
| Pingamizi la Chadema kwa JK latua kwa Msajili | Send to a friend |
| Tuesday, 31 August 2010 00:21 |
Geofrey Nyang’oroCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeteketeza azma yake ya kumwekea pingamizi mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete. Taarifa zimeeleza kuwa chama hicho kiliwasilisha pingamizi hilo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini jana saa 7:30 mchana. Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, ndiye aliyewasilisha pingamizi hilo. Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alipoulizwa hakutaka kukubali au kukataa kuliona pingamizi hilo na akasema atazungumzia suala hilo leo. Awali Chadema ilipanga kuweka pingamizi hilo la kutaka Kikwete azuiwe kugombea urais, Agosti 27 mwaka huu, lakini, ilisitisha kwa kile ilichoeleza kuwa inasubiri mambo mengi zaidi ambayo wangeyaingiza kwenye pingamizi hilo. Chama hicho awali kilitaka kuweka pingamizi hilo kwa kile kilichoeleza kuwa Rais Kikwete amekiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi kwenye kampeni. "Tulishindwa kupeleka pingamizi hilo jana kwa sababu tumesikia kwamba huku anakoendelea na kampeni zake, mgombea huyo ameendelea kufanya makosa mengine ambayo tutataka tuyaingize kwenye pingamizi hilo," alisema Mnyika mwishoni mwa wiki. Akizungumza na gazeti hili jana muda mfupi baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Mnyika alibainisha kuwa mambo mengine mapya yaliyoingizwa kwenye pingamizi hilo ni mgombea huyo wa CCM kuahidi kukilipia Chama cha Ushirika cha Nyanza deni la Sh 5 bilioni na kuahidi kununua meli kwa ajili ya watu wa mikoa ya Kagera na Mwanza. Mnyika alisema tayari Chadema imewasilisha pingamizi hilo jana lakini, ina mashaka kama ofisi ya msajili itawatendea haki. “Sisi tumeshawasilisha pingamizi letu kwa msajili wa vyama vya siasa kama Sheria ya Gharama za Uchaguzi zinavyoelekeza, lakini, tuna tumaini lenye shaka ndani yake kama tutatendewa haki,”alisema Mnyika na kuongeza. “Mheshimiwa Kikwete wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi, moja kwa moja akitumia nafasi yake kama rais, ameongeza na /au kuahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa kupandisha kima cha chini kutoka Sh130,000 hadi Sh235,000,”inasema sehemu ya kwanza ya pingamizi hilo lenye sehemu tatu. Katika pingamizi hilo, Chadema pia ilieleza kuwa mgombea huyo wa CCM, ameahidi kutoa Sh5 bilioni kwa chama cha Ushirika cha Nyanza ili kilipe madeni yake mbalimbali na kuahidi kuwa serikali itachukua madeni yote ya vyama vya ushirika. Chadema pia imesema katika sehemu ya tatu ya pingamizi hilo kuwa mgombea Kikwete alitumia nafasi yake kwa kuwaahidi watu wa mkoa wa Kagera kuwa atawanunulia Meli mpya, kubwa na ya kisasa. "Ahadi hizo ni sehemu ya mambo yaliyokatazwa kwa mujibu wa kifungu cha 21 (1) (a) na (e) cha Sheria ya Gharama za Uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010," imeendelea sehemu ya pingamizi hilo. Mnyika alifafanua kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo, vitendo hivyo vilikuwa na nia ya kushawishi wapigakura wampigie kura mgombea huyo wa CCM. Kuhusu ahadi ya kuchukua madeni ya Chama cha Ushirika cha Nyanza, alisema kitendo hicho nacho kililenga kuwashawishi wananchi wa Mkoa wa Mwanza kumpigia kura. “Nyongeza ya mishahara, ahadi ya Sh5 bilioni na ahadi ya meli kutumika kama hongo/rushwa kwa hao wote wahusika ili wampigie kura Kikwete," alisema Mnyika na kueleza kifungu kinachozuia mambo hayo kuwa kinasema: "Mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa na kama ilivyoelezwa katika sehemu hii, atakuwa, au, kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki katika mchakato wa uteuzi na uchaguzi.” Wakati huo huo, mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amemshukia Meneja wa Kamati ya Kampeni CCM, Abdulrahman Kinana na kumtaka anyamaze kwani katika orodha ya uchafu wa watuhumiwa wa ufisadi nchini hatoki. Juzi Kinana aliwaambia waandishi wa habari kwamba, Dk Slaa anawadanganya wananchi kuhusu suala la ufisadi na kumtaka aache kufanya hivyo na anadi sera zake. Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara katika Jimbo la Mikumi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro jana, Dk Slaa alisema fisadi ni fisadi tu na hana njia nyingine ya kumpamba kwa maneno mazuri mtu anayeiba mali za umma. “Namuonya Kinana anyamaze, nisije nikamshukia kwa sababu katika orodha ya wana-CCM waliofanya uchafu hatoki kupitia kampuni zake,” alisema Dk Slaa. Dk Slaa alimgeukia Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo kwamba pamoja na cheo chake cha uwaziri na ubunge katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, lakini wilaya yake ni moja kati ya tano zilizopata orodha chafu sana . Dk Slaa anaendelea ziara zake za kampeni na leo anatarajia kufanya mikutano kadhaa katika mkoa wa Dodoma kwa kutumia usafiri wa helikopta. |
| Last Updated on Wednesday, 01 September 2010 01:12 |



Geofrey Nyang’oro











Comments
Wakari Dr.Slaa (mtumishi wa Mungu na mtumishi mwaminifu wa watu)anaainisha hoja za ufisadi,kutokuw ajibika na ukosefu waa maadili kama visababisho vikubwa vya kudumaa kwa Tanzania yetu kiuchumi,kisias a na kijamii.Na huku akitoa mapendekezo ya kitafiti yenye kutoa maono juu ya suluhisho la matatizo tetu,watu (wenye akili za ndiyo mzee)wanajibu hoja kwa kumtuhumu kwa kuacha upadre na kuingia kwenye siasa...MZAHA WA KINDONDOCHA!
Kimsingi,kwa mujibu wa dhana na falsafa ya Mabadiliko,kila mwenye akili timamu anajua nchi hii inahitaji mapinduzi(a complete change).Maono ya Dr.Slaa ni mabadiliko ya nchi yetu kimfumo,kifikya ,kimkakati na kiutashi,hasa utashi wa kisiasa.Na hapa tunaruhusiwa kuiga kwa vitendo, kauli mbiu iliyobadilisha historia ya Marekani, YES WE CAN!
Ndani ya miaka karibia 40 CCM imeonyesha kujaribu na kushindwa KABISA kusimamia mabadiliko hayo.Nimesema imejaribu mana nafahamu kimkakati kuna wakati Tanzania ilijengewa misingi ya utengamavu hasa na waasisi wake,wakiongozw a na (Mwenye heri) Mwl.Nyerere.Misingi hii hata hivyo imeshabomoka kwa namna isiyoweza kutengenezwa na walioibomoa...DHIKI KUU!
Jakaya kikwete (nafahamu hapendi kuitwa Doctor,mnampaka zia tu) alijitokea kam nuru ya asuuhi yenye matumaini chanya, Mtanzania nikasema"I think we gat somebody". Akakuruka pale mwanzo kwa ari kasi na nguvu mpya ndani ya kiriba cha zamani.Na kama maandiko matakatifu yasemavyo kwa habari ya ubora wa dhahabu kupimwa na moto; Ghafla dhahabu kikwete ikapitishwa kwenye moto wa "List of shame" kutahamaki chali mtoto wa Bagamoyo.....NGUVU YA SODA?
Anahitajika kiongozi anayetoka kwenye mfumo tofauti kupambana na ufisadi na kuushinda.Mana ni kweli Kikwete amepambambana na ufisadi kama aimbavyo makamba kila kukicha,lakini amepambana na kushindwa vibaya....AIBU!
Inashangaza kuwa wamemaliza "style" za kutudanganya na sasa wameamua kudanganyana wenyewe kwa msemo wa kifedhuli-tuliahidi,TUMET ELEKEZA! Jibu letu sabari hii ni jepesi sana...HATUDANGANYIKI! !
Tunahitaji kiongozi mwenye "Moral Authority" na si kutisha kwa nguvu za kimtandao wala kidola.Maana yake ni rahisi tu, kwamba huwezi kupambana na ufisadi kama nawe unanukia ufisadi.
Miaka 15 ya ubunge wa Daktari Slaa,halmashaur i ya Karatu imekuwa ikipata HATI SAFI kwa mipango,mikakat i na matumizi bora na yenye kuthamini pesa za maskini wa Tanzania.kama kiongozi, Dr amejitengenezea "authority" ya kunyooshea vidole waliofuja pesa za umma.
Je kikwete anaweza kukemea matumizi mabaya ya pesa za umma huku mawaziri wake wakitembea na zahanati nne za kisasa baranbarani?(Kwa mahesabu ya Dr Slaa, kila shangingi moja linathamani sawa na zahanati nne za sh. Milioni 50 kila moja) .
Ni mengi ya kuandika lakini lamaana hapa ni nchi yetu. Si kikwete, si slaa, wala vyama vya siasa na propaganda zao.Muda wa kulaumu umeshapita.Sasa ni muda wa kufikiri kwa vitendo.Ni mihimu watu tuamue sasa kama tunayahitaji kuboresha maisha yetu.
Mfumo wa Dunia ya sasa unalazimisha siasa kutegemeza nyanja zingine katika maisha ya mwanadamu hasa wa nchi zinazoendelea(p olitical determinism).Hatahivyo, ni mihimu sasa, wasomi wetu wakasaidia kuelimisha na kupevusha fikra za wananchi wote,tuwe na ufahanu wa msingi wa masuala ya msingi hasa yahusuyo uongozi wa kisiasa wa nchi yetu, na baadaye kuoanisha kiurari unaofaa na nyanja zingine muhimu kama uchumi na sekta ya kijamii,kwa namna ya kuwezesha mfumo wa kila sekta kutekeleza wajibu wake na huku zikisaidiana na kutegemeana(Str uctural Function) katika kuwaleta watanzania Maisha Bora na sio ahadi za Bora Maisha.
Miaka mitano imepita, Mama demokrasia anatupatia tena nafasi ya kuacha uchuro wa kukaa uchi wakati nguo tunazo!
kupiga miayo wakati ghala imejaa chakula!
Ni nafasi nyingine ya kuthaminisha maisha yetu na kupanga bei ya utu wetu.
Ni nafasi nyingine Mungu ametoa ya kufanya maamuzi mazito juu ya UHAI WETU na uhai wa Taifa letu.
Kila mtu aongozwe na utashi wa moyo wake na si utashi wa fulana, mabando wala ngonjera...ukisikiliza sauti ya ndani kabisa, kwa uaminifu kabisa na huku ukijaribu kufikiri kuwa utakaloamua ndilo kusudi la MUNGU; ukifikia hatua ya tafakuri ya namna hii, hakika utagundua kwa urahisi kabisa ni nani hasa anafaa kupewa kura yako, kwa uraisi, ubunge na udiwani.
Mungu Ibariki Tanzania
Uchaguzi mwema wapendwa
Robert LENGEJU
Morogoro,Tanzan ia
Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akatata wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.
Ni Dr. Slaa aliesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuelekeza zaidi kwa watanzania, ni Dr.Slaa amesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma, ni Dr.Slaa amekuwa mtanzania baada ya nyerere kutoa hoja zinazomlenga mtanzania maskini, ni Dr.Slaa anaeweza kuthibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr.Slaa anaeweza kuwapa elimu bure watoto wetu pale mlimani achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao nyerere aliwatoza ada? kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?
Ni Dr. Slaa anaeongelea treni ya umeme kwenda kigoma, Dodoma, Tabora, na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters. Ni Dr.Slaa anaeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. kwani kuna tofauti gani kati ya Tanzania, Kenya na Ethiopia, ambako ni chini ya 20 ya pesa yao? kwanini sisi tuna kasoro gani kuwa maskini kiasi kwamba mtu asafiri kutoka ethiopia kuja Dar es salaam afike kabla ya mtu anayetoka Kariakoo kwenda Mwenge?
Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya buzwagi, geita, bulyankulu, tulawaka,nzega, tanzanite hawa wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr.Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shinilingi 350 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.
Ni Dr.Slaa anaeweza kusimamia mashirika ya jamii kuleta tija achana na CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirkia yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.
Ni Dr. Slaa ambae amepanga kubadili katiba ili Rais afuite matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa? Hivi inaingia akilini kweli? hata kama mtu anasemwa ni fisadi hakuna hatua yoyote -naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu -katika hotoba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.
CCM hawawezi hayo? eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo! Ni
Dr.Slaa anaeweza kufanya hayo si tumeona mnazi mmoja aliwataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu. Je akiwa rais watakimbia nchi nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupue muone moto utakavyowaka? Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati-jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, kigoma, mbeya,lindi, mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?
Nani asiye jua madakitari wetu wengi bingwa wapo botswana wakati hapa kwetu watu wanakufa tu? Nani asiejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??
Jamani wafanyakzi, wakulima, na wanafunzi ni jukumu letu kupeleka habari hata kama vyombo vyetu vya habari ni vya hao hao. Hawasemi tu ukweli, hata wao ni maskini na wanakubali kupitia vyombo vyao tuendeee kusema piga na shavu la kushoto.
Ni Dr. Slaaa, mzalendo wa kweli na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila kitu. Naona huruma wenzangu waliokunywa maji ya bandari.
Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? wamekosa nini hawa? Jamani tuache woga inawezekana. Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumia. Tumtume Dr.Slaa kuwakurupusha wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi.
Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana tena ni rahisi. Peleke ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela.
Wakari Dr.Slaa (mtumishi wa Mungu na mtumishi mwaminifu wa watu)anaainisha hoja za ufisadi,kutokuw ajibika na ukosefu waa maadili kama visababisho vikubwa vya kudumaa kwa Tanzania yetu kiuchumi,kisias a na kijamii.Na huku akitoa mapendekezo ya kitafiti yenye kutoa maono juu ya suluhisho la matatizo tetu,watu (wenye akili za ndiyo mzee)wanajibu hoja kwa kumtuhumu kwa kuacha upadre na kuingia kwenye siasa.
Kimsingi,kwa mujibu wa dhana na falsafa ya Mabadiliko,kila mwenye akili timamu anajua nchi hii inahitaji mapinduzi(a complete change).Maono ya Dr.Slaa ni mabadiliko ya nchi yetu kimfumo,kifikya ,kimkakati na kiutashi,hasa utashi wa kisiasa.
Ndani ya miaka karibia 40 CCM imeonyesha kujaribu na kushindwa kusomamia mabadiliko hayo.Nimesema imejaribu mana nafahamu kimkakati kuna wakati Tanzania ilijengewa misingi ya utengamavu hasa na waasisi wake,wakiongozw a na Mwenye heri Mwl.Nyerere.Misingi hii hata hivyo imeshabomoka kwa namna isiyoweza kutengenezwa na walioibomoa.
Jakaya kikwete (nafahamu hapendi kuitwa Doctor,mnampaka zia tu) alijitokea kam nuru ya asuuhi yenye matumaini chanya, Mtanzania nikasema"I think we gat somebody". Akakukuruka pale mwanzo kwa ari kasi na nguvu mpya ndani ya kiriba cha zamani.Ghafla dhahabu kikwete ikapimwa na moyo wa "List of shame" kutahamaki chali mtoto wa Bagamoyo!
Alihitajika kiongozi anayetoka kwenye mfumo tofauti kupambana na ufisadi na kuushinda.Mana ni kweli Kikwete amepambambana na ufisadi kama aimbavyo makamba kila kukicha,lakini amepambana na kushindwa vibaya!
Tunahitaji kiongozi mwenye "Moral Authority" na si kutisha kwa nguvu za kimtandao wala kidola.Maana yake ni rahisi tu, kwamba huwezi kupambana na ufisadi kama nawe unanukia ufisadi.
Miaka 15 ya ubunge wa Daktari Slaa,halmashaur i ya Karatu imekuwa ikipata HATI SAFI kwa mipango,mikakat i na matumizi bora na yenye kuthamini pesa za maskini wa Tanzania.kama kiongozi, Dr amejitengenezea "authority" ya kunyooshea vidole waliofuja pesa za umma.
Je kikwete anaweza kukemea matumizi mabaya ya pesa za umma huku mawaziri wake wakitembea na zahanati nne za kisasa baranbarani?(Kwa mahesabu ya Dr Slaa, kila shangingi moja linathamani sawa na zahanati nne za sh. Milioni 50 kila moja) .
Ni mengi ya kuandika lakini lamaana hapa ni nchi yetu. Si kikwete, si slaa, wala vyama vya siasa na propaganda zao.Muda wa kulaumu umeshapita.Sasa ni muda wa kufikiri kwa vitendo.Ni mihimu watu tuamue sasa kama tunayahitaji maisha bora ama la.
Mfumo wa Dunia ya sasa unalazimisha siasa kutegemeza nyanja zingine katika maisha ya mwanadamu hasa wa nchi zinazoendelea(p olitical determinism).Hatahivyo, ni mihimu sasa, wasomi wetu wakasaidia kuelimisha na kupevusha fikra za wananchi wote,tuwe na ufahanu wa msingi wa masuala ya msingi hasa yahusuyo uongozi wa kisiasa wa nchi yetu, na baadaye kuoanisha kiurari unaofaa na nyanja zingine muhimu kama uchumi na sekta ya kijamii,kwa namna ya kuwezesha mfumo wa kila sekta kutekeleza wajibu wake na huku zikisaidiana na kutegemeana(Str uctural Function) katika kuwaleta watanzania Maisha Bora na sio ahadi za Bora Maisha.
Miaka mitano imepita, Mama demokrasia anatupatia tena nafasi ya kuacha uchuro wa kukaa uchi wakati nguo tunazo!
kupiga miayo wakati ghala imejaa chakula!
NI nafasi nyingine ya kuthaminisha maisha yetu na kupanga bei ya utu wetu.
Ni nafasi nyingine Mungu ametoa ya kufanya maamuzi mazito juu ya UHAI WETU na uhai wa Taifa letu.
Kila mtu aongozwe na utashi wa moyo wake na si utashi wa fulana, mabando wala ngonjera...ukisikiliza sauti ya ndani kabisa, kwa uaminifu kabisa na huku ukijaribu kufikiri kuwa utakaloamua ndilo kusudi la MUNGU, ukifikia hatua ya tafakuri ya namna hii, hakika utagundua kwa urahisi kabisa ni nani hasa anafaa kupewa kura yako, kwa uraisi, ubunge na udiwani.
Mungu Ibariki Tanzania
Uchaguzi mwema wapendwa
Robert LENGEJU
Morogoro,Tanzan ia
Wakari Dr.Slaa (mtumishi wa Mungu na mtumishi mwaminifu wa watu)anaainisha hoja za ufisadi,kutokuw ajibika na ukosefu waa maadili kama visababisho vikubwa vya kudumaa kwa Tanzania yetu kiuchumi,kisias a na kijamii.Na huki akitoa mapendekezo ya kitafiti yenye kutoa maono juu ya suluhisho la matatizo tetu,watu (wenye akili za ndiyo mzee)wanajibu hoja kwa kumtuhumu kwa kuacha upadre na kuingia kwenye siasa.
Kimsingi,kwa mujibu wa dhana na falsafa ya Mabadiliko,kila mwenye akili timamu anajua nchi hii inahitaji mapinduzi(a complete change).Maono ya Dr.Slaa ni mabadiliko ya nchi yetu kimfumo,kifikya ,kimkakati na kiutashi,hasa utashi wa kisiasa.
Ndani ya miaka karibia 40 CCM imeonyesha kujaribu na kushindwa kusomamia mabadiliko hayo.Nimesema imejaribu mana nafahamu kimkakati kuna wakati Tanzania ilijengewa misingi ya ukuaji hasa na waasisi wake,wakiongozw a na Mwenye heri Mwl.Nyerere.Misingi hii hata hivyo imeshabomoka kwa namna isiyoweza kutazamika.
Jakaya kikwete (nafahamu hapendi kuitwa Doctor,mnampaka zia tu) alijitokea kam nuru ya asuuhi yenye matumaini chanya, Mtanzania nikasema"I think we gat somebody". Akakukuruka pale mwanzo kwa ari kasi na nguvu mpya ndani ya kiriba cha zamani.Ghafla dhahabu kikwete ikapimwa na moyo wa "List of shame" kutahamaki chali mtoto wa Bagamoyo.
Alihitajika kiongozi anayetoka kwenye mfumo tofauti kupambana na ufisadi na kuushinda.Mana ni kweli Kikwete amepambambana na ufisadi kama aimbavyo makamba kila kukicha,lakini amepambana na kushindwa vibaya.
Tunahitaji kiongozi mwenye "moral. Authority" na si kutisha kwa nguvu za kimtandao wala kidola.Maana yake ni rahisi, huwezi kupambana na ufisadi kama nawe unanukia ufisadi.
Miaka 15 ya ubunge wa Daktari Slaa,halmashaur i ya Karatu imekuwa ikipata hasi safi kwa mipango,mikakat i na matumizi bora na yenye kuthamini pesa za maskini wa Tanzania.kama kiongozi, Dr ana "authority" ya kunyooshea vidole waliofuja pesa za umma. Je kikwete anaweza kukemee matumizi mabaya ya pesa za umma huku mawaziri wake wakitembea na zahanati nne za kisasa kwenye nyumba za starehe?(Kwa mahesabu ya Dr Slaa, kila shangingi moja linathamani sawa na zahanati nne za sh. Milioni 50 kila moja) .
Ni mengi ya kuandika lakini lamaana hapa ni nchi yetu. Si kikwete, si slaa, wala vyama vya siasa na propaganda zao.Ni mihimu watu tuamue sasa kama tunayahitaji maisha bora ama la.
Mfumo wa Dunia ya sasa unalazimisha siasa kutegemeza nyanja zingine katika maisha ya mwanadamu hasa wa nchi zinazoendelea(p olitical determinism).Hatahivyo, ni mihimu sasa, wasomi wetu wakasaidia kuelimisha na kupevusha fikra za wananchi wote,tuwe na ufahanu wa msingi wa masuala ya msingi hasa yahusuyo uongozi wa kisiasa wa nchi yetu, na baadaye kuoanisha kiurari unaofaa na nyanja zingine muhimu kama uchumi na sekta ya kijamii,kwa namna ya kuwezesha mfumo wa kila sekta kutekeleza wajibu wake na huku zikisaidiana na kutegemeana katika kuwaleta watanzania Maisha Bora na sio ahadi za Bora Maisha.
Mungu Ibariki Tanzania
Uchaguzi mwema wapendwa.
" Dr SLAA, yes we can, huyu ni mtanzania wa pili kwa nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo, ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo, ni Dr. Slaa aliesimama mnazi mmoja kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi, ni Dr. Slaa aliesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuelekeza zaidi kwa watanzania, ni Dr.Slaa amesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma, ni Dr.Slaa amekuwa mtanzania baada ya nyerere kutoa hoja zinazomlenga mtanzania maskini, ni Dr.Slaa anaeweza kuthibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma, ni Dr.Slaa anaeweza kuwapa elimu bure watoto wetu pale mlimani achana na longolongo za sisiemu kuwatoza ushuru watoto waulizeni majukwaani wao nyerere aliwatoza ada? kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini? ni Dr. Slaa anaeongelea treni ya umeme kwenda kigoma,dodoma,t abora, mwanza, waulize mpango wao sisiem kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa mababu wetu waliyotumia wakati wa ukoloni hawa hawatutakii mema, hawa hawana tofauti na akina kalupeters, ni Dr.Slaa anaeongelea mfumko wa bei -nani hajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. kwani kuna tofauti gani tanzania na kenya, ethiopia, ambako ni chini ya 20 ya pesa yao? kwanini sisi tuna kasoro gani kuwa maskini kiasi kwamba mtu asafiri kutoka ethiopia kuja dar es salaam afike kabla ya mtu anatoka kariakoo kwenda mwenge? ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matilion ya pesa kutoka migodi yetu ya buzwagi, geita, bulyankulu, tulawaka,nzega, tanzanite hawa wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa wameruhusu wizi huo, ni Dr.Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shinilingi 350 achana na sisiemu inayoshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokizi mahitaji, ni Dr.Slaa anaeweza kusimamia mashirika ya jamii kuleta tija achana na sisiemu wanafyonza michango yetu kule kwani haya mashirkia yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? mbona kwingine yameweza? ni Dr.Slaa anweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu, bila kulipiza visasi, ni Dr,Slaa ambae amepanga kubadili katiba ili Rais afuite matakwa ya waliemwajiri ambao ni wananchi, waulize sisiemu hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe ela? hivi inaingia akilini kweli? hata kama mtu anasemwa ni fisadi hakuna hatua yoyote -naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu -katika hotoba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandkwa kidogo tu gazetini kwamba amekutwa na [NENO BAYA] yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine, sisiemu hawawezi hayo? eti wanataka ushahidi nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielezlezo? tunaiona rushwa kwa matokeo yake -barabara bilion 200 siku mbili imeharibika kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? hawawezi sisiemu eti wantaka vielelezo -ni Dr.Slaa anaeweza kfanya hayo si tumeona mnazi mmoja aliwataja wote! hapo ni mbunge je akiwa rais watakimbia nchi nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupue muone moto utakavyowaka? tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati-jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be seriuos stupid??????? hivi kweli leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda mwanza, shinyanaga, tabora, kigoma, mbeya,lindi, mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori???????? fikiaria ni wewe umevuliwa nguop mbele ya mama mkwe wako>??? harafu unaipiagia kula sisiemiu???? nani asie jua madakitari wetu wengi bingwa wapo botswana/ HAPA watu wanakufa tuu, nani asiejua matatizo ya umeme, maji, makzai, maradhi, yanavyotutesa? nani asiejua wakulima wetu waivyokuwa na masoko ya mazao yao, nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga, nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuxchuua kila kitu?? jamani wafanyakzi, wakulima, wanafunzi ni jukumu letu kupeleka habari hata kama vyombo vyetu vya habari ni vya hao hao, hawasemi ukweli hata wao ni maskini na wanakubali kupitia vyombo vyao tuendeee kusema piga na shavu la kushoto, ni Dr. Slaaa dr wa ukweli sio dr wa misifa anaweza kutuvusha tulipo, nchi hii ni maskini wa kujitakia, Tanznia ni tajiri tuna kila kitu mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila kitu? naonea huruma wenzangu waliokunywa maji ya bendari hivi kun mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? hivi kuna mabae hajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja,? wamekosa nini hawa? jamani tuache woga inawezekana mbona kenya wameweza? mbona malawi wameweza?mbona zimbabwe wameweza?mbona ghana wameweza? mbona tunwea kufnya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumia, tunamtuma Dr.Slaa kuwakurupusha kuweka katiba sawa huo ndio msingi wa yote, ni Dr. Slaa asiopgopa mgo,mbea binafsi hawa sisiemeu wanaogopa hwawezi kabisaaaaaaaaaa a, jamani 2010 hakuna kudanganyika, enough is enough achani kudanganyika, nawatamani watu wa kule mara -hakuna kura inaibiwa zote zinasimamiwa, tukibadilika inawezekana tena ni rahisi, peleke ujumbe huu kwa babu na bibi kule kijiji kwa simu kama ipo, au posta, au gari ili mradi wale jamaa waliochoka kuishi wasi ikwapue barua wakidhani ni ela mara daabda ya kuwavua nguo abiria, hii inatia aibu miaka 49 ya uhuru? karne ya 21 shida zote hizi inakera inaudhi na haivumiliki hawa sio wenzetu baba mbunge mjomba katibu wa wizara, biinamu waziri mkuu, wao wao wao na wanataka watiu wasisome ili wasiwe kuhoji wasome wao tuuuuuuuuuuuuuu uuu, wengine 40% ya ada kima cha chini laki 2, utalipaje hiyo 40% tunaonewa tunadhulumiwa, hawtundei haki -yaani wamefika sehemu wansema vijisenti ntamani yule mgaya angepata hivyo vijisent pengine asingejitoa mhanga inauma, hao hao wameandikwaaaaa aaaaaaaaaaaaaaa aaaaaaaaaaaaaaa aaaaaaa lakini bado wanangangania hawakumbuki maneno ya mwalimu kuhusu wazir wa uengereza, mkubwa nae amewachia tuuuuuuuuuuuuuu uuu si washikaji acha tule good tym jamani tunaumia pisheni wanaoweza waongoze? jamani ifike sehemu ubinadamu uwepo, tupige kura na ninwashauri tongotongotongo zetu zitatuumiza haya Dr.Slaa huyoooooooooooo ooooooooooooooo ooooooooooooooo ooo mpeni shoka amalize misitu tuanze upyaaaaaaaaaaaa aaa aaaaaaaaaaaaaaa aaaaaaaaaaaaaaa aaaaaa bila hakuna kitu,
Mtanzania mwenye haki ya kikatiba kutoa mawzo yake bila woga tuangane jamani sisi wote ni wana sisiemu lakini maji yamevuka shingo hapa hamna kitu kura tunampa Slaaa lakini tunabaki kuwa sisiemu cha msingi maendeleo bwana kuna ndani hamna kitu
JAMANI GUEST HOUSE ZIKO WAPI? HUYU MISS CHACHALA ANAHITAJI MWANAMME WA SHUGHULI ILI KUMZINDUA MAANA KALEWA NA CHUKI BINAFSI! TUNACHOTAZAMA HAPA NI JINSI YA KUMPATA MTANZANIA MZALENDO WA KWELI, ATAKAYETUONYESH A DIRA YA MAENDELEO YA KWELI YA KIUCHUMI. SASA KAMA AKILI YAKO IMEDUMAA KIASI KWAMBA HUNA HOJA ZA KUCHANGIA, UTUJULISHE MAPEMA ILI TUKUTAFUTIE MWANAMME WA KUKUZINDUA ILI UAMKE KUTOKA USINGIZINI, KULIKO KUTULETEA UTUMBO NA UFUKUNYUKU HAPA!
THE WHOLE OPPOSITION HAVE FAILED US FOR NOT PREPARING US KISAWASAWA.
I COMMEND CCM FOR THE GOOD MATAYARISHO THAT THEY HAVE DONE SO FAR.
who did know that Dr. SILAHA would contest the presidency?let him try next time!BTW iam not for CCM,i dont see any good strategy tht will see us sail through!!!