MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Wabunge CCM wagoma kukutana na Kikwete  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 21:24

WAJIPANGA KUKWAMISHA MUSWADA  MABADILIKO YA KATIBA
Midraji Ibrahim, Dodoma
SASA ni dhahiri kuwa wigo wa mpasuko kati ya wabunge wa CCM na Serikali unazidi kupanuka, baada ya wabunge hao kugoma kukutana na Rais Jakaya Kikwete mjini Dodoma.Katika kikao chao kilichofanyika Ijumaa usiku ukumbi wa Pius Msekwa mjini hapa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwaomba wabunge hao kukutana na Rais Kikwete ili kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya Serikali badala ya kuendelea kuikwamisha bungeni.

Wabunge hao wanadaiwa kukataa rai hiyo huku wakimweleza waziwazi Pinda kwamba, itakuwa ni kumkosea heshima na adabu Rais, iwapo watakutana naye halafu wakwamishe marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayotarajiwa kufikishwa bungeni wiki ijayo.

“Itakuwa siyo heshima kukutana na Rais halafu tukwamishe muswada wa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kwa sababu tumejipanga kuhakikisha kwamba haupiti,” vilieleza vyanzo vyetu vya uhakika kutoka ndani ya kikao hicho.

Badala yake, wabunge hao walikubali kuteua miongoni mwao watu watano ambao wataonana na Rais Kikwete leo atakapowasili mjini hapa akitokea Mwanza kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 34 ya CCM.

Wazungumzaji wakuu kwenye kikao hicho wanadaiwa walikuwa pamoja na,  Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Shinyanga, Steven Masele.
 
Marekebisho hayo yalitarajiwa kuwasilishwa kesho, lakini walikataa hadi Ijumaa kwa kile walichodai kuwa, wengi wao watakuwa hawajarejea kutoka Mwanza  kwenye sherehe za maadhimisho ya CCM.

Inadaiwa na wabunge hao wa CCM kuwa, marekebisho hayo yanalenga kukimaliza chama hicho na kukiweka madarakani Chadema baada ya kuondolewa kwa wakuu wa wilaya, kushiriki mchakato wa katiba na kazi hiyo kukabidhiwa wakurugenzi wa halmashauri.

“Hii ni dhahiri kuwa marekebisho haya yanaiumiza CCM na kuisimika Chadema madarakani. Kuwaondoa Ma-DC kwenye mchakato wa katiba na kuweka wakurugenzi wa wilaya ambao wote ni Chadema, hatuwezi kukubali kamwe,” kilieleza chanzo chetu.
Pia, inadaiwa na wabunge hao kuwa marekebisho waliyopewa Dar es Salaam kwenye kamati, ni tofauti na yale yaliyowasilishwa bungeni, huku kukiwa na ongezeko la kurasa nne.

Hata hivyo, inadaiwa baada ya wabunge hao kugoma kukutana na Rais Kikwete, alisimama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wasira, akiwataka kupitisha marekebisho hayo kwa sababu ni agizo la Rais, hali iliyosababisha azomewe huku akitupiwa maneno ya kashfa.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao, walisema athari wanayoiona mbele kwa kutopitishwa kwa marekebisho hayo, Chadema watapeleka mashtaka kwa umma kwamba sheria ile ilipitishwa kulinda CCM, hivyo haina manufaa kwa umma.

“Lakini CCM hatujajipanga, kila siku anayesimama jukwaani anazungumzia kujivua gamba, kwa hali hii tusubiri mashambulizi mazito siyo tu kutoka kwa Chadema hata nchi za nje,” kilieleza chanzo chetu.

Pia, wabunge hao wa CCM wanadai kuwa miongoni mwa sababu za kukwamisha marekebisho hayo, ni kile walichodai Rais Kikwete kuwadharau kutokana na wao kupitisha muswada wa sheria hiyo, halafu yeye (Kikwete) anakutana na Chadema dakika chache na kukubaliana na hoja zao.

“Sisi tumekaa hapa (bungeni) kwa zaidi siku mbili na akili zetu timamu, tukapitisha muswada ule, anakutana (Kikwete) na Chadema dakika chache anatuletea marekebisho! Hiyo ni dharau na hatuwezi kukubali,” alilalamika mbunge mmoja.

Kura ya kukosa imani na Rais
Katika kikao cha wabunge hao kilichofanyika Alhamisi wiki hii, baadhi yao walihoji sababu zinazokwamisha masuala mbalimbali serikalini kutopatiwa ufumbuzi, huku Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, akipendekeza kwamba kama tatizo ni Rais Kikwete, watumie utaratibu wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani.

Shelukindo anadaiwa alitaka kujua sababu za masuala mbalimbali kukwama na kutopatiwa ufumbuzi wa haraka na kwamba, iwapo tatizo ni Rais Kikwete, wapo tayari kufuata utaratibu wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani.

Hata hivyo, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Olle Sendeka, alisimama na kumtaka mbunge huyo kufuta kauli yake, suala ambalo Shelukindo alikubali.

Pia, katika kikao hicho kiliwataka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda, Naibu wake, Dk Lucy Nkya na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni, kujiuzulu kutokana na kuwa chanzo cha mgomo wa madaktari.

Katika kile kinachoonyesha mpasuko huo kuchukua sura mpya, wabunge hao wamekuwa wakikwamisha miswada ya Serikali, suala ambalo siku zilizopita walikuwa wakiipitisha hata pale yanapokuwepo malalamiko kutokana kwa wananchi, kwa kile kilichokuwa kikielezwa kuwa ni ‘msimamo wa chama.’


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Monday, 06 February 2012 09:49
 

Comments 

 
0 #16 2012-02-08 09:47
Wabunge wa CCM watambue kuwa hili taifa ni la watanzania na sio lao peke yao na ili kuleta maendeleo ni muhimu kupokea mabadiliko yenye manufaa katika kuandaa sheria ya kuongoza nchi.kubalini kukosolewa hoja yenu ya kudhalilishwa haina msingi.
Quote
 
 
0 #15 2012-02-06 19:22
mm nahisi wabunge wa ccm wangeangalia utaifa kwanza, na si kutetea chama, ilituweze kujenga nchi yetu kwa pamoja, maana tunakoelekea ni kubaya sn.
Quote
 
 
0 #14 2012-02-06 11:39
Wabunge wa ccm,kwanini mnashindwa kufanya maamuzi ya busara kusolve tatizo la katiba?
Quote
 
 
0 #13 2012-02-06 11:18
wabunge wa ccm ni majibwa tu,mnawaza maslahi ya chama???,hamuoni hata haya!nawaonea huruma sana mnakavyoumbuliw a.mtakwisha na kusambaratika mapema tu.
Quote
 
 
0 #12 2012-02-06 10:48
katiba si ya ccm wala chama chochote kwanza muelewe sisi tusiokuwa na chama tuko wengi kwaiyo aituhusu iyo katiba? Tunakuomba sana mweshimiwa Rais usfanye makosa ktk swala la katiba yaliotokea nchi jirani ni kutokana na katiba zao kuwa za kibaguzi.
Quote
 
 
+12 #11 2012-02-05 13:53
Nafikiri siasa ya Wabunge wa CCM imefikia kikomo. Sasa mlifikiri ndiyo ninyi wenye majibu sahihi? Kwa nini msiwasilikize wenzenu kama mna busara za mwalimu. Napendekeza mkapingane kwa hoja na si kupiga propaganda nje ya bunge na mwisho mnaafika kuamua kwa kufuata mkumbo. Mambo mengi yamepitishwa kimizengwe na CCM sababu ya uwingi Bungeni na wala siyo yalistahili. Sasa katiba ya nini wakati sisi tunakufa mahospitalini kwa kukosa huduma? Hata aibu kama CCM leo inasherekea wakati wapiga kura wanakufa kama inzi oneni aibu jamani. Kweli nimeamini CCM ni chukua chako mapema. Chama hakina maslahi na wananchi wa Tanzania bali ni kujaza mifuko ya viongozi
Quote
 
 
+10 #10 2012-02-05 13:40
Enyi wabunge wa CCM? Msimfanye rais kuwa robot. Kwamba mnachokisema yeye afuate blindly. Hivi kukubali chema kitokacho chadema Rais kafanya dhambi? Wananchama wa chadema sio watanzania? Mnataka rais awe dictator kwa kukubali kila kitokacho kwenu? Kumbe mlizoea kufanya madudu mkitumia mgongo wa katiba mbovu. Heshimu ukweli wa mambo na ukweli ndo utaiweka nchi hii salama. Sio kubebwa na katiba mbovu hata pale mnapovurunda. Nyie lengo lenu ni kuhakikisha CCM inatawala jmilele. Lakini ebu angalia Kenya. KANU kwa kukubali ushindi wa wapinzani kuna kilichoharibika ? Si nao KANU sasa hivi ni wapinzani? Na si kwa maendeleo ya kenya? Hata CCM ikiwa kwnye upinzani itafanya vizuri kwa sababu itamulika udhaifu wa chadema na si ajabu ikatwaa tena madaraka huko mbele iwapo chadema watajisahau na kufanya madudu wanayoyapinga sasa hivi. Kikwete kumbe una kazi. Wenzako wanataka wakufanye robot, usifikiri bali kusema ndiyo kwa kila litokalo kwao hata kama ni kushibisha matumbo yao kama swala la posho!
Quote
 
 
+9 #9 2012-02-05 13:18
Waliposema CCM ni janga la taifa, hii ndio maana halisi. Wabunge wamesahau kwamba wanatengeneza katiba ya nchi sio katiba ya chama!, Huyu Sendeka nao amelishwa nini siku hizi, mbona kahama kambi ya wapambanaji?,amekua kambi ya mafisadi tena?, msitari mmoja na Chenge?, Aisee!

Naamini hawana uwezo wa kuzuia hayo mabadiliko, ni hatari kwa chama kuliko kuyapitisha!

Kwanza wakuu wa wilaya sio tu kwamba wasishiliki, bali hawana kazi ya maana hivyo cheo hicho kifutwe sambamba na wabunge wa kuteuliwa ambao kimsingi hawana wanaemuwakiliha !
Quote
 
 
+9 #8 2012-02-05 13:08
sasa watanzania tujiulize tatizo la kupata katiba nzuri ya wananchi ni rais au ni wabunge wa ccm?..wanaccm wenzangu nchi ni muhimu zaidi kuliko chama rais kaliona hilo wabunge badilikeni kabla hamjabadilishwa !
Quote
 
 
+6 #7 2012-02-05 13:07
Wabunge wa CCM naona mnapenda ubaguzi. CHDEMA nao wanahaki ya kukutana na Raisi na kuwasilisha hoja zao sio CCM tu.
Quote
 
 
+9 #6 2012-02-05 13:03
CCM haitakiwi walalamike wanatakiwa kujilaumu wenyewe kwa uzembe walioufanya kwa kupitisha miswada wanayojua kabisa ina mapungufu. Kwa nini wanaikataa miswaada yenye maslahi kwa watanzania? Pia sio CHADEMA peke yao waliokutana na Rais NCCR na CUF pia nao wamo
Quote
 
 
+7 #5 2012-02-05 12:47
Hali ya CCM ni mbaya kuliko hata uchumi wa nchi hii kwa sasa;si mbali sana nguvu ya uma itaamua
Quote
 
 
+9 #4 2012-02-05 12:15
Siku zote wabunge wa ccm wanachofikira ni maslai ya chama na si ya taifa..tunachotaka ni katiba nzuri ya watanzania bila kujali itikadi ya vyama.kwani hao ccm wanafikiri 2015 wataipata serikali..lah hasha haiwezekani.tumechoka na serikali ya kifisadi,kishka ji with no responsibilitie s.
Quote
 
 
+6 #3 2012-02-05 12:13
hapa ndipo unaona picha halisi ya viongozi tulionao wa ccm ni jinsi gani wanavyotaka kuendesha nchi kama ya kwao binafsi kwani Rais anasikiliza makundi yote na kutoa haki sawa wabunge wanachoangalia ni maslahi ya chama chao, hivi hawajifunzi kutoka nchi nyingine? wanadhani ccm itakaa madarakani milele? au wanadhani nchi ni ya ccm pekee?
Quote
 
 
+26 #2 2012-02-05 01:03
the end is near.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner