
| Masha ang'oa vitasa ofisi ya Mbunge Mwanza | Send to a friend |
| Tuesday, 30 November 2010 01:46 |
Frederick Katulanda, MwanzaALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa. Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe. “Nimefuatilia kwa DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) nikaambiwa amechukua Masha, nikafuatilia kwa Katibu Tawala wa Mkoa yeye alijibu kuwa naye alifuatilia suala hilo kupitia kwa Das na kupewaa majibu kama yangu, sasa sijajua ni kwa nini, ninavyojua ofisi haipaswi kukosa samani kwa vile kuna fedha za kununulia vitu hivyo,” alisema. Kwa Upande wake, Masha alikiri kuondoka na vitu hivyo na kwamba, asingeweza kuacha vifaa vyake binafsi katika ofisi hiyo. Masha alisema vifaa alivyoondoka navyo ni vile tu ambavyo ni mali yake. “Wakati naingia hapa nilikuta ofisi ikiwa na kiti kimoja na meza tu, vifaa vingine niliweka vyangu, kama kompyuta na meza zake, simu na samani nyingine kulingana na mahitaji yangu,” alisema Masha. Alisema Wenje anapaswa kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya, ili kupewa vifaa vya ofisi hiyo ambavyo yeye aliviondoa alikuwa havitumii kwa vile wao wanajua vilipo. “Jamani vifaa vya ofisi anapaswa kuuliza ofisi ya mkuu wa wilaya, sasa kama anataka nimwachia na vyangu binafsi, mie nimetoa vyangu…hivyo vya ofisi vipo, nadhani amefika na kukutana na kiti kimoja na meza vile vingine vilivyokuwemo pia vilikuwa mali ya ofisi,” alieleza Masha. Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza (RAS), Doroth Mwanyika, hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa nje ya ofisi, lakini ofisa mmoja wa ofisi yake alithibitisha kuwepo kwa malalamiko ya Wenje na kwamba, yalikuwa yakishughulikiwa. |
| Last Updated on Thursday, 07 April 2011 11:31 |



Frederick Katulanda, Mwanza











Comments
Nafikiri unahitaji uangalizi wa karibu huenda kukosa ubunge kumekuathiri kisaikolojia.
Nakuomba chonde chonde JK, hata kama unampenda vipi Masha, ukimchagua hata ukuu wa wilaya Wananchi hatutakuelewa hata kidogo. Kati ya watendaji waliokusababish ia upate kura chache na Masha yumo.
Hii aibu aliyoitafuta mwenyewe kamwe haitofutika maishani mwake.
Amuulize mzee Malecela kwanini mpaka leo Watanzania wanaangalia kila anachokifanya na kukitenda. Pamoja na kuomba radhi, dhambi ya maneno yake ya dharau bado inamtafuna mpaka leo.
Hebu tueleze Masha,umekaa bungeni miaka mitano. Posho ya jimbo kama sikosei ni Tshs 500,000 x 12months x 5years = Tshs 30,000,000/=
Hizo pesa zote umefanyia kitu gani mpaka leo unang'oa mpaka vitasa? Tutakukumbuka kwa lipi wananchi wa jimbo la Nyamagana?
MASHA UMEJIHARIBIA NA HUFAI KABISA KWA UONGOZI HATA WA NYUMBA KUMI.
Katika mazingira ya kistaarabu, Masha alitakiwa kufanya makabidhiano ya ofisi katika mazingira ya wazi kabisa. Kuonyesha kilicho chake na mali za ofisi.
DAS alitakiwa kutunza inventory ya vifaa vya ofisi. Yeyote anayeingia na kutoka anatakiwa kuona na kujua kilichopo kwa uwazi kabisa.
Hivi Mhe.alipoambiwa kuwa na mwl.kuwa subiri, je kama angekuwa na hurka ya kukosa subira si angejikuta amehama chama ama kuwa na mgogoro na viongozi wenzake serikalini? Mbona alitulia na mwisho wake si amekuwa rais wa nchi yetu?
Subira na uvumilivu ni mihimili mikubwa ktk maisha ya binadamu yeyote.
Mungu ibariki Tanzania; amina