
| Dk Slaa atajwa Urais Chadema | Send to a friend |
| Wednesday, 21 July 2010 08:32 |
|
Mussa Mkama ![]() KAMATI kuu ya Chadema jana ilikutana jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mkakati wa kumpata mgombea urais wa chama hicho baada ya mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kuamua kugombea ubunge. Habari kutoka kwa viongozi wa chama hicho zinasema kuwa mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa ndiye anayeangaliwa zaidi kushauriwa kujitosa kwenye nafasi hiyo baada ya mjumbe wa kamati kuu, Profesa Mwesiga Baregu kugoma kugombea urais. Tayari Dk Slaa ameshachukua fomu za kutetea kiti chake cha ubunge cha Karatu, lakini habari zinasema kuwa Chadema inamtaka katibu huyo mkuu kugombea urais baada ya kulichangamsha Bunge kwa hoja nzito katika vipindi vyake alivyolitumikia jimbo hilo. Chadema, ambacho kimeongezeka nguvu katika kipindi cha miaka mitano baada ya kuingiza wanachama machachari ndani ya Bunge, imekuwa ikisaka mgombea urais ambaye ataweza kuendeleza umaarufu wa chama hicho na vyombo vya habari vimekihusisha chama hicho na mipango ya kumshawishi waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye na Spika wa Bunge, Samuel Sitta kuingia kwenye mbio za urais kwa tiketi ya chama hicho. Hata hivyo, taarifa za vyombo vya habari zimeeleza kuwa vigogo hao wawili wa CCM wamekataa kukiasi chama chao. Katika uchaguzi mkuu uliopita, Mbowe alishika nafasi ya tatu kwenye harakati za kuingia Ikulu baada ya kufanya kampeni zilizogusa sehemu kubwa ya nchi, akitumia helikopta, lakini safari hii atagombea ubunge wa Jimbo la Hai. Kama Dk Slaa atajitosa kugombea urais kwa tikei ya Chadema, CCM watakuwa wamepata mteremko wa kuchukua jimbo la Karatu ambalo wamekuwa wakilisaka kwa udi na uvumba. Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika alikataa kuzungumzia kikao hicho na kueleza kuwa waandishi watapewa taarifa kamili leo. “Baada ya kikao kumalizika kesho, tutaitisha mkutano na waandishi wa habari... kitafanyika wapi na saa ngapi tutawajulisha usiku,” alisema Mnyika. Tayari CCM imeshamteua mwenyekiti wakr, Jakaya Kikwete kuwa mgombea urais wakati CUF imemteua tena Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea wake. Mwenyekiti wa TLP, Agustine Mrema naye hatagombea urais kwa tiketi ya chama hicho baada ya kuamua kurejea Vunjo kugombea ubunge. Mrema pia alishawahi kuwa mbunge wa Temeke.. |
| Last Updated on Thursday, 22 July 2010 08:08 |
















Comments
nasema hivi kwa kua kama wapo wanaofahamu Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini duniani basi ni mimi na wewe ambao tunatumia Internet na kufuatilia habari kwa ajili ya kazi zetu za kila siku. hadi leo nina hakika asilimia zaidi ya 50 hawafahamu ni nini richmond, epa wala kagoda. katika hao wanaofahamu basi wapo wanaopongeza hatua zilizochukuliwa na viongozi walioko madarakani eti kulishughulikia , pia kuna wanafiki wanaokunja uso kuponda yaliyofanyika lakini mioyoni mwao wanaimani kubwa na uongozi ulioko madarakani eti umefanya vizuri. tuliobaki ukweli ni kwamba tupo kidogo tusiokubali hali hii tuliyonayo. na hivyo mchango wettu kumueka dokta slaa madarakani utakua mdogo. ingekua Zanzibar Dr. angepita kwa kua ZNZ CCM sasa inashinda kwa kupindisha sheria, kutumia nguvu, vitisho, na wizi wa dhahiri lakini wananchi wameshaikataa. kwa hiyo nashauri tuangalie njia nyengine kwa docta ila uraisi itahitaji nguvu ya ziada na muda wa miezi mitatu hautoshi jamani. haya ni mawazo yangu
Nawashauri vyama vya siasa muda bado wa kuingoa CCM mwalimu alisema labda miaka 40 ndio CCM itatoka madarakani huu ni msemo wa kweli tu. Mimi nafikiri vingozi wote wa vyama vya upinzani wa ngazi ya taifa chukuweni fomu za ubunge kwani kuishinda CCM ni kuwa na viti vingi vya ubunge ili kila jambo ambalo si manufaa kwa watanzania halitapita kiurahisi kwa kura nyingi ambazo CCM wana viti vingi Bungeni, mkifanya hivyo tutaweza kuishinda CCM kwa hoja ambazo si za msingi kwa watanzania. nawashauri hivyo kwani katika uraisi CCM wamejipanga ila kwa wabunge hakuna hoja ingawa mimi ni sina chama chochote cha siasa.
Yaani huyu jamaa sijui kama akili zake za kupambambanua mambo ziko sawasawa. Yaani akiwekwa Jk na Dr. Slaa kwa kusimamia hoja za msingi JK ataweza? Mfano ni hotuba ya kuahirisha Bunge kwenye mambo ya msingi ambayo yalikuwa ya kukalipia yeye alikuwa anacheka tena peke yake. Bwana Acha watanzania wanaotaka wananchi waneemeke washike nchi. Si kwamba CCM wote ni mabomu la!!! kuna vichwa vizuri tu lakini vimezungukwa na watu wasio faaa.
Kwanza ww kama ww, amua kwamba utampa kura dr, halafu angalia familia yako, marafiki na jamaa zako wote, upande wa wafanyakazi sina shaka kura amepata
....Kimsingi napenda kuheshimu mawazo ya watanzania wenzangu lakini pale yanapokuwa chini ya Kiwango cha uelewa wa Darasa la VII lazima tuseme, huyu Bana kinachomsumbua ni ushabiki wa undugu,uhasama, umbea au uwanaCCM ambao mimi ndo naufahamu kuliko yeye aliyeishia Kilima Tembo? Garma naas jiulize unawatakia mema watanzania au unajali zaidi maslahi yako? Umekuwa mpofu hauna mfano...wairaqw hatuna dalili ya ushabiki pasipo ukweli wa jambo. Ebu waeleze watanzania upungufu wa Sla'a' kuwa Rais tofauti na Kikwete. Tuache unafiki,nataka nijue ukweli wa moyo wako.
Ninyi ndo watu ambao hatuwahitaji kabisa katika nchi yetu maana akili zenu bado ni finyu,hivi huoni kuwa unachokisema hujui maanayake! Kwa maana umekariri vibaya aliyoyasema mwalimu,kama huji ni bora uulize ili uambiwe na kufafanuliwa maana yake,kama hutapata wa kukufafanulia fikiria hotuba ya mwalimu aliitoa katika mazingira gani na wapi na kwa lengo gani! Usikariri! Kwa taarifa yako huu ni mda mwafaka wa kuhitaji mabadiliko;na hata kama hatutayapata wajukuu wetu watayaleta na kuishi maisha bora kuliko haya ya ushabiki na kuacha ndugu zetu vijijini wakifa kwa njaa na huduma duni za kiafya,eeeeeeee eeeeeee mungu ibariki Tanzania,AMEN