MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Slaa amshukia Rais Kikwete  Send to a friend
Thursday, 05 January 2012 21:20

ASEMA AMESHINDWA KUTATUA MATATIZO YA UCHUMI, AMTUHUMU KUTUMIA SIASA KWA MAMBO MAZITO ASHANGAA MAFISADI EPA WAKITAMBA
Leon Bahati
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa ametoa tathmini ya mwaka mmoja tangu Rais Jakaya Kikwete alipoingia kuongoza nchi katika ngwe ya pili, na kusema mkuu huyo wa nchi ameshindwa kutatua mambo mengi mazito yanayohusu uchumi na maisha ya Watanzania.Akitoa tathimini hiyo jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa aliorodhesha baadhi ya  matukio aliyoita ya kuhujumu uchumi wa nchi pamoja na athari mbalimbali za maisha ya Watanzania.

Dk Slaa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi aliangushwa na Rais Kikwete, alisema wakati matatizo hayo yakionekana kuathiri uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania, bado utatuzi wake umekuwa ni wa kisiasa, usiozingatia utaalamu.

Alifafanua kwamba udhaifu katika kukabiliana na matatizo hayo ya kiuchumi, umezidi kuongeza ugumu wa maisha kwa watu wa kipato cha chini huku neema ikielekezwa kwa wachache, wakiwamo watuhumiwa wa ufisadi ambao pamoja na kuwapo na ushahidi wa kuwashitaki, wamekuwa wakikingiwa kifua.

"Tumesikitishwa na hali tete na mwelekeo mbovu wa uchumi wa nchi yetu na kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi kunakoendelea kusababishwa pamoja na mambo mengine, mfumuko wa bei na thamani ya shilingi kutokuwa imara. Hali hii siyo tu ni tishio kwa maisha ya wananchi bali pia kwa usalama wa nchi kwa ujumla," alisema Dk Slaa.

Alisema hata hotuba ya mwaka mpya aliyotoa Rais Kikwete, alishindwa kueleza hatua thabiti na za haraka za Serikali katika kukabiliana na hali mbaya na uchumi.

"Badala yake aliendelea na utaratibu uleule wa hotuba zake za kuorodhesha visingizio vya nje vya uchumi wa dunia bila kuweka mkazo katika kuelekeza hatua za kuinua uchumi wa ndani pamoja na kulinda wananchi dhidi ya misukosuko ya nje," alilalamika Dk Slaa.

Huku akisisitiza kuwa ana nakala ya hotuba ya Rais Kikwete na ameisoma kwa makini, alisema  siyo kweli kwamba hali ya mbaya ya uchumi imesababishwa na tatizo la uchumi wa dunia kama alivyosema mkuu huyo wa nchi, bali ni uzembe unaotokana na watendaji wake.

Kutokana na Chadema kutoridhika na hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyopo nchini kwa sasa, Dk Slaa alisema Kamati Kuu ya chama hicho imeitisha kikao kitakachofanyika Januari 22, mwaka huu kuangalia njia za kuchukua kuwalinda Watanzania.

Alisema matatizo yote ya kiuchumi yatajadiliwa na kufanya uamuzi wa hatua muafaka za kuchukua, ili kusimamia uwajibikaji wa Serikali kwa maslahi ya umma.

Mtendaji mkuu huyo wa Chadema, alisema kwa sasa hali inaonekana kuwa Serikali inatatua matatizo ya nchi kisiasa zaidi kuliko kutumia wataalamu wake katika kuweka mikakati imara iliyobuniwa kisayansi.

Alitoa mfano kwamba, uhaba wa sukari unaolikumba taifa kwa sasa hauwezi kutatuliwa kwa kununua sukari nje na kuitoa kwa mgawo kwani kunaongeza tatizo badala ya kuliondoa.

Dk Slaa alidai kwamba ana vielelezo vingi vya siri vinavyohusu Serikali, na kwamba utawala wa Rais Kikwete unaogopa kusema ukweli kuhusu sababu zinazosababisha uchumi wa nchi kudorora huku gharama za maisha zikipanda kila kukicha.

Alifafanua kwamba Serikali inashindwa kueleza ukweli wananchi kuhusu, "Hali mbaya ya kifedha ambayo inalikabili Taifa hivi sasa kwa kupungua kwa mapato ya ndani na nje, ukilinganisha na bajeti iliyopitishwa."

Dk Slaa alisema Serikali imeshindwa kueleza mpango wake wa kuongeza uzalishaji na kupunguza matumizi yake.

Alionya kwamba, baadhi ya viongozi wa Serikali wameendelea kujineemesha kwa kujiongezea malipo huku wakizidi kuongeza bei ya huduma za msingi, zinazotolewa na taasisi zake.

Ingawa Dk Slaa hakuweka wazi suala hilo, lakini nyongeza ya posho za wabunge kwa sasa zimekuwa zikitikisa taifa. Posho za vikao za wabunge ziliongezeka kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku kwa kigezo cha kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma.

Dk Slaa alirejea kuonya, "Hali hii ikiachwa iendelee itakuza pengo la wenye nacho na wasio nacho katika taifa na wakati huo huo itaongeza zaidi gharama za maisha kwa wananchi hususani wa kipato cha chini, tofauti na ahadi ya Rais Kikwete na CCM ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania."

Ufisadi
Dk Slaa alisema Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa katika kushughulikia matatizo ya ufisadi, ambayo yamelikabili taifa na kusababisha mabilioni ya fedha za umma kuchukuliwa na wachache.

Alisema licha ya watuhumiwa kufahamika wazi na kwamba chama hicho kiliwatangaza hadharani, hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.

Alisema Sh70.7 bilioni zilizorejeshwa na waliozichota kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), hadi sasa hazijulikani zilikoenda jambo ambalo tayari taasisi za kimataifa zimeingilia kati na kuitaka Serikali itoe maelezo.

Dk Slaa alisema Watanzania wengi, wakiwepo waandishi wa habari wanaelekea kusahau sakata la marejesho ya fedha za EPA, lakini mataifa yanayochangia bajeti ya Serikali wamekuwa wakihoji suala hilo.

Alisema ana barua iliyoandikwa kwa Serikali ikihoji ziliko fedha hizo ambazo ni sawa na asilimia 54 ya fedha zote zilizochotwa kwenye akaunti hiyo ya EPA, mwaka 2004/05.

Katika kuthibitisha kwamba Serikali imekuwa ikiwakingia kifua watuhumiwa wa ufisadi ili wasichukuliwe hatua, alitoa mfano chama chake kiliwasilisha kwa Mkurugezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ushahidi dhidi ya mtuhumiwa wa ufisadi wa ununuzi wa rada.

Kwenye ushahidi huo ambao uliambatanishwa na vielelezo vya uchunguzi wa Taasisi ya Uingereza ya Kuchunguza Makosa ya Jinai (SFO), Dk Slaa alisema zilionyesha jinsi mtuhumiwa alivyojipatia Sh1 bilioni na kuziweka kwenye akaunti nchi za nje.

Alisema hali hiyo inashangaza kwani  watu wa kawaida wanaotenda makosa hata kwa kuhisiwa tu wanakamatwa na kupelekwa mahabusu kabla ya kufikishwa mahakamani, lakini vigogo wa Serikali wanaonekana kulindwa.

 Dk Slaa alisema wananchi wanataabika kutokana na migogoro mbalimbali ikiwepo ya ardhi, elimu, afya na maji.

Alisema migogoro hiyo inashindwa kutatuliwa kwa sababu badala ya kushughulikia chanzo, Serikali imekuwa ikitafuta ufumbuzi wa matokeo yake.

Dk Slaa alitoa mfano wa migogoro hiyo ya ardhi kuwa ni ile kati ya wananchi na wawekezaji, wakulima na wafugaji na ile ambayo Serikali yenyewe imejikuta ikipambana na raia wake.

Migogoro mingine, alisema ni ya wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini akasema tayari amewasiliana na Umoja wa Vijana wa chama hicho (Bavicha) kufuatilia kwa ukaribu suala hilo ili kuweka wazi hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Saturday, 07 January 2012 05:30
 

Comments 

 
-2 #44 2012-01-07 05:37
Slaa anazungumza kwa uchungu. hizo zote ni hasira za kuukosa urais mwaka 2010. slaa ana mtazamo hasi dhidi ya JK. haoni mazuri ya JK. yeye anaona kila kilichfanywa ni kibaya. he has no balanced view. Tulitegemea atueleze mabaya na mazuri

Haelewi uchumi wa dunia unaendaje. wala hana habari kuwa mtikisiko wa uchumi kidunia una mguso wake katika nchi changa

Baba wa taifa alisha wahi kusema kuwa kama merikebu zinzyumba itakuwa vimashua? Ileweke kuwa wote tupo katika bahari moja

Rais ajae awe ana elimu ya uchumi.
Quote
 
 
+1 #43 2012-01-07 05:31
ccm kama ilivyokuwa kwa vyama vinginevyo vya uhuru Afrika lazima kilewe madaraka na baadaye kushindwa uhcaguzini na huu ndiyo mwelekeo
Quote
 
 
0 #42 2012-01-07 05:07
Vyanzo vikuu vya kushindwa kwa uchumi wetu:
1.Siasa na utawala mbovu.
2.Uwezo mdogo wa watanzania wengi wa kufikiri kutatua matatizo yao.
3.Uvivu na porojo za watanzania wengi.
4.Kukosa wabunge watetezi wa taifa (tulio nao 'the difference is the same')
5.Mfumo wa elimu kariri ambayo haimjengi mtoto kuwa mgunduzi.
6.Kubwa la yote ni 'attitude of mind' mtazamo wa mambo kwa ujumla.
Hivyo, siyo rais pekee ni lazima kila mtu afanye mabadiliko muhimu.
(Kisiasa,fikra, kiuchumi,kumuog opa Mungu na kielimu)
Quote
 
 
0 #41 2012-01-07 02:01
Huyu ndulamapolu ndula ni Mtanzania kweli au? Kila alichoorodhesha kinasema tu "CDM mnaonekana...". Wanaonekana hivyo au ndivyo walivyo? Chadema wamesaidia chama kilichoshika dola kuona wapi wafanye kazi kwa kuwanyooshea vidole mafisadi. Wamezawadiwa kwa kutupiwa tuhuma za "kuonekana...". Ndula anaamini huo ndio ukweli. Pole.
Quote
 
 
0 #40 2012-01-07 01:33
Atafanya nini na wapi ili ninyi mnaohoji mpate vya kuongea zaidi? Acheni mawazo finyu ndg. zangu, cha msingi ni kumsihi ajipange vzr zaidi kwa 2015. Nina imani CCM kwisha hbr yake mwaka huo. Labda Dr. Maghufuli (Raisi), Dr. Asha-Rose (Waziri Mkuu).
Quote
 
 
0 #39 2012-01-07 00:44
kuna watanzania na mitanzania,wata nzania ni wake wanaokubali ukweli,bilioni 70 zimerudishwa,lk n zpo wapi,kama hazionekani za nn sasa walizirudisha.wazungu waliokuwa nje wanaona huruma,lkn mitanzania inaona sawa na porojo.dr slaa pigana KANU iliondoka kwa kubweteka na CCM itaondoka kwa kutokubali mbadiliko.magufuli anaact kwa nauli ya sh 200,lkn mabilion ya epa,ndege feki ya rais,richmond wapo kimya.bado mitanzania inaona dr slaa ana porojo.hvyo vitu kama si chadema na dr slaa mngejua yanayoofanyika?kama dr slaa muongo unadhani srikali ingemuacha huru?jamani,mabadili ko si vita,na hata mabadiliko yakitokea hao ccm wakijipanga nao wanaweza tena kurudi madarakani.mm naona mitanzania inayopinga ina mahusiano na mafisadi.bibi yako anakufa kijijini kwa shida ya gari ya hospitali hakuna,wakati watu wanasign mikataba feki inayoweza kununua hata hizo gari kila kijiji na si wilaya.Watanzania tukubali point achaneni na mitanzania.
serikali kweli inafanya maendeleo,lkn kwa spidi yake na mali asili zetu ni sawa na chini ya asilimia 15.mtashangaa ccm 2015 wamchagua fisadi agombee,sumaye, lowasa na wengineo wote mafisadi,ww sumaye ulifanya nn,kwa nn leo tunamkumbuka sokoine tusikukumbuke ww,ben alichukua kiwira,ulisema nn,nawe ukachukua lunch,leo unajifanya kumlaumu kikwete.ni bora kikwete hana kashfa tatizo lake urafiki na kuwa kimya.muda umefika na NINAAMINI SLAA AKICHUKUA NCHI MAFISADI TUTAWASHITAKI UPYA.
Quote
 
 
0 #38 2012-01-07 00:22
NAWAPONGEZA VIONGOZI WA CHADEMA KWA KUWA NA JICHO LA KUONA NA KUJALI. WENGINE WANAMACHO LAKINI HAWAONI NA ETI NDO VIONGOZI MUNGU SAIDIA HILI JAHAZI MV TANZANIA LISIZAME
Quote
 
 
+1 #37 2012-01-06 15:34
NDULAMAPOLU UNAONESHA JINSI GANI, HUONI HALI HALISI YA MAISHA YA WATANZANIA UNAAKILI KAMA HAO CCM,HIVI KAMA SIO CHADEMA NA HANGETUAMBIA KUHUSU EPA, RICHIMOND,MEREM ETA NA NYINGINE NYINGI SANA SASA WEWE UNATAKA KUTUAMBIA NINI WEWE.
Quote
 
 
+1 #36 2012-01-06 15:22
ndulamapolu ndula we ndo hujui kitu chuoni mikopo haipatikani we ulishawahi kuwa chuoni ukakosa chakula utasomaje maisha magumu huyaoni wewe unaishi wapi wewe na ombea watu wengine wasijue hiyo serikali yako inachokifanya mambo yetu yatakuwa magumu kabisa.
Quote
 
 
+5 #35 2012-01-06 15:14
Watu wengine bwana utadhani hawajaingia jando.Kwa hiyo tukimbilie amani huku mali zetu zinaporwa na watu toka nje.Kama wewe mwoga lala chini ya kitanda.Wacha wanaume tuihoji Serekali mali zetu zinatunufaishaj e?.
Quote
 
 
+1 #34 2012-01-06 14:58
DR NAONA UMESAHAU KUWA 2015 SI MBALI, JIPANGE VIZURI, ACHANA NA MAANDAMANO YASIYO NA TIJA. CHADEMA ISIPOTUMIA UDHAIFU WA SERIKALI YA CCM ITAKUWA NA KIBARUA KIGUMU UCHAGUZI WA 2015.
Quote
 
 
+4 #33 2012-01-06 14:35
mmm napata wakati mgumu napotazama kinachoendelea kati ya siasa ya bongo, ila watanzania lazima watambue kuwa bila ya wapinzani wa sasa mambo mengi tunayoyajua tungefungiwa ndani ya kabati. anayesema DR. SLAA amefanya nini lipindi cha mwaka mmoja tangu ashindwe uchaguzi nadhani ni ufinyu wa mawazo na ndio wale wanaotaka mtu kuwaletea maendeleo chumbani kwao hajui kuwa hata kujua tu anavyoibiwa tayari ni mchango huo watanzania,

asante,
Quote
 
 
-20 #32 2012-01-06 14:10
Wimbo mpya huo mmeusikia? wapiga disco tu hawa hawana lolote zaidi ya kutaka kuwachonganisha watanzania na serikali yao. kwani hatuoni jitihada za serikali? Ninyi mnaoendesha maandamano kila kukicha ndio mnaoleta matatizo , watu hawafanyi kazi za maendeleo kwa ajili ya vurugu zenu. kwa maana hiyo unataka kuwaambia nini Watanzania? zaidi ya kutaka Sifa isiyokuwa na tija? CDM kwa sasa graph yenu inashuka badala ya kupanda; 1. Mnaonekana ni wachonganishi. 2. Mnaonekana siyo watu wa maendeleo. 3. Mnaonekana watu wa kulipa visasi. 4.Mnaonekana ni vishawishi vya fujo na vurugu. 5. Mnaonekana Msiowatakia Amani Watanzania. 6. Mnaonekana vyanzo vya Vurugu na Migomo Vyuo Vikuu. hayo ni madokezo katika madhambi yenu mengi. Sijui kama mnalo lolote Jipya: Mwisho Mlipoona mmejichanganya katika Mchakato wa Katiba Mpya Mmmepoa kidogo mkitafuta jinsi ya kuwahadaa wananchi ili wawaone kweli mnayo nia ya dhati kutaka kuwaletea mabadiliko, kumbe mlitaka kujijenga kisiasa, Ukweli Slaa kwa sasa ungekaa pembeni huna jipya na huitakii Mema Tanzania. Hivyo Watanzania amkeni Mtambue kuwa Hawa Jamaa hawana Jema kwetu: TUNATAKA AMANI YETU NA UPENDO WETU DAIMA HATA KAMA HATUNA KITU. IDUMU TANZANIA YETU. 50YRS
Quote
 
 
+5 #31 2012-01-06 14:09
Hapa naomba tuache siasa bali tuangalie hali halisi. Je ni kweli serikali haioni kuwa wananchi hawafaidiki na rasilimali za Taifa?? Hapa naomba kutoa changamoto kwenye MADINI NA UTALII. Nchi za Ulaya na Marekani ambao hawana mbuga zilizoneemeka kama sisi, wnaingiza hela nyingi kwa utalii. Usishangae kuwa sehemu fulani inatokana na ZOO za wanyama waliotoka Loliondo , nk sitaki kusema sana. Tuboreshe miundombinu na kukusanya kodi sitahiki kutoka kwa wawekezaji. Jamani uwekezaji sio majengo, tunataka hizo kodi ikusanywe sio kuwaachia wanasafirisha pesa yote nje ya nchi kwa miaka 5 kisha wanauziana biashara, kuanza miaka 5 mingine ya kuchuma bila kodi.

Sijui niseme nini kuhusu madini, naona ni kero tu labda wizara ya madini inaweza kusema jinsi wanavyosaini hiyo mikataba ni kwa faida ya nani??
Quote
 
 
+4 #30 2012-01-06 14:05
Nchi inajazwa watu wa kuhamisha fedha itaachaje kuwa masikini.Kama madini yetu na hifadhi zetu tukizitumia kwa manufaa yetu lazima nchi ibadilike.Tanzanite imevunwa na wawekezaji toka nchi tumefaidika na kitu gani?. Watu kama Sunda, Erasto, Mathias wamevuna madini na kujenga magorofa kuongeza ajira. Tanzanite One wamejenga kitu gani?. Viongozi acheni kutuma lizia rasilimali za watoto. CHADEMA jijengeni tuwape uongozi wa nchi 2015 muokoe mali za watoto wetu zinazovunwa bure.Nchi inashindwa kujiendesha yenyewe inategemea misaada ya wahisani wakati kumejaa madini na wanyama kila mahali.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner