MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Msiba wa Regia waibua mazito  Send to a friend
Tuesday, 17 January 2012 21:27

CHADEMA NUSURA WAZICHAPE MSIBANI IFAKARA, MBOWE AIPIGA SERIKALI KIJEMBE, MAKANI AANGUKA AKIAGA MWILI, KAFULILA AWA KIVUTIO
Na Waandishi Wetu
MAKUNDI mawili yanayopinga ya wanachama wa Chadema jana nusura yazichape kavukavu yalipokuwa katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema huko Ifakara, kutokana na chuki na makovu ya uchaguzi wa wa ndani wa chama hicho wa mwaka 2010.

Wakati hayo yakitokea huko Ifakara, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitumia fursa aliyopewa wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo kuipiga vijembe Serikali huku Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Bob Makani akianguka ghafla.

Marehemu Regia ambaye alifariki dunia Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari iliyotokea Ruvu, Pwani, unatarajiwa kuzikwa leo Ifakara.

Katika tukio la Ifakara, mgogoro baina ya kambi mbili zilizotokana na makovu ya uchaguzi huo wa ndani kati ya wafuasi wa marehemu na ya Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga ulisababisha kutimuliwa msibani hapo kwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Salum Ngozi.

Ilielezwa kwamba baada ya Ngozi kufika msibani hapo juzi majira ya saa moja usiku na kusalimiana na viongozi wa Serikali, alifuatwa na baadhi ya makada wa chama hicho wakimtaka aondoke eneo hilo jambo ambalo aliligomea. Wafuasi hao wa Chadema waliamua kutumia nguvu kumwondoa hali iliyowalazimu polisi waliokuwa eneo hilo kuingilia kati. Askari walimtoa mwenyekiti huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wilaya.

Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Ngozi kutimuliwa katika msiba huo. Mara ya kwanza ilikuwa juzi na kumlazimu Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Francis Miti kuingilia kati.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Ngozi alikiri kutokea vurugu hizo msibani na kudai kwamba, alifanyiwa fujo na kikundi cha watu aliowaita wahuni na kwamba amefungua kesi ya kufanyiwa vurugu katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero na kwamba baada ya kumalizika kwa mazishi atasimamia suala hilo ili haki itendeke.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe mbali na kukiri kuufahamu mgogoro huo, alisema asingependa kuzungumzia suala hilo sasa wakati watu bado wanaendelea na msiba.

Mbowe aipiga vijembe Serikali

Jijini Dar es Salaam, tukio la kuaga mwili wa marehemu Regia liligeuka jukwaa la siasa baada ya Mbowe na Makinda kupiga siasa.

Mbowe alitumia msiba huo kutoa dukuduku lake juu ya shughuli za chama chake kisiasa na kiutendaji wakati akitoa salaam za rambirambi kwa marehemu.Mbowe aliirushia kombora Serikali na vyama vingine vya upinzani kuhusu mwenendo wa Chadema kuendesha siasa katika vyuo vya elimu ya juu akisema ni mpango maalumu kuwanoa wanasiasa mahiri.

Aliishauri Serikali na vyama vingine vya siasa kuiga utaratibu huo wa Chadema akisema unasaidia kukuza vipaji na kuwaandaa viongozi makini kwa kuwapa nafasi vijana kushiriki katika uongozi.

“Kuna jambo moja ambalo ningependa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine walitafakari na wasilibeze hili. Viongozi huandaliwa na viongozi makini hawazuki tu,” alisema  na kuongeza;

“Naeleza hivyo maana mara nyingi tumekuwa hatueleweki na tumekuwa tukibezwa. Sisi tunatambua viongozi wa baadaye  kisha tunakuza vipaji na kutoa fursa za nafasi za uongozi kwa vijana.”

“Vijana lazima waandaliwe kimaadili na ndiyo maana tuliingia vyuo vikuu lakini tukatafsiriwa kuwa ni wakorofi na wachochezi wa vurugu. Lakini leo tumepata viongozi wazuri vijana kwa njia hiyo kutoka vyuoni kama vile Mheshimiwa Zitto (Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini), Mnyika (John Mbunge wa Ubungo, Mdee (Halima-Mbunge wa Kawe), Silinde (David Mbunge wa Mbozi) na Mtema (Regia Marehemu).

“Hawa tuliwaandaa, hawakuzuka. Rai yangu kwa Serikali na kwa wazazi ni kwamba vijana hawa wakifanya siasa tusiwakwaze na kuwafukuza, bali tuwalee.”

Spika Makinda katika kile kilichoonekana kama ni kumjibu Mbowe, alitumia fursa hiyo kufafanua uendeshaji wa shughuli za Bunge akisisitiza kwamba linaendeshwa kwa kanuni na wala si kufurahisha watu.
Alimsifia marehemu Mtema kwamba alikuwa akizijua vyema kanuni za Bunge: “Bunge huendeshwa kwa kanuni na si kwa matakwa tu ya kufurahisha watu. Yeye marehemu alizijua kanuni ndiyo maana hata wakati alipokuwa akikosea alikuwa tayari kuomba radhi.”

Mzee Makani aanguka
Hata hivyo hafla hiyo iliingia dosari baada ya Makani kuanguka muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu. Baada ya tukio hilo, alibebwa na kupelekwa pembeni ambako alipepewa kwa takriban dakika tano kisha kurejea katika hali yake ya kawaida na kurudi kwenye kiti chake.

Baadaye Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ambaye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakimpatia Mzee Makani huduma ya kwanza aliwaambia waandishi wa habari kuwa alianguka baada ya kuishiwa nguvu ghafla.

“Sasa anaendelea vizuri na amerudi kushiriki kumuaga mpendwa wetu katika safari yake hii ya mwisho,” alisema Mbatia.

Kafulila ashangiliwa

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana alishangiliwa kwa makofi baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa wabunge walioteuliwa na Ofisi ya Bunge kuwamo katika msafara kusindikiza msiba huo akiwakilisha chama chake.

Baada ya kiongozi wa shughuli hiyo, Ofisa Mwandamizi wa Ofisi ya Bunge, Saidi Yakub kumtaja Kafulila baadhi ya waombolezaji walishangilia kwa makofi, vicheko vya chini kwa chini na minong’ono ya hapa na pale.

Hatua hiyo ya waombolezaji inatokana na hali ya kisiasa ilivyo kati ya Kafulila na chama chake hicho ambacho mwishoni mwa mwaka jana kilitangaza kumvua uanachama hatua ambayo ameipinga mahakamani. Kama ikitekelezwa, itamvua ubunge.

Imeandikwa na Venance George, Morogoro, Aziza Masoud na James Magai, Dar


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 19 January 2012 00:23
 

Comments 

 
0 #37 2012-01-18 22:04
nadhani tusiangalie saana yaliyotokea huko, yashapit, 2one ni kwa vp 2tam replace huu jembe aliye2potea!!!! !!!!

malumbano wakati nchi inadidimia c iahu vijana wenzangu, nchi ye2 iko pabaya!!!!
Quote
 
 
0 #36 2012-01-18 19:57
OFISI YA BUNGE KUPITIA OFISA MWANDAMIZI NDG. YAKUB NI WACHOCHEZI NA WALETA FUJO KATIKA MGOGORO WA NCCR.KWANI ILIKUWA NI LAZIMA AWAKILISHE MBUNGE ALIYE KATIKA MGOGORO KATIKA MAZISHI YA MBUNGE MTEMA. ACHENI UNAFIKI MNATUBOA.
Quote
 
 
0 #35 2012-01-18 19:53
poleni wafiwa ,kazi ya mungu.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU REGIA mahali pema peponi AMINA.
viongozi tueshimu msiba kwanza malumbano baadae mjengoni na sio msibani.
Quote
 
 
0 #34 2012-01-18 19:09
Quoting sadia:
Hivi marehemu Regia si alikuwa mremavu?lakini mbona tunasikia kuwa gari lililopata ajali alikuwa anaendesha yeye mwenyewe?hii ina kuwa vipi mremavu wa miguu anaachiwa anendeshe chombo cha moto au sheria kwa wanyonge tu?



kuwa mlemavu haina maana kuwa huwezi kufanya kitu kingine. Tunamshukuru Regia kwa kuonyesha hivyo. Labda tu sasa tuangalie ni aina gani ya gari mlemavu yupi anaweza kuendesha,gari linaweza likatengenezwa ( kubadilishwa) ili liweze kuendeana na ulemavu wa mtu. Tafadhalini tusitumie msiba huu kuwapunguzia walemavu nafasi za kufanya vitu ambavyo watu wasio na ulemavu unaoonekana wanavifanya. Ukifikiri sana sisi wote ni walemavu.
Quote
 
 
0 #33 2012-01-18 17:52
serikali ya tanzania fungukeni masikio tazameni yale yaanayotokea nigeria,yakitok ea hapa tanzania sijui mtamlaumu nani?mtayalaaumu mataifa ya magharibi au mtajilaumu wenyewe?nipeni majibu
Quote
 
 
0 #32 2012-01-18 16:35
waandishi nyie sometimes ni wagombanishi mbona sioni uhusiano wa ugomvi wowote kati ya mbowe na anna makinda coz wote wameongea kitu sahihi na wala makinda hakumjibu mbowe kama nyinyi mwananchi mulivyoandika.
Quote
 
 
0 #31 2012-01-18 16:17
Marehemu Regia alikuwa shujaa wa kuiga ndani CHADEMA. Ameacha pengo kubwa ndani ya chama cha CHADEMA. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. Amina
Quote
 
 
0 #30 2012-01-18 15:54
imefikia wakati utengenezwe utaratibu wa kuhakiki uwezo wa viongozi kutumia vyombo vya moto for long trip driving, kwani kwa hali ya dada yetu hakutakiwa kabisa ku drive hata town trips, sasa kutokuwa fit kunaweza kuchangia mambo mengi, angezingatia dhamani yake mbele ya jamii angejijali sana na kutafuta professional driver, hili lili changia pia kifo cha chacha wangwe, amemchukua mshkaji hata leseni hana am-drive kwenda Dar, huu ni utani kwenye maisha yetu, please washauriwe vizuri juu ya hili please
Quote
 
 
0 #29 2012-01-18 15:10
Si nikamuona Kafulila akitoa Sera kule Kigoma nimejiuliza Kama NCCR hawamtambui yeye alikuwa anaongea kwa Tiketi ya Chama kipi? Lkn safi sana kwa kuhudhuria Msibani kwa Mwanaharakati Mwenzio, Dini safi ni ile inayo jali watu k.m hawa. REST IN PEACE REGIA.
Quote
 
 
0 #28 2012-01-18 15:06
Kweli umona jamaa wa Bungeni walivyo na afya Story picha imeshinda hata habari maneno, Mwananchi acheni kuwachonganisha wenzenu
Quote
 
 
0 #27 2012-01-18 14:46
Hivi marehemu Regia si alikuwa mremavu?lakini mbona tunasikia kuwa gari lililopata ajali alikuwa anaendesha yeye mwenyewe?hii ina kuwa vipi mremavu wa miguu anaachiwa anendeshe chombo cha moto au sheria kwa wanyonge tu?
Hivi jamani nani kasema mlemavu hawezi kufanya vitu. Kuna wanavyoweza na kunawasivyoweza . Tushiriki kuwanyanyua walemavu kama walivyofanya CHADEMA. Marehemu hakupenda kabisa kuchukuliwa kama mlemavu hivyo hawezi kitu. Upande huo tuwaachie waliompa leseni.
Quote
 
 
0 #26 2012-01-18 14:45
hawa viongozi kwakweli wanashindwa kuelewa tofauti ya jukwaa la siasa na sehemu yenye msiba?hebu tuheshimu wanafamilia kwakipindi hichi kigumu jamani.TUWEKE PEMBENI TOFAUTI ZETU!!!
Quote
 
 
0 #25 2012-01-18 14:34
jamani waandishi wa habari acheni vijembe visivyokuwa na msingi na huu ni uchonganishi wa wazi kabisa maana sioni mahusiano kati mheshimiwa Mbowe na Speaker wa bunge , kuweni mfano bora kila tunawalalamikia kuhusu uchonganishi...kama gazeti litanunuliwa tuuu
Quote
 
 
0 #24 2012-01-18 13:59
Quoting elineema:
chadema ina watu makini tena sana.Hawawezi kulumbana ovyo ovyo, huyo jamaa katumwa na ccm.Nawapeni pole wadau wote na wapenz wa chadema kwa msiba uliotufika!?

Hajatumwa na CCM labda elineema sio mfuatiliaji na huijui vizuri hali ya CHADEMA hapa ifakara. Kilichopo ni kwamba kulikuwa na wabunge wawili wa viti maalum hapa ifakara Suzan Kiwanga na Hayati Regia Mtemanyenja na walikuwa hawaivi. Mwenyekiti yuko kundi la Suzan na Katibu yuko kundi la hayati Regia kwa hiyo kutimuliwa kwa Ngozi msibani inatokana na bifu la wabunge hao.
Quote
 
 
0 #23 2012-01-18 13:53
polen sana wanaifakara wenzangu kwa kupotelewa mpiganaji mwezetu, mungu ailaze roho marehem amina.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner