MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Mabadiliko CCM kuwang'oa mafisadi  Send to a friend
Tuesday, 14 February 2012 05:47

KINGUNGE ADAIWA KUPINGA, ASEMA HAYALENGI KUBORESHA MFUMO WA CHAMA
Midraji Ibrahim, Dodoma
SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitisha mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1977 juu ya namna ya kuwapata wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), imeelezwa kuwa mabadiliko hayo yanatarajiwa kuwa kitanzi kwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho tawala kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Juzi, Nec ya CCM ilibariki mabadiliko muhimu ya katiba ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa ndani ambayo ni pamoja na kuanzisha utaratibu ambao wajumbe wa NEC waliokuwa wanatoka mikoani, sasa watakuwa wanachaguliwa kutoka wilayani na wabunge, wawakilishi na madiwani sasa hawataruhusiwa kushika nyadhifa za chama.

Katika marekebisho hayo, viongozi wakuu wastaafu wakiwamo Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marais wa Zanzibar na makamu wenyeviti wa chama hicho, wameundiwa Baraza la Ushauri na sasa hawatakuwa wajumbe wa NEC.

Hata hivyo, uamuzi huo umepingwa vikali na baadhi ya wajumbe ambao walisema marekebisho hayo hayana tija zaidi ya kutaka kudhoofisha upande mmoja ambao uko kwenye harakati za urais mwaka 2015 na kuutaja kwamba, ni genge la watuhumiwa wa ufisadi.

“Wamejaribu kuondoa wazee wastaafu ili Kamati Kuu isiwe na watu ‘strong’, lakini yote hayo yanalenga kwa mtu siyo mfumo. Chama kinatakiwa kufanya marekebisho yake kwa mfumo siyo mtu... ngoja twende tutaona itakavyokuwa,” alisema mjumbe mmoja wa NEC ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Mjumbe mwingine ambaye pia hakutaja kutambushwa jina lake gazetini alisema uamuzi huo wa kurejesha nafasi hizo wilayani, unalenga kuwazuia baadhi ya watu wasiingie katika vikao hivyo vya uamuzi na kuwazuia watuhumiwa wa ufisadi kuweka watu wao katika wilaya zote nchini hata kama wana fedha.

Alisema hata kama watuhumiwa wa ufisadi wana fedha nyingi, itakuwa vigumu kwao kuweza kupandikiza watu wao katika wilaya zote nchini.

“Kwa hiyo sasa hivi angalau kutakuwa na mkakati wa kuhakikisha mafisadi hawaweki watu wao wengi wilayani. Kwani itakuwa vigumu kumudu kuweka wajumbe wa NEC wilaya zote nchini, lakini pia, wao wenyewe itawawia vigumu kupenya.”

Mwishoni mwa mwaka jana, mpango wa kujivua gamba ndani ya CCM uligonga ukuta katika kikao cha NEC hatua ambayo ilimfanya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kutumia busara na kurejesha utekelezaji wa mpango huo kwenye Kamati Kuu (CC) kwa utekelezaji.

Kingunge apinga
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru, ndiye mjumbe pekee aliyepinga marekebisho hayo, huku akiituhumu sekretarieti kwa kukiuka katiba ya chama hicho.

Kingunge anadaiwa kuwatuhumu Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kwa kuvunja katiba hiyo kutokana na Halmashauri Kuu kutokuwa na uwezo wa kupitisha marekebisho hayo zaidi ya kupendekeza kwa Mkutano Mkuu ambao ndiyo wenye mamlaka hayo.

"Mzee ametueleza wazi kabisa kwamba marekebisho hayo hayana maudhui zaidi ya kumlenga mtu mmoja, aliuza sekretarieti imepata wapi kwamba Halmashauri Kuu ina uwezo wa kufanya marekebisho haya?,” alisema mtoa habari hayo.

Lakini, katika utetezi wake, Sekretarieti ilisema kuna kifungu kinachotoa mamlaka hayo kwa NEC kupitisha marekebisho hayo na kutoa taarifa kwa Mkutano Mkuu. Hata hivyo, Kingunge hakukubaliana na hoja hiyo.

Ilielezwa pia kwamba marekebisho hayo yaliyopitishwa kwa kupigiwa kura na wajumbe kwa kupata theluthi tatu kutoka Tanzania Bara na nyingine tatu kutoka Visiwani, wote walikubali isipokuwa Kingunge pekee.

“Ila tulichojifunza kwa Mzee (Kingunge) ni kwamba lazima utetee unachokiamini hadi mwisho na alimtaka Katibu Mkuu kuandika kuwa amepiga kura ya hapana ili iwe kwenye kumbukumbu,” chanzo chetu kilieleza.

Hata hivyo, Kingunge alipotafutwa jana kwa simu kufafanua msimamo wake hakutaka kuzungumza chochote akisema kwamba alikuwa kikaoni...”Samahani niko kwenye kikao, asante.”

Yapokea taarifa ya Katiba Mpya

Katika hatua nyingine, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema Nec imepokea taarifa ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Tanzania na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa lakini ikaitaka Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, huku akitaka wanachama wao kujitokeza kutoa maoni pindi tume itakapoundwa.

Nape alisema mjadala ulikuwa iwapo Tume ya Maadili iundwe au la lakini kutokana na katiba kuruhusu kuundwa kwa tume mbalimbali wajumbe walikubaliana iundwe.

Aidha, alisema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alitoa taarifa ya mgomo wa madaktari na wajumbe waliitaka Serikali kuharakisha makubaliano yaliyofikiwa na iwe inachukua hatua kabla ya migomo kusababisha madhara kama ilivyotokea.

Uchaguzi Mdogo Arumeru
Alisema NEC imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM kwenye uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki na viti vinane vya udiwani vilivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, utaratibu utakaotumika katika nafasi ya ubunge ni ule wa kura za maoni kwenye mkutano mkuu wa jimbo na kwamba Februari 13 hadi 18 wagombea watachukua na kurejesha fomu. Februari 20, mkutano mkuu wa jimbo utapiga kura na kesho yake, kamati ya siasa ya Wilaya ya Arumeru itajadili wagombea na kutoa mapendekezo kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa ambayo itakutana Februari 24 na kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu ya CCM ambayo itakutana Februari 27.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Wednesday, 15 February 2012 00:35
 

Comments 

 
+1 #12 2012-02-14 20:58
mfa maji haishi kutapatapa
Quote
 
 
0 #11 2012-02-14 20:52
HIVI ILIKUAJE MFANYA BIASHARA MAARUFU AKAGOMBEA UBUNGE NA KUSHINDA KULE ZANZIBAR SASA KUNA SABABU ZIPI ZA KUMUENGUA ROSTAM AZIZ MBONA MNACHEKESHA NAKUBALIANA NA KINGUNGE KUWA KATIBA IMEKIUKWA KWA HALIMASHAURI KUU ITAPATA TAABU KUSHAWISHI MKUTATANO MKUU WAKUBALIANE NAO KINGUNGE ANAYEANDAA ILANI YA UCHAGUZI NI SAHIHI MABADILIKO YAMELENGA MTU WALA SI WATU KWENYE MCHEZO WA MPIRA NI HATARI SANA KUMLENGA MTU MMOJA TIMU HAISHINDI IKUMBUKWE MWENYE HELA SI MWENZIO NA MABEPARI WA NJE HAWAWEKEZI KWA WAJAMAA UCHWARA NI SABABU NCHI UKATA UMEZIDI HIVI HELA ZA KAMPENI NA UCHAGUZI MTAZIPATA WAPI ?KUCHANGISHA WANACHAMA MASKINI?
Quote
 
 
0 #10 2012-02-14 19:41
Samsonkiimbila@ yahoo.com
Quote
 
 
0 #9 2012-02-14 18:56
tuna waunga mkono asiliniamia kwau amuzi wenu
Quote
 
 
0 #8 2012-02-14 18:10
swala sio mkwe kama anaweza kuwatumikia watu wake vizuri tutampa kura ila kama ni mbabaishaji hatumpi ngooo! mbona hata mbowe amewa jaza marafiki zake kwenye ubunge wa kuteuliwa? ila kwakuwa ni wachapa kazi poa tu wanawajibika
Quote
 
 
0 #7 2012-02-14 17:06
kikwete,muheshi miwa wetu,weka mawaziri wa upinzani wasaidie hii nchi,angalia mboe alichokisema kuhus kadko,kia.achana na mawazo ya watu wanaokushinikiz a kuhusu vyama,angalia maendeleo ya nchi
Quote
 
 
-1 #6 2012-02-14 16:54
hivi mbona baadhi ya waTANZANIA mbona mmekosa ustaarabu kiasi hiki ni wapi mlisikia kuwa mwananchi amemkashifu rais akaachwa tu bila kifungo maana naona baadhi ya ma blogers wanaweka matokeo ya mtoto wa rais ktk blog zao kwani baba yake ndie aliyemwambia afeli au kwani yeye huyo mtoto si mtoto mtanzania kama wengine wanavyofeli acheni ushamba wananchi.akifaulu kapewa mtihani, HATA MWENYENZI MUNGU HAYUPO HIVYO TUBADILIKE
Quote
 
 
0 #5 2012-02-14 16:47
mzee kakasirika
Quote
 
 
0 #4 2012-02-14 16:28
ukweli ni kwamba mh.rais wa jamhuri ya muungano amefika mahali akakata tamaa ndo maana basi anashindwa kuchukua maamuzi mazito juu ya hao mafisadi. Na mh.rais wa jamhuri katika utendaji wako na waziri mkuu msimuogope yeyote fisadi kwani ukweli huishi na uongo hufa tena mapema. habari zikufikie mheshimiwa rais jamhuri ya muungano J.K.
Quote
 
 
-4 #3 2012-02-14 11:51
Impossible!!! hakuna cha kushuhulikia mafisadi wala waadilifu yaani waadilifu kupewa vyeo ila kila mtu ni chukua chako mapema. Sianini mpaka tuone na haitatokea. Washukiwa wa ufisadi kama mhe Lowassa ndiye anafaa kuwa Rais wa nchi hii kwani ni mchapa kazi.
Quote
 
 
+4 #2 2012-02-14 11:17
ccm jitahidinimambo sio lahisi2015
Quote
 
 
+1 #1 2012-02-14 08:51
Siyo rahisi kwa mafisadi kutoinfluence suala zima la uchaguzi. Kwa mfano Mwenyekiti wa Mafisadi Tanzania tayari keshampandikiza mkwe wake ambaye kamwoa bintiye ili awe mgombea wa ubunge Arumeru Mashariki kwa kofia ya chama chao cha magamba. Anaapa atahakikisha mkwewe anachukua jimbo ili kumuenzi "mzee"
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner