MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Vigogo UVCCM wajiuzulu  Send to a friend
Tuesday, 18 May 2010 23:38

**Ni mwenyekiti na naibu katibu wake
JOTO la kisiasa ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM sasa limefikia nyuzi 100, baada ya Mwenyekiti   wake Hamad Yusuf Masauni na Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo visiwani Zanzibar, Nassoro Moyo, kuamua kujiuzulu. 
 
Ramadhan Semtawa, Dar na Leon Bahati, Iringa
 
Tangu juzi, vijana hao wa CCM wamejichimbia mjini Iringa kwa ajili ya mkutano huo muhimu wa baraza kuu, ambao ulitanguliwa na semina na kamati ya utekelezaji lakini ukiwa umegubikwa na msuguano ambao unakiweka chama katika wakati mgumu katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. 
 
Kabla ya kwenda Iringa, tayari wajumbe walishaingia kwenye vita baada ya kusambazwa waraka uliokuwa ukimtaka Masauni ajiuzulu huku wajumbe wengine kutoka kambi ya mwenyekiti huyo nao wakimtaka Moyo aachie ngazi.
 
Hadi jana jioni, hali ilikuwa ni ya wasiwasi baada ya kufanyika kikao cha kamati ya utekelezaji ambacho inaelezwa Moyo aliandika mwenyewe barua ya kujiuzulu kwa maslahi ya umoja huo.
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Moyo aliandika barua hiyo ikiwa ni sehemu ya kunusuru jumuiya katika kipindi hiki ambacho imekumbwa na mparaganyiko mkubwa.
Wakati wote jioni, ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulikuwa umedhibitiwa vema na polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakishirikaina na wana usalama wengine.
 
Habari zinasema Masauni alijiuzulu saa mbili usiku baada ya kubanwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.
Hali tete ilianza kwenye kikao cha sekretarieti ya umoja huo ambayo iliwajadili viongozi hao wawili kwa muda mrefu, kuliko hata ilivyokuwa imekadiriwa kwa mkutano huo kufanyika.
 
Habari tulizozipata wakati tukienda mitamboni saa 3.00 usiku jana zilisema mara baada ya kumalizika kwa Kamati ya Utekelezaji, Makamba alimwita kwa mara nyingine Masauni na kumshinikiza kujiuzulu. Hata hivyo, vyanzo vya habari  vilisema kuwa hata Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa CCM alikuwa amebariki viongozi hao kujiuzulu.
 
Kutokana kujiuzulu kwa Masauni sasa nafasi itakaimiwa na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa.
Taarifa zaidi zilidai kuwa baada ya wajumbe wa Baraza Kuu kupata habari kuwa Masauni aliamua kujiuzulu wengi wao walionekana wakiwa kimya huku wakitafakari  mustakabali wa jumuiya hiyo.Mkutano huo ulianza saa 2:30 asubuhi na ulipaswa uwe umekamilika kabla ya saa 3:30 asubuhi ili kupeleka ajenda zinazotakiwa kujadiliwa na kikao cha baraza kuu, kwenye kikao kingine cha kamati ya utekelezaji ili zipitishwe.
 
Awali vyanzo vyetu vya habari, vilieleza kuwa kuchelewa kukamilishwa kwa kikao hicho kulitokana na mvutano mkubwa ulioibuka kutokana na pande mbili kupingana, kila moja ikotoa sababu za kutaka mmoja kati ya viongozi hao wawili ajiuzulu.
 
Baraza kuu lilikuwa lianze saa 4:00, lakini kutokana na kikao cha sekretarieti kumalizika saa  6:20, iliamuliwa kuwa kikao cha baraza kianze saa 8:00 na kuwataka wajumbe wajiandae, wakati huo ndipo wajumbe wa kamati ya utekelezaji  wakakutana.
 
Mkutano wa kamati hiyo ulipokea taarifa za sekretarieti juu ya mada za kujadiliwa kwenye baraza kuu na kabla ya kuanza kwa kikao, Moyo aliwasilisha barua ya kukubali kujiuzulu kupisha uchunguzi wa kile kinachoitwa ni kuvuruga chama. Katika tuhuma hizo, Moyo anatajwa kuzusha vurugu ndani ya umoja huo, akidaiwa kushiriki kusambaza nyaraka za kumpinga Masauni.
 
Mvutano mkali pia ulielezwa kuzuka ndani ya kamati ya utekelezaji na hadi saa 12:00 jioni kikao hicho kilikuwa hakijamalizika na taarifa zikawepo kwamba baraza hilo lianze kwa semina ndogo kuhusu mada ya ugonjwa wa Ukimwi ili kuweka sawa mambo.
 
Taarifa nyingine zinadai kwamba, kundi linalopinga Masauni kulazimishwa kujiuzulu   liliibuka na hoja kwamba kuna kundi la mafisadi ambao wanataka aondolewe kwenye madaraka yao ili wamuweke mtu wao ambaye atajenga mazingira mazuri ya ushindi wa rais kwa mwaka 2015.
 
Hadi jana mchana ajenda za kikao cha baraza kuu zilikuwa bado hazijajulikana huku baadhi ya wajumbe, akiwemo Makamba akiachia jukumu hilo viongozi wa jumuiya hiyo.
Makamba alipoulizwa alichukuaje kitendo cha kutojulikana kwa ajenda za mkutano saa chache kabla ya baraza kuanza kikao, alijibu: "Mimi ni mjumbe tu, ajenda wanapanga wenyewe watendaji, muulize katibu mkuu wa UVCCM." 
 
Lakini, vyanzo vingine vilidokeza kwamba juzi usiku Makamba alimtaka Masauni ajiuzulu, hatua ambayo mwenyekiti huyo aliipinga na kutaka kwanza arudi kwa wapiga kura wake akawaeleze.
 
Kuhusu madai kuwa wanachama wanaomuunga mkono Masauni walipanga kuandamana, Makamba alisema:" Kwanza waandamane kwenda wapi? Mimi nasisitiza siwezi kumwambia mtu ajiuzulu kwa tuhuma... halafu wanamtaja na Ridhiwani Kikwete, (mtoto wa rais)... yeye ana mamlaka gani kumshinikiza Masauni ajiuzulu?
"Huku ni kumwonea tu kijana huyu na kutaka kumhusisha katika mambo ambayo hahusiki wala hajatenda. 
 
Waache kumchafua kijana wa watu, sijakuwa naye popote kushinikiza mtu ajiuzulu. Ni uongo mtupu.
 
"Ridhiwan ni mjumbe kama nilivyo mimi; sisi sote ni wajumbe tu ndugu yangu; tuna mamlaka gani ya kumshinikiza mtu ajiuzulu. Waache fitna; waache kumchafua; kijana wa watu hajatenda chochote."
 
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, jana jioni wajumbe 38 wa Baraza Kuu kutoka Zanzibar walitanda eneo la ukumbi wa mikutano wakitaka  kumuona kwanza mwenyekiti wao Masauni akiwa amekalia kiti, ndipo waingie ukumbini.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Wednesday, 19 May 2010 23:15
 

Comments 

 
+1 #52 2011-06-22 12:26
mwisho wa CCM umewadia, huu ni mwanZo wa kufa, SOON TUTAENJOY MATUNDA YA VYAMA VINGI.
Quote
 
 
+3 #51 2010-05-19 21:46
Chadema oyeee; tumia busara chagua mabadiliko ya kweli
Quote
 
 
0 #50 2010-05-19 21:41
Quote
 
 
+2 #49 2010-05-19 21:39
Good God! Wipe out this monster party CCM.
Quote
 
 
-3 #48 2010-05-19 21:38
Hao watu wa CHADEMA msahau kuja kuchukua nchi hii. Kwanza CHADEMA yeneyewe imejaa mafisadi tupu na ndiyo wameona uchochoro wa kujihifadhi. Sahau CHADEMA.
Quote
 
 
+1 #47 2010-05-19 21:29
ukumwangalia tu huyo jamaa unaona kabisa amezidi unga. du this is politics in bongo were we do first then we comeback and regret, surely it is too much for a our small growing economy.
hope the problem we do things because it is a custom and at the end we have no choice. let him go away and another one be incharge
Quote
 
 
+1 #46 2010-05-19 21:25
kama kaghushi sio mwaminifu na hastahili kuopngoza. suala jeeeeeeeeeeeee mkuki kwa nguruwe tu?
Quote
 
 
+1 #45 2010-05-19 19:56
Lowassa ni mtu hatari kwa nchi yetu. Bado kuna mengi atafanya ili awe rais 2015, NI BOSS WAMAFISADI WOOOTE.
Quote
 
 
0 #44 2010-05-19 19:54
Nampongeza sana masauni kwa kujua kuwajibika ili wabaya wake wafanye watakalo kuepusha jumuiya kuvunjika.
Quote
 
 
0 #43 2010-05-19 19:01
Sisi wote tumeshuhudia ufisadi at work. Yep! hakuna Lowassa au nini hizi ni mbinu za CCM mama. Masauni kawekwa for a purpose, wamemtumia na sasa wanamkacha kwa kumtemea mate. Kwani umri wa mtu ni siri? Masauni siyo mhamiaji. Ana ndugu na wazazi na inajulikana mahali, na wakati alikozaliwa. Kulikua na rafu na mchezo mchafu kwenye uchaguzi wa UVCCM na referee Makamba ndiye kinara wa huu ufisadi. Yanawatokea puani. Kwa bahati mbaya Tanzania hatuna upinzani wenye meno. Kenya, Zambia, Malawi, nk upinzani uliona udhaifu wa namna hii kwenye vyama vikonge tawala and they stepped in to grab power through the ballot box. Sisi tusubiri t-shirt na pilau tuwachague jamaa watakaorudi kujaza matumbo ambayo tayari yanakaribia kupasuka kwa hela waliyowarubuni. Usiuze kura yako wakati ni huu wa kujikomboa!
Quote
 
 
0 #42 2010-05-19 17:40
UVCCM ndio chimbuko la viongozi wa nchi hii nawaomba muwe makini na maamuzi yenu mnayofanya wakati mnapoendesha mambo yenu la sivyo mtatengeneza viongozi wabovu siku za usoni
Quote
 
 
0 #41 2010-05-19 17:33
Tumuombe mungu ainusuru nchi yetu!! Lakini hili la HAMAD YUSUPH kuna siri ndani yake si umri.
Quote
 
 
0 #40 2010-05-19 17:20
Mwisho wa CCM unakaribia, Lowasa na mafisadi wenzako saidia kuisambaratisha ifie mbali.
Quote
 
 
+1 #39 2010-05-19 17:18
Lowasa endelea kusambaratisha CCM ife kifo kitakatifu, tumeshaichoka sanaaaa.
Quote
 
 
0 #38 2010-05-19 16:00
CHADEMA WAMELIONA HILO WANALIFANYIA KAZI
VIJANA WA UKWELI TUAMKE TUIUNGE MKONO CHADEMA ITUKOMBOE NA HAWA WASEMA UONGO
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner