MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Afya za mawaziri watano ni tete  Send to a friend
Wednesday, 15 February 2012 21:27

WAWILI WAENDA INDIA KIMYAKIMYA, DK CHAMI AWA MBOGO, ASEMA WANAOSUBIRI KUONA WENZAO KWENYE MASANDUKU WATASUBIRI SANA
Waandishi wetu
WAKATI tetesi za kupanguliwa Baraza la Mawaziri zikizidi kupamba moto, hali ya afya ya baadhi ya mawaziri imeelezwa kuwa tete hivyo kulazimika kupelekwa India kwa matibabu.Miongoni mwa Mawaziri hao ni wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami ambaye jana aliibuka na kuwataka watu aliowaita wanye uchu wa kuchukua nafasi yake, waache mara moja kutumia afya yake kupiga propaganda chafu za kisiasa.

Hadi sasa, mawaziri ambao taarifa za kuugua kwao zinafahamika ni pamoja na Profesa Mark Mwandosya mwenye dhamana ya Maji, Naibu Waziri Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk Chami. Wengine ambao taarifa zinaonyesha kuwa walikuwa nje ya nchi  kwa matibabu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.

Ingawa haijafahamika maradhi yanayowasumbua hadi sasa, wadadisi wa mambo ya kisiasa wamekuwa wakichukulia hali ya afya ya baadhi yao kama moja ya sababu inayoweza kuwafanya wawekwe kando pale Rais Jakaya Kikwete atakapoamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kuwapa fursa ya kupumzika na kuendelea na matibabu.
Dk Chami

Dk Chami alisema jana kwamba tangu arejee kutoka India alikokwenda kutibiwa, afya yake imeimarika na hakuna siku aliyoshindwa kutekeleza majukumu yake huku akisema wanaoeneza uvumi huo ni mahasimu wake kisiasa wanaonyemelea nafasi yake.

Alisema mbali ya kufika ofisini kwake kila siku, alishiriki kikamilifu kwenye Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uliomalizika hivi karibuni Mjini Dodoma na kujibu hoja mbalimbali zilizoelekezwa kwa wizara yake.
Aliwalinganisha maadui zake kisiasa na fisi mwenye uchu anayemfuatilia mtu kwa nyuma bila kujali umbali wa safari kwa matumaini ya kuneemeka mkono ukidondoka huku akisema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri wake kwa vigezo anavyoona vinafaa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

“Nashangaa sana, afya yangu ni njema, imeimarika. Tangu nimerejea kutoka India, sijawahi kwenda hospitali wala zahanati yoyote, naingia ofisini kila siku kuanzia asubuhi na kutoka jioni, nimehudhuria Mkutano wa Bunge, Dodoma na leo nina kazi ya kutembelea viwanda, sasa huku ndiko afya yangu kuzidi kudorora?,” alihoji Dk Chami na kuongeza:
“Suala kubwa hapa ni uwaziri, lakini mtu unaposema fulani  anaumwa sana au haumwi lazima usimame katika ukweli.
Hizi ni propaganda chafu za kisiasa zinazoenezwa na baadhi ya watu wenye uchu wa kutaka nafasi hii. Rais ana mamlaka yake ya kuteua mtu kwa vigezo anavyoona vinafaa na mamlaka hiyo haitegemei afya ya mtu. Anaweza kuwa mzima au mgonjwa lakini anateua kwa kadri itakavyompendeza yeye.”

Dk Chami aliwataka wananchi wa jimbo lake la Moshi Vijijini kutokuwa na hofu kuhusu afya yake akisema imeimarika na  amejipanga kuongoza mapambano ya kuleta maendeleo.
    
Chami alirejea nchini mwishoni mwa mwaka jana kutoka India alikotibiwa kwa miezi miwili akiwashukuru Watanzania kwa moyo wa upendo walioonyesha kwake kwa baadhi yao kufunga na kufanya mikesha, kumuombea ili apone.

Kinachomsibu
Akizungumzia ugonjwa uliompeleka India, Waziri huyo alisema alikuwa akisumbuliwa na maumivu upande wa kulia wa kifua chake na alipofika India, ilibidi madaktari wamkate kipande cha nyama na kukisindika ili kutambua bakteria husika baada ya awali, kushindwa kuwabaini.

Alisema wakati akiendelea na tiba hiyo, dawa alizokuwa akizitumia zilimletea athari, iliyosababisha mwili kuvimba. Alisema kifua kilipata ahueni mapema na muda mrefu ulitumika kutibu uvimbe aliopata.
Akiwa katika ziara kutembelea kiwanda cha MMI Steel, Dk Chami alitumia fursa hiyo kuelezea pia afya yake akitamba yupo 'fiti' na hana mgogoro wa kiafya kama baadhi ya watu wanavyojaribu kumshinikiza Rais Kikwete afanye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

“Nipo vizuri sana na uzito umeongezeka kwa kilo 15. Sasa wale ambao wanafikiria kuwaona wengine katika masanduku (majeneza) watasubiri sana” alisema.

Kombani na Chikawe
WaziriKombani alipelekwa nje ya nchi kutibiwa na sasa amerejea nchini. Awali, taarifa zilisema alipaswa kwenda kufanyiwa upasuaji ambao hata hivyo, haukuwekwa wazi.
Waziri huyo hakuonekana katika Mkutano wa Sita wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema ndiye aliyekuwa akijibu maswali ya Wizara Katiba na Sheria.

Jana, taarifa zilizopatikana wizarani kwake zilisema Kombani hajaonekana ofisini kwa takribani wiki tatu.
Baadhi ya vigogo wa wizara hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, walisema waziri huyo hayupo ofisini kutokana na kuumwa na kwamba alikuwa nje ya nchi wa matibabu kwa takriban wiki tatu.

Msemaji wa wizara hiyo, Omega Ng’ole alisema hajui kama Waziri Kombani alikuwa anaumwa huku akisema waziri kwenda nje au kutokwenda kwa ajili ya matibabu ni suala binafsi hivyo kushauri atafutwe mwenyewe.

Akizungumza kwa simu, kuhusu afya yake Kombani alihoji: “Unataka kufahamu kama mwandishi au ndugu?” baada ya kujibiwa alisema si jambo baya kwa kiongozi kwenda au kupelekwa nje ya nchi kutibiwa.

“Hivi mtu kuumwa ni jambo la kutangaza kweli… nini cha kushangaza kama mtu akiumwa?,” alihoji.

Alisisitiza kwamba, hakuna ubaya kwa kiongozi yoyote kwenda nje ya nchi kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

“Mtu akienda nje kufanyiwa uchunguzi hiyo nayo ni habari? Hilo jambo kwangu ni mambo madogo tu, hiyo siyo habari bwana,” alisema Kombani na kuongeza kuwa hawezi kusema kama ni mgonjwa au la kwa kuwa hilo ni jambo lake binafsi... “Mimi nakwenda nje kila siku, kila wakati katika shughuli zangu za kikazi na hata siku moja sijawahi kuulizwa na mtu.”

Kwa upande wake, Waziri Chikawe naye anadaiwa kwamba hivi karibuni alikwenda India kupata matibabu. Hata hivyo, haikuelezwa kinachomsibu kutokana na usiri mkubwa uliopo serikalini juu ya matibabu ya viongozi hao.

Dk Mwakyembe
Dk Mwakyembe ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi na kupelekwa India Oktoba 9 mwaka jana, anatarajiwa kwenda tena nchini humo wakati wowote kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.

Mmoja wa watu wa karibu na Dk Mwakyembe alisema juzi kwamba Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anatarajiwa kurudi katika Hospitali ya Appolo kwa ajili ya kuangalia kama matibabu aliyopata yamemsaidia kwa kiwango gani.

Ingawa Dk Mwakyembe alijitokeza hadharani katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe hivi karibuni, hali ya afya yake haikuwa ya kuridhisha kutokana na ngozi yake kuonekana imeathirika.

Profesa Mwandosya
Profesa Mwandosya ambaye amekuwa akitajwa kama mmoja wa makada wa CCM ambao wangeweza kuwa tishio katika mbio za urais ndani ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Appolo kwa zaidi ya miezi mitatu. Sasa hivi, Waziri Mwandosya nchini India ambako anaendelea kupata matibabu.

Ikulu
Kuhusu taarifa za kuwepo kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Kurugenzi ya Mawasiliano imesema wajibu wa kubadilisha baraza hilo uko kwa Rais ikiwa ataona kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana jioni alipokuwa akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds FM na kusisitiza: “Rais atakapoamua kufanya hivyo atafanya kwa matakwa yake mwenyewe.”

Habari hii imeandikwa na Joseph Zablon, Keneth Goliama, Fidelis Butahe na Boniface Meena.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 16 February 2012 23:55
 

Comments 

 
0 #30 2012-04-24 14:20
kwani kumwa wao ndo iwetabu kama wanaitajika kuukumiwa kutokana namakosa yao basi sheria ichkue mkondo wake au kama vipi wahukumiwe wakiwa huko huko hospitali
Quote
 
 
0 #29 2012-04-20 02:16
watanzana tumezidi
kwa majungu na ndo maana hatuendelei
Quote
 
 
0 #28 2012-03-21 12:31
muguawabaliki wenzetu wenye uhakika wakutibiwa india sisi tutafia hapahapa mungu tusaidie waja wako hatuna chakutegemea zaidi yako amina
Quote
 
 
+1 #27 2012-02-17 09:45
Mi naona wasifanye mabadiriko ya haraka wata waua wenzao siku si zao.

Na mnao mtesa mwakyembe, wenzenu tuna mwita OBAMA
Quote
 
 
0 #26 2012-02-16 20:42
WAANDISHI WA HABARI HIVI MMEKOSA HABARI YA KUANDIKA TAARIFA ZA MAWAZIRI WANAKWENDA KUTIBIWA ZINA TIJA GANI KWA WATANZANIA KAMA SIO MAJUNGU ?
Quote
 
 
0 #25 2012-02-16 18:47
Hii labda itawakumbusha kuwa kufa kupo palepale hata kama wanahisi hawafi kwa mihela na kodi za wananchi wanazotumbua !!!!!!
Quote
 
 
0 #24 2012-02-16 18:42
Viongozi kutibiwa nje ni tatizo kwani kiongozi anapaswa kuonyesha mfano na siyo kujipendelea, ikiwa wewe kiongozi unaona hospitali za hapa nchini hazina huduma za kufaa kutibu magonjwa wawezaje kumhamasisha unayemwongoza atibiwe hapo? Mlipaswa kuziboresha hospitali zetu kwa kuhakikisha zina wataalam wa kutosha na zina dawa aina zote na za kutosha, lakini badala yake mnakimbilia India na kuwaacha wananchi watibiwe kwenye hospitali zisizo na dawa, hivi kweli hiyo ni sahihi? Hamuoni kama mnatuongezea wananchi mizigo mikubwa ya kuwatibisha wakati ninyi hamtutumikii ipasavyo? badala ya kuweka ruzuku kwa wananchi mnatubebesha mizigo mikubwa. kodi za wafanyakazi wa serikali ziko juu sana na kuwaachia kipato kidogo mno wakati ninyi mishahara yenu haikatwi kodi yoyote, Je hiyo ni sahihi? bei za umeme na huduma mbalimbali kwa jamii ziko juu hapo napo ni wananchi wanabeba mizigo hakuna ruzuku wala msaada. licha ya hivyo serikali ni kubwa mno wizara za serikali, mikoa na wilaya zake vinazidi kuongezeka kila kukicha, ili kutengeneza ulaji kwa maswahiba. Government spending is too big na kwa sababu hiyo mambo yamekwama, kwa hali hii niionayo kweli tutafika? Maisha bora kwa kila Mtanzania yako wapi ama maisha bora yalilenga kwa viongozi tu?
Quote
 
 
-1 #23 2012-02-16 18:23
Hivi kuumwa ni ajabu? Mbona waandishi mnataka sana kujua habari za kuumwa za Mawaziri? Mbona ninyi mnapoumwa hamjiandiki magazetini. Raisi yupo aliyewaweka kama upo utekelezaji ambao haufanyiki atajua cha kufanya yeye. Andikeni habari za maendeleo ya Wananchi na zile ambazo zinahusu kutotekelezwa. Ukijua ugonjwa wa Kombani, Mwakyembe, Chami n.k tutapata maendeleo kiasi gani. Acheni umbea
Quote
 
 
0 #22 2012-02-16 18:03
Ugonjwa ni kwa wote jamani, kwani wao nani wasiugue? Hakuna hospitali yenye kitanda cha ziada vyote vimejaa, sote tumeumbwa na uwazri ni cheo tu si utu wa ziada. TUNACHOoMBA RAIS ASIFANYE MABADILIKO BALI UTEUZI MPYA PALE ANAPOONA NAFASI INAHITAJIKA KWANI HUO NDIO UTENDAJI MWEMA UTAKAOONDOA MAZOEA YA VYEO AMBAYO YANAPUNGUZA UTENDAJi. MUNGU WABARIKI WATANZANIA!
Quote
 
 
0 #21 2012-02-16 17:29
Mhe Celina na Chami mnatushangaza watanzania. Kumbukeni Mficha magonjwa kilio kitamuumbua.
Quote
 
 
+2 #20 2012-02-16 17:18
hafu mimi nashangaaa saaaana wezi wote mwendo mdundo wapiganaji homa na malaria kila kukicha au ndiyo mpango mwenyewe wa kuwaua wapinaji ili wezi waendelee kuhondomola mwanawane? ka nchi ketu haka tanganyika? kazi kwelikweli!
Quote
 
 
0 #19 2012-02-16 15:33
Quoting Dr Eng:
Tuwaombee mawaziri wetu kwa Mwenyezi Mungu ili awabariki na kuwaponya. Tumwachie Rais atoe uamuzi katika kupanga au kupangua baraza lake. Nia isiwe kuwakomoa mawaziri, bali kuendeleza utekelezaji wa kasi inayotakiwa katika utendaji. Mungu Ibariki Tanzania

Me nachukia sana jinsi pesa yetu inavyotumika vibaya jirudini. Na muache kuwekeana sumu, mnamuua Mwakyembe wetu sasa
Quote
 
 
0 #18 2012-02-16 14:54
Inasikitisha sana kwa matumizi makubwa hivi ya kutibu mawaziri hawa. Sio haki kabisa kwa mtanzania maskini asiye na chakula cha leo jioni. Mtaadhibiwa na Mungu. Ona mitoto yenu inavyofeli shuleni. hiyo ni ole wenu. Afadhali Mwakyembe tunajua ni mtetezi wa wanyonge na wakampa sumu...wengine hata iweje malipo ni hapa hapa
Quote
 
 
0 #17 2012-02-16 14:06
Ama kweli hicho ndo kihama kwa nchi masikini.waacheni wakatibiwe India iko siku tutashitaki kwa mungu na asipotusikia tutawashitaki kwa sheteni, na kitaeleweka tu.
Quote
 
 
-1 #16 2012-02-16 14:02
Hakuna anaye penda fulani kuugua ila tunacho jiuliza kulikoni kilamara Apollo India,kwani vifaa vya apollo havinunuliki vikawa hapa kwetu na kuwatumia Madaktari bingwa wa kwetu,huku ni kudhalilisha taaluma ya Afya hapa nchini,TUNAITAK A APOLLO YETU HAPA TZ NA WALALAHOI TUFAIDIKE NAYO!!!.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner