MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Si shwari.ARUSHA VURUGU, RISASI, MABOMU  Send to a friend
Wednesday, 05 January 2011 21:08

Mussa Juma, Arusha
POLISI mkoani Arusha, jana lilimwaga damu za watu kadhaa, walioshiriki na wasioshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano ya Chadema, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Ispekta Jenerali Saidi Mwema.

IGP Mwema alitangaza kuyapiga marufuku maandamano ya Chadema akibainisha kwamba taarifa za kiintelijensia zimebaini kwamba kungekuwa na vurugu wakati wa kufanyika kwake.

"Maandamano hayo ni marufuku, lakini wanaruhusiwa kufanya mkutano wao wa hadhara. Kuna taarifa za kiintelijensia kwamba kunaweza kutokea fujo na uvunjifu wa amani,” alisema IGP Mwema alipozungumza na waandishi wa habari juzi jioni.

Awali Chadema iliruhusiwa kufanya maandamano hayo yaliyoandaliwa kushinikiza taratibu zifuatwe katika uchaguzi wa wenyeviti au mameya wa halmashauri nchini.

Maandamano hayo pia yalilenga kuwahamasisha wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kushiriki kutoa maoni yao bila woga juu ya kuandikwa upya katiba ya nchi, pindi kamati itakapoanza kazi.

Maandamano hayo yalipangwa kuwashirikisha wabunge wote wa Chadema, na yalipangwa kuanza jana saa 4:00 asubuhi na kuishia kwenye viwanja vya NMB mjini Arusha ambako mkutano wa hadhara ungefanyika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengeye juzi aliruhusu maandamano hayo lakini akasisitiza kwamba jeshi lake litatoa ulinzi ili kuhakikisha yanakuwa ya amani.

"Tumekubali maandamano na mkutano wa Chadema lakini tunaomba wafuate taratibu na wahakikishe  hakuna uvunjifu wa amani ambao unaweza kutokea," alisema Andengenye.

Hata hivyo baadaye juzi jioni IGP Mwema, aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini  Dar es Salaam na kutangaza kuyafuta.

IGP Mwema aliwaeleza waandishi wa habari kuwa ameamua kufuta kibali cha maandamano hayo kutoka na kupata taarifa za kiintelijensia kwamba “kungetokea vurugu”.

Agizo hilo Jipya la IGP Mwema lilifanya viongozi wa chama hicho kilichojizolea umaarufu, hasa baada ya kuanzisha hoja ya Katiba, kukaidi na kusisitiza kuwa maandamano hayo yangefanya jana kama ilivyopangwa.

Na walipojaribu kufanya maandamano hayo polisi ilianza kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao uamuzi ambao ulifanya watu kadhaa wakiwamo wabunge wa Chadema kujeruhiwa vibaya.

Hadi jana jioni zaidi ya watu kumi, akiwepo mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbusi, walijeruhiwa kwa kipigo huku watu wengine watatu, wakiwa wako hoi baada ya kupigwa risasi za moto.

Wakati watu hao wakiumizwa kwa vipigo, mali kadhaa ikiwamo gari la mbunge  wa viti maalum mjini moshi, Grace Kiwelu viliharibiwa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pia alikumbwa na dhoruba pale alipojikuta akitumbukia kwenye mtaro wa maji machafu na polisi kumshabulia, wakati alipokuwa akishiriki maandamano pamoja na wabunge kadhaa wa Chadema.

Wakati hayo yakiendelea, shughuli zote katika mji wa Arusha zilisimamia huku barabara kadhaa nazo zikifungwa tangu asubuhi kutokana na vurugu za polisi na kamatakama ya watu iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi hilo.

Vurugu za polisi pia zilifika katika makazi ya watu na katika hospitali ya wilaya ya Arusha ya Kaloleni ambako, wagonjwa kadhaa walizimia kutokana na polisi kurusha mabomu ya machozi jirani na hospitali hiyo.

Daktari za zamu wa hospiali hiyo, Anna Kimaro alielezea kushangazwa na hatua ya polisi kurusha ovyo mabomu ya machozi jirani na hospitali.

Baadhi ya wagonjwa, Mwanaidi Mussa na Sabra Khalfani, walisema wamedhurika na hali hiyo kwani walipatwa na mshtuko.

“Mwanangu alipoteza fahamu kabisa hadi sasa hajisikii vizuri,” alisema Sabra alipozungumza na Mwananchi hosipitalini hapo, huku akiwa amebeba mtoto wake Abdul Yusuph, mwenye umri chini ya mwaka mmoja.

Katika vurugu hizo, pia baadhi ya waandishi wahabari walijeruhiwa kwa kupigwa na polisi akiwepo mwandishi wa gazeti hili, Moses Mashala,mpiga picha wa kituo cha televisheni cha Channel ten, Ashraf Bakari, mwandishi wa kujitegemea wa BBC, Moses Kilinga na wengine kadhaa.

Kamanda Andengenye hakupatikana jana kuelezea idadi kamili ya majeruhi kwani polisi, waliwazuia wanahabari kufika kituo kikuu cha polisi huku wakiwataka kuondoka eneo la kituo hicho katika muda dakika tano.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Friday, 07 January 2011 08:36
 

Comments 

 
+1 #107 2011-01-08 20:53
SUALI NI HV INGEKUWA VP NGUVU ILIYOTUMIKA KUZUIA MAANDAMANO INGETUMIKA KUYALINDA NA KUYAONGOZA JE UNAISI KUNGEKUWA NA DOSARI YOYOTE KWA MATUMIZI HAYO?
Quote
 
 
-1 #106 2011-01-07 08:19
Quoting HALIKUHUSU:
Quoting Mangi Lelo:
Nini Huyu Majungu Silaha mbona ana pupa la madaraka ebu subiri 2015 ujaribu bahati yako.Kama sasa ni hivi ukishika madaraka itakuaje...subiri usitumie nguvu,amani na usalama wa nchi bora kuliko yote :zzz

TAFAKARI KABLA YA KUONGEA WW HUJUI UNENACHO TATIZO LAKO UMEJAA USHABIKI BADALA YA KUTIZAMA UKWELI NA HAKI...UNAWEZA KUBAINISHA SLAA AU CHADEMA WAMEFANYA KIPI KIBAYA KILICHOPELEKEA HIZO VURUGU??!!!HIVI JAMANI WATANZANIA MTAZINDUKA LINII??!!! :sad:

WEWE Hapo, pamoja na kutafakari ukumbuke kuwa wanaokufa kwenye vita hasa za kiafrika ni wanyonge ndiyo hao ambao kupata dhamana kwao ni kazi kubwa. Just think, mimi naumia sana nikikumbuka vita ya kenya nimepoteza girl friend wangu akiwa mjamzito tayari ndoa tulikuwa kwenye matangazo ya wiki ya pili.Kule zenji mjomba hadi leo ana mguu mmoja.
Now see, how odinga and kibaki enjoy life, see in zanzibar how sefu enjoys kuku wa masaa yote. Chonde vijana limeni, someni, fanyeni biashara akiingia slaa, lipumba au kikwete ikulu hakukutoi wewe ulipo kama hujitahidi. Tusidanganyike, tugangalike.Maisha bara au bora maisha huanza na wewe binafsi, acheni uvivu fanyeni kazi kama singepore zamani.
Quote
 
 
+1 #105 2011-01-07 08:04
TUNAKUTAKA GBAGBO WA TANZANIA JIUZURU KWA KUSABABISHA MAUAJI ARUSHA
Quote
 
 
+2 #104 2011-01-07 07:52
wewe ant.ally taimu, mbona unaongea kama [NENO BAYA]. yaani unafurahi watu kuuwawa ili ccm ikae madarakani, kweli wewe na kasauti kako haka inaonyesha unasuguliwa.
kama huna cha kusema tuache midume ya mbegu tuungurume, we kaa kimya mrembo.
Quote
 
 
-34 #103 2011-01-06 17:51
jamani watanzania mko wapi? mnapelekeshwa na watu wenye kupenda madaraka? slaa ni mgonjwa hafai hata kidogo kufuatwa, amkeni na acheni kupelekwa kama [NENO BAYA], tumbeni mungu na tusiwasikilize wabaya hawa.
Quote
 
 
-12 #102 2011-01-06 17:38
Quoting Mangi Lelo:
Nini Huyu Majungu Silaha mbona ana pupa la madaraka ebu subiri 2015 ujaribu bahati yako.Kama sasa ni hivi ukishika madaraka itakuaje...subiri usitumie nguvu,amani na usalama wa nchi bora kuliko yote :zzz

TAFAKARI KABLA YA KUONGEA WW HUJUI UNENACHO TATIZO LAKO UMEJAA USHABIKI BADALA YA KUTIZAMA UKWELI NA HAKI...UNAWEZA KUBAINISHA SLAA AU CHADEMA WAMEFANYA KIPI KIBAYA KILICHOPELEKEA HIZO VURUGU??!!!HIVI JAMANI WATANZANIA MTAZINDUKA LINII??!!! :sad:
Quote
 
 
+17 #101 2011-01-06 17:34
kiukweli nashindwa kupata njia nzuli ya kueleza hisia zangu,ninachowe za kusema ni kwamba kilichotendeka Arusha jana kina onjesha ni kwa namna gani selikari inayoongozwa na chama cha mapinduzi ilivyo ya kikteta,lakini selikari ni lazima itambue kuwa CHADEMA inaungwa mkono na watanzania zaidi ya milioni tatu.
Quote
 
 
+5 #100 2011-01-06 17:22
Hivi Zitto Kabwe alikuwepo manake sijamuona wala sijasikia jina lake, au ndiyo ameshaamua kivyake kvyake,
Quote
 
 
+11 #99 2011-01-06 17:13
We SAID MWEMA ogopa kilio cha watanzania wanalia usiku na mchana. mpaka wengine wanakata tamaa ya kuishi kwa sababu ya maisha magumu. Leo hii unachukua vijana wako wawamalize iliufaidi hii dunia mwenyewe. Dhamira itakusuta tuuu kama upo mbele ya haki. Hii ni laanana ndugu yangu. Hii damu itakurudia si mchezo.
Quote
 
 
+10 #98 2011-01-06 17:09
Jeshi la polisi hakika linafanya kazi kwa kutegemea uongozi husika ndio maana tunaona umuhimu wa katiba mpya maana ndio utakuwa ukombozi wa Watanzania kwa ujumla.Tatizo viongozi wetu kwa mashairi a.k.a kauli wako vizuri mno kuliko utendaji wao kwanza full kulindana na katika serikali hii ni wachache sana wako kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na bila haya nawataja 1.Dr Mwakyembe 2.Magufuli.N awapa pongezi waliobaki wengi chenga tu
Quote
 
 
+10 #97 2011-01-06 16:58
inasikitisha sana na ni aibu kwa jeshi la polisi,kitendo cha kupiga mabomu mpaka ma ospitalini.si kizuri inaonesha ni jinsi gani polisi hawajui kazi zao.hii ni aibu kwa IGP na kwa raisi.namna hii hakuna amani kwa wa tz.
Quote
 
 
+6 #96 2011-01-06 16:32
MUNGU,warehemu waliokufa katika harakati za kupigania haki wape ujasiri walio baki,ili wasivunjike moyo...tanzania tunaitaji ukombozi wa kweli.CHADEMA IMEJITOLEA kuikomboa nchii hii.hakuna hamani bila vita
Quote
 
 
+9 #95 2011-01-06 16:26
Hay Serikali imepata mpira wa soksi ikauvalia mjumu! Wameshindwa kudhibiti mfumuko wa bei, umaskini na hali mbaya ya wananchi wanadhibiti maandamano. Wanataka tusahau hali ngumu ya maisha tubaki kujadili maandamano. Jamani njaa ni kali kuliko FFU!
Quote
 
 
+14 #94 2011-01-06 16:07
Polisi ndio waanzilishi wa vurugu zilizofanyika Arusha na kugharimu maisha ya watu watatu na majeruhi wengi.Ebu fikiria RPC anatoa kibali kwa ajili ya maandamano kwa CHADEMA kwa maandishi anakuja IGP from DSM anaongea na waandishi wa habari kutoa maamuzi yake kwao no writings! CHADEMA wafuate lipi lililoko kwenya Maandishi au lililozungumzwa tu na IGP? na huyu IGP iweje ameanzia wapi kupata hizi habari? au RPC wa Arusha alikuwa akimdanganya bosi wake kuwa kutakuwa na ulinzi mkali endapo vurugu zitatokea? Polisi inataka kuwafanya Watz kuwa ni mbumbumbu kiasi gani? Au inteligensia gani inatumika na RPC na ipi anatumia IGP? au moja anatumia new verision? It seems IGP alipokea instruction kutoka kwa Makamba kuwa afanye linalowezekana hayo maandamano yagonge mwamba?. Anyway CCM and its goverment is giving free credibilty to CHADEMA! suala la CHADEMA Arusha lingeachiwa OCD wa Ars lakini kwakuwa CHADEMA ni tishio IGP lazima atoe tamko.. Bravo CHADEMA tuko pamoja......
Quote
 
 
+7 #93 2011-01-06 16:02
Tatizo haki aitendeki kwani uomkutano unge fanyika vurugu ingetokeawapi inspector said mwema haruhusu mahandamano
achiaisia zawatu unapowanjima furusa ya kuwaona wabunge
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner