MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Wasichana wang’ara kidato cha nne  Send to a friend
Thursday, 27 January 2011 08:40

Fidelis Butahe na Hussein Issa
 BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Oktoba, 2010 yanayoonyesha kuwa wasichana wanaongoza kwa kiwango cha ufaulu. 

Hata hivyo matokeo hayo yameonyesha kuwa kiwango cha ufaulu katika mtihani huo kimeshuka kwa asilimia 22 ilinganishwa na matokeo ya mwaka 2009.  Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, aliwaambia waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo hayo jana, kuwa wasichana wamefanya vizuri zaidi kuliko wavulana. 

"Kati ya watahiniwa kumi bora, sita ni wasichana na wanne ni wavulana," alisema Dk Ndalichako na kumtaja kinara wa matokeo hayo kuwa ni Lucylight Mallya kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Marian iliyopo mkoani Pwani.  Hii ni mara ya pili kwa shule hiyo kutoa mwanafunzi bora katika mtihani wa kidato cha nne baada ya Immaculate Mosha aliyeibuka kinara katika matokeo ya mwaka 2009.  Kwa mujibu wa matokeo ya mtihani wa mwaka jana, kati ya shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 40, saba ni shule za seminari na huku Shule ya Seminari ya Uru inaongoza shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.


Matokeo hayo yanaonyesha kuwa shule kumi za mwisho ni mchanganyiko wa shule za serikali na watu binafsi.  Dk Ndalichako alitaja shule kumi bora zenye watahiniwa zaidi ya 40 na mikoa zinakopatikana kwenye mabano kuwa ni Uru Seminari (Kilimanjaro), Marian Girls (Pwani), St Francis Girls (Mbeya), Canossa (Dar es Salaam), Msolwa (Morogoro), Feza Boys (Dar es Salaam), St Mary Goreti (Kilimanjaro), Abbey (Mtwara), St Joseph Semiterambogo (Kigoma) na Barbro-Johansson (Dar es Salaam). 

Alieleza kuwa shule kumi bora zenye watahiniwa chini  ya 40 ni seminari ya Don Bosco (Iringa), Feza Girls (Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Queens of Apostles Ushirombo (Shinyanga), Sengerema Seminari (Mwanza), Sanu Seminari (Manyara), Bethelsabs Girls (Iringa), St Joseph-Kilocha Seminary (Iringa), Dungunyi Seminary (Singida) na Mafinga Seminary (Iringa).  Kwa mujibu wa Dk Ndalichako, shule kumi za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40 ni, Sanje (Morogoro), Daluni (Tanga), Kinangali (Singida), Mtanga na Pande (Lindi), Imalampaka (Tabora), Chongoleani (Tanga), Mwamanenge (Shinyanga), Mipingo (Lindi) na Kaoze (Rukwa).  Alitaja shule zingine kumi za mwisho katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 40 kuwa ni Changaa (Dodoma), Pande Darajani (Tanga), Igawa (Morogoro), Makata (Lindi), Kolo, Kikore na Hurui (Dodoma), Mbuyuni (Mtwara), Thawi (Dodoma) na Naputa (Mtwara).  Dk Ndalichako pia aliwataja watahiniwa kumi bora kitaifa na shule zao kwenye mabano kuwa ni Lucylight Mallya (St Marian), Maria-Dorin Shayo (St Marian), Sherryen Mutoka (Barbro-Johansson), Diana Matabwa (St Francis Girls) na Neema Kafwimi (St Francis Girls).   Wengine ni, Beatrice Issara (St Mary Goreti), Johnston Dedani (Ilboru), Samwel Emmanuel (Moshi Technical), Bertha Sanga (Marian Girls) na Bernadetha Kalluvya (St Francis Girls). 

Dk Ndalichako alisema kuna wanafunzi 42 kutoka baadhi ya shule walifanya mtihani wakati walikwisha ondolewa  katika usajili baada ya kubainika kuwa sifa za kidato cha pili walizowasilisha hazikuwa sahihi.  Alizitaja shule hizo na idadi ya wanafunzi kwenye mabano kuwa ni Ujenzi (4), Kahama Muslim (1) St John Seminari (1), Eckernforde (1), Seuta (1), Jamhuri (1) Mdanya New Vision (12) na Mseru (21).  Dk Ndalichako alifahamisha kuwa watahiniwa 56 wa kujitegemea waliondolewa kwenye usajili kwa kutokuwa na sifa lakini walifanya mtihani huo.  Alivitaja vituo walivyofanyia mtihani watahiniwa hao na idadi yao katika mabano kuwa ni Mwigo (29) na Twitange (27).  Dk Ndalichako alisema mtihani huo ulifanywa na watahiniwa 177,021 na asilimia 50.40 ya watahiniwa wote, wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 69,996 sawa na asilimia 43.47 na wavulana ni 107,025 sawa na asilimia 56.28.  “Mwaka 2009 watahiniwa waliofaulu walikuwa sawa na asilimia 72.51 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo,” alisema Ndalichako

Alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa 40,388 sawa na asilimia 11.50, wamefaulu katika madaraja I hadi III.  “Wasichana waliofaulu katika madaraja I hadi III ni 12,583 sawa na asilimia 7.81 na wavulana ni 27,805 sawa na asilimia 14.62,”alisema Dk Ndalichako.  Alisema idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani huo ni 46, 064 sawa na asilimia 52.09 ya waliofanya mtihani. 

Alisema katika kundi hilo, wasichana waliofaulu ni 22,405 sawa na asilimia 48.41 na wavulana ni 23,659 sawa na asilimia 56.13. Mwaka 2009 watahiniwa wa kujitegemea 49,477 sawa na asilimia 54.12 walifaulu, alisema.  Aliongeza kuwa watahiniwa 458,114 wakiwamo  wasichana 216,084 sawa na asilimia 47.17 na wavulana 242,030 sawa na asilimia 52.83 ndio waliojisajili kufanya mtihani huo mwaka jana.  “Mwaka 2009 watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 351,152, hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa watahiniwa 106,962 sawa na asilimia 30.5,” alisema Dk Ndalichako na kuongeza:  

  “Waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 ni 441,426 sawa na asilimia 96.36 na watahiniwa 16,688 ambao ni sawa na asilimia 3.64 ya watahiniwa wote waliosajiliwa, hawakufanya mtihani.  “Kuna ongezeko la watahiniwa wa shule 109,329 ambao ni sawa na asilimia 43.0 ikilinganishwa na idadi ya waliosajiliwa mwaka 2009. Watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 352,840 sawa na asilimia 97.04, watahiniwa 10,749 sawa na asilimia 2.96 hawakufanya mtihani,” alisema Dk Ndalichako. 

Alifahamisha  kuwa mwaka 2009 watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa 96,892 na 2010 kulikuwa na watahiniwa 94,525 ikimaanisha kulikuwa na upungufu wa watahiniwa 2,367 sawa na asilimia 2.44 ikilinganishwa mwaka 2009.  “Watahiniwa 88,586 wakiwemo wasichana 46,358 na wavulana 42,228 walifanya mtihani huo, watahiniwa wa kujitegemea 5,939 sawa na asilimia 6.28 hawakufanya mtihani.

Shule zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilikuwa 3,194 na zenye watahiniwa chini ya 40 zilikuwa 489.  Akizungumzia matokeo ya mtihani wa maarifa (QT), alisema watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 26,540  kati yao wasichana ni 16,101 na wavulana 10,439.  Alisema mwaka 2009 jumla ya watahiniwa 25,040 walisajiliwa kufanya mtihani huo kukiwa na ongezeko la watahiniwa 1,500,  sawa na asilimia 5.99 ikilinganishwa na mwaka 2009 na kwamba jumla ya watahiniwa 23,585, sawa na asilimia 88.87 ya waliosajiliwa walifanya mtihani huo.  Alisema katika mtihani wa maarifa (QT) jumla ya watahiniwa 8,295 sawa na asilimia 35.17 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu ikilinganishwa na asilimia 28.82 ya waliofaulu mwaka 2009.  Alisema kuwa kiwango cha ufaulu kwa mtihani wa maarifa kimeongezeka kwa asilimia 6.35 ikilinganishwa na wamaka 2009.

  “Jumla ya watahiniwa 311 wa mtihani wa kidato cha nne na watahiniwa 2 wa mtihani wa maarifa (QT) wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu cha 52 (b) cha kanuni za mtihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mtihani huo,” alisema Dk Ndalichako.     mwisho     


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Friday, 28 January 2011 08:34
 

Comments 

 
0 #21 2011-01-31 22:24
Sasa serikali imejipanga vipi kwa wale walifail ? Ndio wamesha fail au watawapatia mafunzo ya ufundi pengene theory hawaiwezi wapeni pratical skills.

Serikali na tasisi nyengine wapitie upya kwa nini wanafunzi amefail mtu anapata ziro haiwezikani ,,huu ni mpango maalum kabisa.

Pia hali inasikitisha wazanzbairi wamefail wengi kwa nini ? Au mumewafelisha ? Huu Ndio mpango maalum wa ccm wameupanga,ache ni siasa zenu kwa kuwafelisha watu wawe mandondocha ili muwadanganye kiurahisi.
Quote
 
 
0 #20 2011-01-28 15:44
Mbona Kichwa cha habari hakiendani na Maudhui ya habari???....
Quote
 
 
0 #19 2011-01-28 12:21
Nimesoma na kuridhishwa na michango mbalimbali iliyotolewa na waliotangulia. Lakini hakuna hata mmoja aliyegusia Baraza la Mitihani lenyewe. Kama mnavyojua kwa miaka kadhaa lilikuwa linalaumiwa kwa kashfa za kuvujisha mitihani. Jambo lilopelekea kuondolewa kwa wafanyakazi wake wengi. Mimi nahisi huenda nalo limechangia kwa kiasi kikubwa. Ama wametunga mitihani migumu kwa makusudi ili kuonyesha kuwa hakuna uchakachuaji tena. Katika hali ya kawaida haiwezekani hali ya kufaulu kushuka kwa ghafla hivyo, waalimu wengi, na vifaa vilivyotumika kwa wale wa 2009 ndio hivyo hivyo. Pia nahisi wizara husika nayo ina mkono katika kuvuruga mitaala, mtakumbuka kuna masomo yalifutwa halafu baadae yakarudishwa tena wakati waalimu wake walikwisha ondolewa na kupewa kazi nyingine za ki-hasibu na utawala. Hvyo tusiwalaumu waalimu wala wanafunzi lakini tulaumu serilaki kwa maana ya wizara ya elimu na baraza la mitihani.
Quote
 
 
+1 #18 2011-01-27 20:12
mbona kichwa cha habari hakiendani na taarifa zilizomo kwenye stori?
Quote
 
 
+2 #17 2011-01-27 18:39
+1 #9 Ajabu na kweli 2011-01-27 15:55
"Hivi mwanafunzi anapofeli na kuambiwa amepata sifuri nani alaumiwe? haiwezekani kiwango cha kufaulu (daraja la 1 hadi la 111)kikawa asilimia 11.5, hii inaonyesha mfumo mzima wa elimu umeoza na ni dhambi kubwa inafanyika sasa ya kuwa-label asilimia kubwa ya wanafunzi kuwa WAMEFELI. kumbuka kum-label mtu kuwa kafeli ni kilema maisha yake yote. Uko wapi usawa hapa? kwangu mimi division one ya Marian ni sawa na Division four ama zero ya mwanafunzi wa shule ya kata huko kijijini kwetu. kwani huyohuyo aliyepata zero akipelekwa seminary anapata division one. sijui ni vigezo gani wanaviweka vya kuangalia nani kafaulu zaidi na nani kafeli zaidi. sababu kwangu mimi aliyepata division three kutoka shule yenye mazingira magumu huyo ndo kafaulu zaidi kuliko aliyesoma Marian. Dhambi hiyo inaendelezwa na serikali hata kwenye mikopo, eti div 1 na 11 ndo wanapata mikopo. Jamani division three ya mtu aliyesoma shule yenye mazingira ya ufundishaji duni ni sawa na division 1 ya st Francis. Ni dhambi kubwa na wala haishii hapa -itatumaliza watanzania wote."
Quote

Maneno yako mazito. Tunaomba Mungu azidishe wenye akili kama wewe.
Quote
 
 
+2 #16 2011-01-27 17:31
Hapa kwa matokeo haya tunaelekea pabaya.
Mbona tunawadanganya wasichana kuwa wameongoza matokeo?kumbukeni waliongoza kama wanafunzi kumi bora na sio shule zao ndo zimeongoza!ukif uata asilimia utaona wasichana wamefaulu kwa kiwango cha 48.41% wakati wavulana ni 56.13%. Wasichana waliopata daraja I & III ni 7.81% wakati wavulana ni 14.62% haya ni kwa mujibu wa taarifa ya katibu wa wizara sasa huu uongo kuwa wanawake wameongoza matokeo umetoka wapi?wasichana bado kazeni buti kwenye matokeo hatupeani kama CCM walivyompa mwezenu uongozi kule mjengoni dodom
Quote
 
 
+1 #15 2011-01-27 17:21
Serikali na taasisi nyengine zisizo kuwa za serikali lazima mufanye uchunguzi kwa nini wame fail wengi sana vijana na hasa wanaume,na pia muakilishe kwa serikali izibe hilo pengo la ku fail ovyo wanafunzi,na hao walipass pia ifanyike uchunguzi inaonekana kuna magumashi yalipita hapo.
Quote
 
 
+5 #14 2011-01-27 17:12
Ni changamoto kwa BAKWATA kubun mbinu za kusomesha vijana wao ili kupunguza pengo la wasomi baina ya wakristo na waislamu ili mwisho wa siku wapate nguvu kazi ya kuendeleza dini ya kiislamu katika mtazamo mpya. Kelele peke yake na kutoa matamko ya malalamiko kwamba serikali haiwatendei haki haitawasaidia.
Quote
 
 
-2 #13 2011-01-27 17:08
cQuoting francis:
Enzi ya wanaume yafukia tamati
Nawapongeza sana wanafunzi wasichana kwa kuongoza katika matokeo ya kidato cha nne hata hivyo ujumbe ninaoupata unaashiria sasa enzi ya mwanaume kuwa kiongozi wa mwanamke inafikia tamati kwa kawaida mwanaume huwa mbele kwa kila jambo na mara nyingi huwa viongozi wa mwanamke lakini nadhani wanafunzi wa vulana wa kizazi hiki wamejisahau sana na wamesahau kwamba wao ni bride winner pia sababu nyingine nadhani uwekezaji kwenye shule za wasichana ni mkubwa zaidi wanashule nyingi na nzuri lakini hakuna shule nyingi za wavulana na ambazo ni nzuri nadhani wadau wa elimu tunapaswa kuliangalia hili.
Quote
 
 
-1 #12 2011-01-27 17:02
Enzi ya wanaume yafukia tamati
Nawapongeza sana wanafunzi wasichana kwa kuongeza katika matokeo ya kidato cha nne hata hivyo ujumbe ninaoupata unaashiria sasa enzi ya mwanaume kuwa kiongozi wa mwanamke inafikia tamati kwa kawaida mwanaume huwa mbele kwa kila jambo na mara nyingi huwa kiongozi wa mwanamke lakini nadhani wanafunzi wa vulana wa kizazi hiki wamejisahau sana na wamesahau kwamba wao ni dride winner pia sababu nyingine nadhani uwekezaji kwenye shule za wasichana ni mkubwa zaidi wanashule nyingi na nzuri lakini hakuna shule nyingi za wavulana na ambazo ni nzuri nadhani wadau wa elimu tunapaswa kuliangalia hili.
Quote
 
 
+1 #11 2011-01-27 16:09
Ningeshangaa kama Shule za serkali zingefanya vizuri wakati muda mrefu waalimu waliutumia kulumbana na mwajiri wao badala ya kufundisha. Hongera Mwanafunzi wa Ilborou kwa bidii yako ya ziada.
Quote
 
 
+1 #10 2011-01-27 15:56
Matokeo haya ni changamoto kwa Uongozi wa Shule husika ambazo hazikufanya vizuri.Kwa wale waliofanya vizuri, hongera sana. Ile dhana potofu kwamba wanawake hawawezi bado ipo? Maandalizi mazuri na udhubutu ni muhimu.
Quote
 
 
+1 #9 2011-01-27 15:55
Hivi mwanafunzi anapofeli na kuambiwa amepata sifuri nani alaumiwe? haiwezekani kiwango cha kufaulu (daraja la 1 hadi la 111)kikawa asilimia 11.5, hii inaonyesha mfumo mzima wa elimu umeoza na ni dhambi kubwa inafanyika sasa ya kuwa-label asilimia kubwa ya wanafunzi kuwa WAMEFELI. kumbuka kum-label mtu kuwa kafeli ni kilema maisha yake yote. Uko wapi usawa hapa? kwangu mimi division one ya Marian ni sawa na Division four ama zero ya mwanafunzi wa shule ya kata huko kijijini kwetu. kwani huyohuyo aliyepata zero akipelekwa seminary anapata division one. sijui ni vigezo gani wanaviweka vya kuangalia nani kafaulu zaidi na nani kafeli zaidi. sababu kwangu mimi aliyepata division three kutoka shule yenye mazingira magumu huyo ndo kafaulu zaidi kuliko aliyesoma Marian. Dhambi hiyo inaendelezwa na serikali hata kwenye mikopo, eti div 1 na 11 ndo wanapata mikopo. Jamani division three ya mtu aliyesoma shule yenye mazingira ya ufundishaji duni ni sawa na division 1 ya st Francis. Ni dhambi kubwa na wala haishii hapa -itatumaliza watanzania wote.
Quote
 
 
0 #8 2011-01-27 14:09
vijana wa mashuleni someni. kusoma si lelemama. serikali inajitahidi kwa kiasi chake kilichobaki ni kwa wanafunzi wenyewe kuongeza bidii.
Quote
 
 
0 #7 2011-01-27 13:58
HALI INATISHA SANA KWA NINI SHULE ZA SELIKARI ZINAENDELEA KUHARIBU KILA MWAKA,
SELIKARI INATAKIWA KUJIPANGA ILI SHULE HIZO ZIFANYE VIZURI, RUDISHENI MTIHANI WA KIDATO CHA PILI.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner