MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Dk Slaa ampiga chenga JK msibani  Send to a friend
Wednesday, 18 January 2012 21:08

AKWEPA KUKAA JUKWAA KUU, WENGI WAMZIKA REGIA
Juma Mtanda na Shakila Nyerere, Ifakara
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, jana alimkwepa tena Rais Jakaya Kikwete safari hii ikiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema yaliyofanyika katika Kijiji cha Lipangalala.Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia  26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.

Katika hafla ya kutangazwa matokeo ya urais iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, Dk Slaa hakuhudhuria tofauti na ilivyokuwa kwa waliokuwa wagombea wenzake wote.

Jana, Dk Slaa tofauti na viongozi wenzake wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hakutaka kujiweka katika mazingira ambayo yangemkutanisha na Rais Kikwete katika mazishi hayo.
Nyumba kulikofanyika shughuli za awali za mazishi, waandalizi waliandaa majukwaa mawili, moja maalum kwa ajili ya wabunge huku jingine likiwa ni maalumu kwa ajili ya viongozi wakuu ambalo alikaa Mbowe, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe.

Mbali ya kukaa viongozi hao, kulikuwa na nafasi ambayo ilikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya Rais. Mbali ya nafasi hiyo, pia kulikuwa na kiti ambacho ilitegemewa kwamba Dk Slaa angekalia.
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Chadema alikikwepa na kwenda kujichanganya katika jukwaa la wabunge na kiti hicho kubaki bila ya kuwa na mtu.

Hata hivyo, Rais Kikwete hakuweza kufika nyumbani hadi mwili wa marehemu Regia ulipopelekwa katika Viwanya vya Viungani ambako uliagwa na mamia ya waombolezaji.

Uwanjani hapo nako kulikuwa na majukwaa mawili. Kama ilivyokuwa nyumbani, jukwaa moja lilikuwa la wabunge na jingine la viongozi wa ngazi za juu lakini bado, Dk Slaa alilikwepa jukwaa hilo ambalo Rais alitarajiwa kuwa angefikia. Rais hakuweza kufika Viungani pia.

Baadaye wakiwa eneo la mazishi, Rais Kikwete alifika na kushiriki tukio hilo na kisha kusalimiana na wabunge mbalimbali na viongozi waliokuwa wamefika akiwemo Mbowe, Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, Zitto na viongozi wengine lakini Dk Slaa hakuonekana.

Ilitegemewa kuwa tukio hilo la msiba lingewaleta wanasiasa hao lakini hadi Rais Kikwete alipoondoka hakuna mahali ambako walisalimiana.
Mbali ya tukio hilo, hata katika hafla mbalimbali ambazo viongozi wa Chadema wamekuwa wakialikwa ikiwemo Ikulu, Dk Slaa hakuwahi kuhudhuria.

Novemba mwaka jana viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe, walifanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu ya Dar es Salaam kujadili suala la Katiba Mpya, lakini Dk Slaa hakuhudhuria.


Chadema wahaha
Wakati viongozi wa Chadema wakihaha kumaliza mgogoro ndani ya chama hicho wilayani Kilombero, Pacha wa marehemu Regia, Remigia Mtema amesema ndugu yake Regia alikuwa akipeleka malalamiko kwa Dk Slaa mara kadhaa kuomba asuluhishe bila mafanikio.

Hata hivyo, Remigia alisema marehemu Regia alikuwa amepanga kuonana tena na Dk Slaa katika siku za hivi karibuni kumweleza kinachoendelea.

Akizungumzia suala hilo, Dk Slaa alisema alishaanza kushughulikia mgogoro huo lakini msiba huo ndiyo uliomkwamisha.

“Ni kweli nimekuwa nikielezwa tatizo hilo na tayari nilishaanza kulifanyika kazi ila sasa siwezi kusema suala hilo limefikia wapi kwani wote tuko kwenye mazishi,” alisema.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wabunge wa Chadema waliotangulia kufika katika msiba huo, Mchungaji Peter Msigwa, Ezekia Wenje na Lucy Owenya, walikutana na uongozi wa kata wa Chadema ili kumaliza mgogoro huo.

Katibu mwenezi wa Chadema kata ya Ifakara, Antony Kamonalelo alisema viongozi hao walikaa na wanachama hao na kuwataka wapunguze munkari ili kumruhusu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Salum Ngozi na Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga kuhudhuria mazishi.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba wanachama hao waliukubalia uongozi huo kumruhusu Susan peke yake kuhudhuria mazishi hayo.

Juzi, wanachama hao walimtimua msibani Ngozi kiasi cha kuwalazimu polisi waliokuwa eneo hilo kuingilia kati kwa kumchukua mwenyekiti huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wilaya.

Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Ngozi kutimuliwa katika msiba huo. Mara ya kwanza ilikuwa siku moja iliyotangulia ambayo ilimlazimu Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Francis Miti kuingilia kati.

Ngozi amekuwa akidai kwamba anafanyiwa fujo na kikundi cha watu aliowaita wahuni na kwamba amefungua kesi ya kufanyiwa vurugu katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero na kwamba baada ya kumalizika kwa mazishi atasimamia suala hilo ili haki itendeke.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Friday, 20 January 2012 07:10
 

Comments 

 
0 #40 2012-01-19 18:59
In my opinion I think Dr Slaa has shown an immense level of immaturity. The whole occassion was about to bring the nation together in respect of the deceased. Dr Slaa was supposed to show respect to the deceased but instead he behaves like spoilt child. I 'll say 2 words to him "GROW UP" and stop your self centred attitude.
Quote
 
 
0 #39 2012-01-19 17:49
mi sijawaelewa mnamaasha nini ,hakuna matatizo yanayowakabilia wananchi wa eneo hilo .hiyo ilikuwa ni fursa pekee mjifunnze

badala yake mnaleta habari nusu nusu
Quote
 
 
0 #38 2012-01-19 17:45
toeni habari za kueleweka mi siwaelewi mna maanisha nini hakuna matatizo mliyojifunza yanawakabili wakazi wa eneo hilo ambapo ingekuwa ni wakati wa kuujulisha umma .msilete habari nusu nusu hapa ,
Quote
 
 
0 #37 2012-01-19 17:38
asingeweza kukaa na mwizi wa kura!!
Quote
 
 
+1 #36 2012-01-19 17:32
Hivi huyu mwandishi alikua ana maana gani sijaelewa kwanini ana sema alimkwepa
Kwanza mwandishi anasema ilikuwa nyumbani ambako Dr. Slaa aliamua kujichanganya na wabunge badala ya kukaa sehemu ya watu maalum, hata hivyo JK hakuwepo. Mara ya pili ni baada ya kwenda uwanjani pia Dr. hakukaa sehemu maalum na JK hakuwepo vile vile. Ukiisoma kwa undani habari hii utagundua kuwa imeandikwa kiudaku sana! Naliheshimu sana gazeti la Mwananchi lakini naona sasa linazidi kupoteza Credibility kadri siku zinavyozidi kwenda. Kama hata rais hakuwa jukwaani ni nani alimkwepa mwenzie? Mwananchi jirekebisheni kabla hamjaharibika zaidi!
Quote
 
 
+1 #35 2012-01-19 16:57
Mairo acha kukurupuka na kuropoka hovyo,mm nilikuwepo kwenye mazishi jana hakukua na kiti kilichobaki wazi upande wa viongozi wakuu,mwananchi ni gazeti linalopendwa na watu ila mnaelekea gazeti hili kua la kidaku
Quote
 
 
+1 #34 2012-01-19 16:57
kweli mwananchi habari mlotoa ni kutaka kui[NENO BAYA]za chadema na ccm nampongeza mh slaa kwa kutambua na kujua kinachoendelea kati yake na rais ndio akamkwepa nawapa pole sana wana chadema na tanzania kwa ujumla
Quote
 
 
0 #33 2012-01-19 16:54
hii inadhihirisha kuwa Dr Slaa ni mpinzani wa kweli na hapendi utawala/kuwepo kwa kikwete madarakani. Ni mpizani wa kweli si wa kupandikizwa. Utamchekea vp adui wako wakati hataki kubadili mwenendo wa uwadui wake kwa familia yako.
Quote
 
 
+6 #32 2012-01-19 14:23
Sisi watanzania tuna akili ndogo sana. Hivi mtu asipoketi jukwaa kuu ndo kusema anamwogopa mwingine? Kwani Baba Ridhiwan anang'ata hata Dr. amwogope? Yamkini Dr. aliona asijikweze kihivyo, bali aamue kukaa mbali. Au kama angeketi pale yamkini waombolezaji wangeanza kushangilia na kusahau kuwa wako msibani. Tatizo la wabongo tunapenda vyombo vya habari vitusaidie kufikiri. Hii tabia siipendi na nailaani. Kila wanachosema waandishi wa habari ni lazima kiwe cha ukweli? Ndo maana tumekuwa tunasema "Tumezoea" Huu ni ugonjwa wa kitaifa.TUBADILIKE
Quote
 
 
-5 #31 2012-01-19 14:12
dr slaa sio mbaya sana,kama kweli unauchungu na nchi yako usikae nao karibu wale unaohisi hawana uchungu na nchi yao
Quote
 
 
-5 #30 2012-01-19 13:27
mimk nadhani Dr.Slaa anafanya sahihi kuonyesha hisia zake waziwazi badala ya kuwa mnafiki,Mpinzan i ni mpinzani hususani mtu ambaye walicchuana nae katika Kushika Dola.
Quote
 
 
+4 #29 2012-01-19 13:27
Shida, Slaa sio mnafiki na anaonyesha dhamiri yake ya kusimamia Ukweli na haki mpaka kufa,Tuache unafiki hakuna wakati wa kusimamia ukweli na wa kusimamia uongo hembu wengine tutoe coment zenye mantic kwasababu kunakila dalili ya kumsifia marehemu hata kama alikuwa mbayaa, Slaa kwenye majonzi na kwenye raha anasimamia ukweli na haki hakuona sababu ya kuuhadaa umma kwa kujifanya mshirika kwa anyewasababishi a mateso na hali ngumu ya kimaisha.Tufike wakati sasa ukweli utawale na tuchangie kama watu wenye uwezo wa kutambua watu na mambo.Baada ya Nyerere na sokoine Tanzania Hatuna kiongozi Mzuri kama Slaa the time will come to realise that but it will be too late to do!and history will judge us what a shame we wll be hata kamatutakuwa makaburini.Slaa ana Hofu ya kweli kwa Mungu ningemshangaa sana kama ningemuona eti kwasababu tuu ya msiba anakuwa ndumilakuwili.He lives what he say and he walk what he talks.
Quote
 
 
0 #28 2012-01-19 13:26
ni haki ya kila binadamu kuchagua marafiki zake japo hatuna uhuru wa kuwachagua maadui zetu. sasa Dr (wa kweli) ni mtu wa watu na aliamua kuchanganyika na watu. angalienda kumsalimia huyu dr.(?) kama nani kwake?. jadilianeni siasa au uchwara wowote mnaotaka lakini jaribuni kuheshimu uhuru wa mtu wa kuchagua.
Quote
 
 
-20 #27 2012-01-19 12:14
Slaa anaona aibu kwa makele yake na domo lake kubwa la kishenzi kutukana watu kila siku.

Pia simuelewi alikuwa Padri gani mwenye kinyongo na watu. Kwani Mheshimiwa Kikwete ndiye aliye sababisha yeye kupigiwa kura chache na watu wake?

Hapo ndipo sasa mjue Watanzania, mkipa Uraisi Slaa mtaona watu watakavyo nyongwa na kuchinjwa maana ana hasira ya kulipiza visasi au kuua hana jingine, He is a mass marderer and nothing else.
Muongopeni Slaa kama ukoma nawambieni. Ana roho mbaya mno.
Quote
 
 
+8 #26 2012-01-19 11:44
Sasa ninyi waandishi wa habari mnaangalia nani kamsalimia nani?
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner