi ni kutatuwa matatizo "nafikiri sijuwi kama unajuwa Tanzania hipo huru au ime tawaliwa bado na kama hipo huru itakuje watu wachukuwe hivyo vitu bila serikali kujuwa" mimi nahisi wewe sio mtanzania na kama Mtanzania labda uliondoka kabla uhuru ndio maana akiri ina asasiya ya kikoloni.
There you go again! Kama kuna kitu unanishangaza Zaim ni kutofahamu umuhimu wa National Pride. Kama Taifa, Tanzania ina mipaka na inalindwa. Tuna mambo ya ndani na yapo mengine tunawahusisha wa nje na hayo ni kwa urafiki. Ikifikia hatua nchi nyingine kuleta ndege ya jeshi lake ndani ya ardhi yetu kuja kufanya smuggling kuna mambo mawili ya kuzingatia:
-kwanza dharau. Haiwezekani ndani ya territory yetu yafanyike mambo ya ajabu namna ile halafu wenyewe tuwe kimya as if its normal transaction. Kitendo cha Qatar kuthubutu kushiriki wizi ndani ya ardhi ya Tanzania, hakuna urafiki tena hapo.
-La pili ni usalama wa taifa letu. Kama watu wanaweza kuleta ndege, halafu jeshi liseme halijui kama ilikuja hapa ni dhahiri next time wanaweza tuma spies kutukagua na tusijue.
Kama una hakika kuwa tuna desturi wa kutoa wanyama kama zawadi basi naamini kuna utaratibu wa kufanya jambo kama lile na kamwe si gizani. Na lingine la wewe kuzingatia kama wewe ni Mtanzania (Japo kwa namna yako ya lugha tayari nahisi una aili ya Asia) ni kwamba misaada si hongo. Ni upotofu kufikiri kuwa tuna sababu ya kuvumilia kila tutakachofanyiw a na mwingine kwa kuwa aliwahi kutusaidia kipande cha barabara. Mikopo na misaada ni makubaliano ambayo hayatufungi kukubali mambo mabaya na ndio maana (kama unafuatilia habari) jana uliona Balozi wa Japan akiomba radhi kwa Tanzania kwa kuwa barabara waliotusaidia kuijenga hawakuijenga kwa kiwango tulichokubalian a na kudhihirisha kuwa tuna msimamo kama Taifa Waziri Magufuli alikataa kuipokea hiyo barabara mpk itakapokuwa ktk kiwango tulichokubalian a.
Kama Mtanzania, Mzalendo na mzawa wa nchi hii, nakataa maneno yako kuwa nchi yetu ni maskini. Barrick wanafakamia dhahabu zetu na kuzipeleka nje ya nchi ktk mikoa kadhaa na wengi mpk wafilipino wankuja kuwaiba hlf we unaitukana nchi yetu na kumkufuru Mungu!
Tanzania si maskini, Watanzania ndio maskini. Na umaskini wa Watanzania unaletwa na CCM sababu ya ulafi na ufisadi wao. Wamekuwa radhi kutoa kontela la dhahabu kwa mzungu ili mifukoni mwao iingie nusu kilo kwa ajili ya familia zao.
Pamoja tushirikiane kuondoa gonjwa hili linalonyong'onyeza maendeleo ya taifa letu ili Tanzania ipige hatua na ndugu yangu Zaim aishi kwa amani akijua kuwa hatudaiwi na tuna haki ya kudai Twiga wetu
Huyu Mkapa anaheshimika kwa lipi? nae ni fisadi kuliko hao waliopo madarakani hivi sasa, hebu ndugu jiulize ni rasilmali ngapi alizojimilikish a huyu fisadi? Anaheshimika kwa lipi zaidi ya kuudidimiza upinzani katika utawala wake? Anaheshimika kwa lipi zaidi ya kuwatukana wasomi kwa kuwaita wasomi uchwara? Huyu nae ni fisadi na ndio maana anajipanga kuwapigia debe mafisadi wenzake(CCM)
Wana Igunga amkeni wacheni kumsikiliza huyu fisadi (Mkapa) kwani katika kipindi cha utawala wake wote hana alichowafanyia, msiendekeze kabisaa kauli za mkapa wala fisadi yeyote wa CCM.
Ndugu tupo hapa kutetea maslahaa ya nchi yetu nafikiri ujanielewa na maana gani keti ufahamu umesema jambo nzuri sana kuwa unao rafiki zako wa asia na wazungu, mfano leo hi rafiki zako wakisikia unashutumu sana kwa mtanzania mwenye asiri hizo hata hisi vipi? kitu muhimu my opinion tusiingize ubaguzi au kutaja kwa vibaya kabila ya mtu sababu sijaona mtu kasema wewe chenge au lowassa kabila fulani ndio maana fisadi na pakifikia hapo
kila mtu ataanza haa kumbe Beano kabila yake na chenge sawa basi naye fisadi na ndio utakuwa mwanzo wakukatana mapanga nafikiri ushanielewa "what's mean.
Nakuhusu Twiga, Tanzania toka kupata uhuru tumeuza au kugawa zawadi mamia ya twiga nimeeleza sio busara kwenda kudai warudi.kitu cha muhimu ne kujuwa wametoka vipi au kwa maslaha yapi sio kutupia lawama bila kujuwa undani wake.
Keti ujuwe nchi yetu ni duni sana tukifunguwa Dispatch book kujuwa vitu vilivyotoka hapa nchini nawao wafenye hivyo wangalie madeni na misaada walitupa tuludishe naona hata tukiwapa panya na wanyama wote awatoshi kulipa madeni tulikuwa nayo.
Kitu muhimu sisi kufanya mabadiliko tumechoka uongozi wao miaka 50 bila maendeleo
KUKUBALI WITO WA WEZI WENZAKE WAKATI WALIMTIMUA,TUNA HOJI CCM WAMEMPA BEI GANI? AIDHA PIA TUNAJIULIZA CCM NA.1 AKA GAMBA, WAMESHINDWA KULIREJESHA JIMBO? TUNAWAOMBA WAPINZANI IGUNGA CHUKUENI JIMBO,TUNAJUA CCM HAWAKUBALIKI NA NDIO MAANA WANAMTUMIA ROSTAM NA ROSTAM ALISHINDA KWA RUSHWA! 2015 NI CHADEMA TENA BADLA YA USHINDI WA 65% WAKAPIGA CHUA-TUTAPIGA 80%