MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
Makombora  Send to a friend
Thursday, 17 February 2011 08:03

Na Waandishi Wetu
JIJI la Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo limetaharuki kufuatia milipiko mikubwa ya mabomu iliyotokea ghala la kutunzia silaha la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongolamboto, huku kukiwa na taarifa za watu kufa na zaidi ya 100 kujeruhiwa. Timu ya waandishi wa Mwananchi waliotembelea eneo la tukio usiku wa jana, walishuhudua nyumba kadhaa zikiteketea kwa moto baada ya kuangukiwa na mabomu.

Kadhalika waandishi hao wa Mwananchi walishuhudia nyumba moja ambayo ukuta wake ulibomoka baada ya kuangukiwa na bomu na ukuta huo kuangukia kundi la zaidi ya watu 12, watu watano wanadaiwa kufa.

Mmoja wa walionusurika kwenye tukio la kuangukiwa na ukuta, Juma Nganyanga, alisema kuna uwezekano ya maiti wengine kuwa chini ya ukuta huo.

Nganyanga alisema aliona kundi la watu wakiwa wamekimbilia kupumzika kwenye baraza la nyumba hiyo baada ya kukimbia nyumba zao, wakati wakiwa katika maombi ya kuomba Mungu awaepueshe na janga hilo, ghafla aliona vumbi likitimka kwenye nyumba hiyo.

Mwenye nyumba hiyo, Farida Magwa, ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi alisema akiwa barabarani na familia yake, aliambiwa kuwa nyumba yake imepigwa bomu na kuna watu wameuawa.

Magwa alisema baadaye waliweza kutoa maiti za watu watano, wakiwamo watoto wawili, lakini kuna uwezekano wa wengine bado wapo wamefunikwa na kifusi cha ukuta huo.

Katika tukio jingine, Mwananchi ilishuhudia maiti ya mwanamke ikiwa kwenye nyumba ambayo imeteketea baada ya kupigwa na bomu eneo la Mzambarauni na maiti nyingine ikipandishwa kwenye gari eneo la gereza la Ukonga.

Pia, Mwananchi lilishuhudia jengo la hosteli ya Kanisa Katoliki Ukonga likiwa linateketea kwa moto baada ya kuangukiwa na bomu, huku wakazi wa hosteli hiyo wakiwa wamekimbia.

Moto huo ambao ulikuwa ukiendelea kuwaka hapakuwapo na jitihada zozote za kuweza kuuzima, kwani watu wote walikuwa wamekimbia.

Mlinzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT) lililopo jirani na hosteli hiyo, alisema alishuhudia mabomu mawili yakitua eneo hilo, moja likitua kwenye nyumba ya hosteli hiyo na lingine pembeni karibu na gereza la Ukonga.

Milipuko hiyo ilianza majira ya saa 2.00 usiku na kuendelea mfululizo hadi saa 6.00 usiku, huku watu wakitaharuki na baadhi ya wanandungu na familia kupotezana.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq, alithibitisha kutokea kwa kifo cha mtu huyo ambaye hata hivyo jina lake lilikuwa halijafahamika.

Katika Hospitali ya Amana, Ofisa Mwandamizi wa Wagonjwa wa Nje, Mussa Wambura, alisema watu wawili walifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kwamba, hadi saa 7:00 usiku walikuwa wamepokea majeruhi 88, wengine hali zao zikiwa mbaya.

Waandishi wa Mwananchi walishuhudia magodoro yakiwa yametandikwa nje ambako wagonjwa walikuwa wamelazwa na wahudumu wa afya kutoka hospitali za TMJ na Hindu Mandal walipelekwa Amana kuongeza nguvu.

Pia, Sadiq alithibitisha kujeruhiwa kwa watu 43 na kwamba, serikali ya mkoa ilikuwa imetenga hospitali mbili za Ilala (Amana) na Temeke kwa ajili ya kupokea majeruhi na kuwatibu.

Awali, taarifa za zisizo rasmi zilizolifikia Mwananchi zilidai kuwa, mabomu yaliyolipuka ni ya masafa marefu.

Taarifa hizo zilithibitshwa na Sadiq ambaye aliwanukuu JWTZ wakisema, mabomu yaliyolipuka yanaweza kwenda umbali wa kilomita 11 kutoka eneo la tukio, Gongolamboto.

Alisema kwa mujibu wa taarifa hizo, wananchi walipaswa kuondoka eneo hilo na kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kwamba, wangekuwa salama baada ya kufika eneo la Tazara wakati kwa wale walioelekea Kisarawe alipaswa kwenda hadi eneo la Pugu Kajiungeni.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, alinukuliwa akiwataka wakazi wa Gongolamboto na maeneo ya jirani kuhama makazi yao kutokana na milipuko hiyo.

Kadhalika Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alinukuliwa akiwataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kuepusha athari zinazotokana na milipuko hiyo.

Wananchi wakimbia makazi
Habari zaidi zilisema mamia ya wananchi waliyakimbia makazi yao, wengi wakielekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam, lakini baadaye matangazo yaliyotolewa na vyombo vya usalama yaliwataka kwenda Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kupata hifadhi ya muda.

Kwa mujibu wa mashuhuda, watu walikuwa wakikimbia ovyo huku wakipanda magari yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji, kusalimisha maisha yao.

Baadhi ya wananchi waliolazimika kuyakimbia makazi yao, walikuwa wakipiga simu chumba cha habari wakilalamikia kupotezana na ndugu zao.

Mamia ya watu kutoka Gongolamboto, Karakata, Tabata, Segerea, Ukonga, Kitunda, Banana na maeneo mengine jirani, walionekana wakipanda daladala, wengine wakining'inia nyuma ya magari hayo yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji, huku mamia kwa mamia ya watu walikuwa wakitembea kwa miguu kuokoa maisha yao.

Kadhalika pikipiki, bajaj na magari ya kama pick-up pia yalitumika kuwahamisha watu kutoka eneo la tukio kwenda kutafuta sehemu ya hifadhi ya muda.

Uwanja wa ndege wafungwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, ulifungwa kwa muda na ndege zote hazikuruhusiwi kuruka wala kutua hadi hapo itakapoarifiwa baadaye.

Waandishi wa Mwananchi walishuhudia abiria wengi wa kigeni wakiwa kwenye uwanja wa huo wakisubiri kujua hatma ya safari zao, baada ya ndege walizokuwa wakizisubiri kuamriwa kutua viwanja vya Kia na Zanzibar hadi hapo watakapopewa maelekezo mengine.

Barabara ya Pugu katika njiapanda inayoingia kambi ya jeshi, ilifungwa na magari yote yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji na yale yaliyokuwa yakielekea Kisarawe yalizuiwa.

Mkazi mmoja wa Kigamboni aliyepiga simu ofisi za gazeti hili jana usiku wakati milipuko ya mabomu hayo ikiendelea, alisema wakazi wengi wa Kigamboni walikuwa nje ya nyumba zao, huku wakishuhudia makombora yaliruka juu kuelekea baharini hali ambayo iliwafanya wakazi hao kukumbwa na wasiwasi mkubwa.

"Hivi ninapokupigia wewe, makombora yanapita juu na kila mtu na familia yake wako nje kwa hofu...unasikia muungurumo huu kombora jingine linapita hapa juu kuelekea baharini," alisikika mwananchi huyo.

Kauli ya Dk Mwinyi
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Mwinyi, alisema milipuko hiyo ilitokea ghala namba tano na kwamba, kilichokuwa kikifanyika ni kuzuia usienee sehemu nyingine.

Dk Mwinyi alisema kambi ya Gongo la Mboto wanaishi wanajeshi na familia zao, lakini maghala ya mabomu yako mbali na kuongeza kuwa, kutokana na milipuko hiyo kuwa mikubwa hawezi kuzungumzia athari.

“Ile ni kambi ya jeshi, watu wanakaa mbali na maghala lakini kwa sababu tukio lenyewe ni kubwa sasa hivi hatuwezi kusema lolote,” alisema Dk Mwinyi.
Wakati mabomu hayo yakiendelea kulipuka mwananchi mmoja alipiga simu chumba cha habari cha Mwannchi, akisema Waziri Mwinyi yalipolipuka mabomu ya Mbagala, aliahidi kujiuzulu iwapo ingebainika kulifanyika uzembe.

Hata hivyo, Dk Mwinyi alipoulizwa usiku wa kuamkia leo kuhusu utekelezaji wa ahadi yake hiyo na majibu ya tume zinazoundwa, alisema kilichokuwa kinafanyika usiku ni kuokoa maisha ya watu, masuala mengine yatazungumzwa baadaye.

“Sasa hivi kuna jambo linaathiri watu, kwanza tuwaokoe halafu haya mengine tutazungumza,” alisema Dk Mwinyi.
Milipuko ya kwanza ilitokea barabarani mwaka 1972 wakati mabomu hayo yalipokuwa yanahamishwa kutoka Kambi ya Kunduchi kwenda Gongolamboto.

Kwenye kambi hiyo ni mara ya pili kutokea kwa milipuko ya mabomu, milipuko ya kwanza ilitokea mwaka 2008 na kusababisha maafa kwa wananchi wanaozunguka kambi hiyo, wanajeshi na familia zao.

Kila mwaka wataalam wa mabomu jeshini ambao hujulikana kama Ammo tech, wanaofanya kazi chini ya Chief Logistic and Equipment (CLE) hukagua mabomu ambayo muda wake umemalizika ili yaweze kupelekwa Kimbiji kuteketezwa.

Mbagala
Hali ilikuwa tete maeneo ya Mbagala na kusababisha watu wakiwa na watoto kukimbia ovyo, huku wengine wakijikusanya pembeni mwa barabara.
Wakazi wa Mbagala ambao walikumbwa na milipuko kama hiyo Aprili 2009, walionekana kuchukua tahadhari mapema baada kuanza kusikia milipuko kwa kuondoka ndani ya nyumba zao.

Mwananchi ilishuhudia wananchi hao wakiwa wamekusanyika pembeni mwa barabara ya Mbagala Rangi tatu-Mbande, hasa eneo la Muhimbili wanakopelekwa wagonjwa wa akili baada ya kupata nafuu, ambako kuna nafasi kubwa.
Maeneo ya Chamazi, Mbande, Charambe na Mbagala Rangi tatu, nyumba zilikuwa zikitikisika kutokana na milipuko hiyo, huku angani kukiwa kumetanda miale ya moto.

Mwandishi wa gazeti hili, Midraji Ibrahim, alisema kwenye nyumba yake iliyopo Chamazi, mikanda ya dari (ceiling board) ilidondoka kutokana na kishindo cha milipuko ya mabomu hayo.
Mlipuko wa 2008

Mwaka 2008 kulitokea mlipuko ghala la silaha kwenye kambi hiyo ya jeshi la Gongo la Mboto katika tukio ambalo vyombo vya usalama vilidai kuwa ulitokana na silaha hizo kupata joto kali.

Imeandaliwa na Julius Magodi, Neville Meena, Midraji Ibrahim na Andrew Msechu


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Friday, 18 February 2011 08:11
 

Comments 

 
0 #118 2011-12-12 16:26
похудела фото
советы малахова для похудения
без глютеновая и безказеиновая диета кулинария
торговый дом диет экс
помогает ли рыбий жир для похудения?
жиросжигатель купить
шоколад доя фигуры при диете для похудения
не получается худеть
стройная, челябинск, курчатова 19
предновогодняя диета от елены малышевой
какие упражнения надо делать чтобы похудели ноги
лечебный санаторий в зеленоградске или светлогорске очищение организма
клиника в донецке для больных сахарным диабетом
лиси мусса 50 шагов к похудению
правильное питание для сиамских кошек
диета для набирания
конструктор диеты без смс
как похудеть с помощю фотошопа
примерное меню диабетика
организация работы диетическая столовая на 100 мест
скачать бодифлекс плюс
гармоны от ожирение
отзывы об энержи диет
катогенная диета если есть эпилепсия
упражнения для ушей, талии
сайт е стояновой похудеть
можноли похудеть если завернуться салафановым пакетом
пизда худая
диета елены пряниковой
лечебное питание при диабете 2 го типа
медицинский центр здоровье женщины спб
сахарный диабет 2 типа инсулинопотребн ый
подросток и ожирение
похудение от аниты цой
диетический каталог сайтов site uz
классные часы в 10-11 классах здоровый образ жизни
как правильно питаться чтобы похудеть советы диетологов
калории попкорн
мажу на тело скипедар похудела
как быстро избавиться от вздутия живота?
Quote
 
 
0 #117 2011-02-18 12:26
kwakweli inabidi kufikiria kabla hamjasema mnayoyasema au kutenda mnayoyatenda..nahisi waziri waulinzi na kamati zake sio watendaji kwa yaliyotokea ila niwafikishaji wa majukum,,ukirej ea kwa yale ya mbagala, hivo basi tuache kulaum na kutukana hovyo kama watu tusiokua na akili tutumie hekima kwani taifa halijengwi na raisi na mawaziri ila ni sisi wananchi.pole kwa wote walioathirika.
Quote
 
 
+1 #116 2011-02-18 08:39
Oyaa mwenge,udsm,ari dhi University,Mlim ani city,Tcra ubungo plaza,ubungo tanesco,chuo cha maji. AZENI KUCHIMBA MAHANDAKI KABLA HAMJAUNDIWA KAMATI NA KUPEWA POLE LUGALO MILITARY BASE NDIO INAYOFUATA MSISEME SIKUWAAMBIA!!!! !!!!!!!!!
Quote
 
 
0 #115 2011-02-18 06:39
Sasa hili ni Janga, na hapa ni mahali pa kuonyesha umoja na mshikamano wa ki-Tanzania usio na unafiki.Tuwahudumie hao waliathirika na mabomu kwa kushirikiana na maelekezo yanayotolewa na viongozi wanaotuongoza. Tusisahau Tz, tunahitaji ulinzi wa Mungu; hayo yanayotokea ni dalili tu kuwa hatuko salama, hivyo tuondoe tofauti zetu zote, na tu-mwombe Mungu atuepushe na majanga na maafa, n ahao viongozi pia tuwaombee Mungu awape hekima na maarifa- ila na wao waache kuihujumu nchi kwa uroho wao wa madaraka na ufujaji wa mali; wajue ipo hukumu ya Mungu mbele yao.
Quote
 
 
-1 #114 2011-02-18 06:38
Poleni Watanzania kwa msiba huu mkubwa. Amkeni watanzania wekeni woga pembeni. Amua kwa nia moja. Kutatua tatizo hili moja kwa moja, ni KUMUONDOA KIKWETE haya mengine yatajishughulik ia yenyewe.
Unganeni sahau vyama vya siasa.
Quote
 
 
+1 #113 2011-02-18 06:08
kwa matukio haya inaelekea hatuna uwezo (capacity) ya kuhifadhi mabomu.
nafikiri njia mbadala ni kubinafsisha jeshi, au tuachane kabisa na biashara ya mabomu pindi vita ikizuka tutaviagiza kwa hao wenzetu wenye ujuzi wa kuzihudumia
Quote
 
 
0 #112 2011-02-18 03:30
mengi watu wamesema lakini lamuhimu jamani tumesoma kutoka misri kwani tanzania hatu wezi tutapigwa stoli mpakalini tuhamke sasa mbaraki kakimbia kwanini nasisi tusimkimbize kikwetwe halaaaaaaaaaaaa aaaaa
Quote
 
 
+1 #111 2011-02-18 03:27
WEWE WAZIRI JIUZULU UONESHE UWAJIBIKAJI TUMECHOKA NA we WA KAMATI KAMATI,HATUTAKI KAMATI,TUNAKUTA KA WEWE UJIUZULU!!!!!ki kwete madalaka matam lakini machungu tunaomba uwapishe wanao takakutu ongozea taifa letu kwani wewe tayali humedoloraaaaaa aaaaaaaaaaaaaaa tokaaaaaaaaaaaa aaa aaaa..........
Quote
 
 
0 #110 2011-02-18 02:13
Quoting Andrew Nyantory:
Naomba nitangulie kwa kusema ASHAKUM SI [NENO BAYA], wachangiaji wengi tanatanguliza hasira mbele kwani tuna uchungu na yaliyo tufika, napenda kuuliza kwani ripoti ya mbagala ilikua siri? kama haikua siri ni nani kati yetu aliyeifuatilia na kuichambua na kuhakikisha yaliyopendekezw a yanatekelezwa? serikali ni watu na sio mtu, kama tunataka kujua ni ni mkosaji tuisome sasa kwa kuwa tumechomwa mkuki mwingine na tujue ni nani aliyepewa dhamana ya kulinda usalama wetu na akazembea hii ndiyo civi duty

na wewe unajiona sehemu ya utawala,wewe ni mtawaliwa tena unanyonywa,masu ala ya kusema sijui serikali ni watu,ni misemo inayotumika tu lakini in reality haina uhalisia,kama huamini MBONA UKIJITOKEZA KUANDAMANA NA SURA YAKO MBAYA KAMA KIATU UNAPIGWA KAMA PAKA ALIYEIBA MBOGA YA MCHANA!!!!na bado unaamini eti wewe ni serikali! viongozi wanachaguliwa na wananchi kuwawakilisha,n a wanatakiwa wawajibike katika huo uwakilishi,wana poshindwa,walio wachagua wanaweza kuchukua hatua zozote wanazoona zinafaa kuwawajibisha,K UMBUKA KUNA WATAWALA NA WATAWALIWA,NA SIKU ZOTE WATAWALIWA NDIO HUONJA JOTO YA JIWE MAMBO YANAPOHARIBIKA, SASA BADO UTAENDELEA KUTETEA TU!!!!
Quote
 
 
0 #109 2011-02-18 01:06
mabomu tulopewa enzi za mwalimu hadi leo ya nini!!??
k'ninah zao wasiowajibika na kusababisha madhara yasokua ya lazima...kazi zao nikutaka trainings na safari za nje ya nchi,,,,pumbu zao!
Quote
 
 
0 #108 2011-02-18 01:04
[NENO BAYA]nina zao hao wanajeshi wasiofanya kazi zao kama inavyotakiwa!
Quote
 
 
0 #107 2011-02-17 23:24
Sorry was wrongly quote, I wanted to quote this one on message 89 from KACHIKEQuoting kachike:
Lawama zisizo na ushahidi hazitasaidia kuondokana na matatizo kama haya.Watu wengine kazi yenu ni kulaumu tu,toeni ushahidi na ushauri kwa hayo mnayoyasema.Vinginevyo tunawaona mbumbumbu tu msiojua kitu,Tukifuatil ia sehemu zenu za kazi ni uchafu na madudu matupu mnayofanya.
Quote
 
 
0 #106 2011-02-17 22:43
MH !!! MAMBO HAYA BWANA NI AJABU, KAMATI ZA BUNGE ZINAJADILI UMEME NA KUJICHANGANYA NA MA DOWANS MABOMU YANALIPUKA ONA SASA MAWAZO YOTE YANAHAMIA KWENYE MABOMU HUKU MISWADA INAPITA MH ! POLE KWA WAHANGA, SERIKALI NA WABUNGE KWA UJUMLA.
Quote
 
 
+2 #105 2011-02-17 22:12
Ninawapa pole watz wote waliopatwa na maafa haya.Mungu awafariji waliofiwa na ndugu zao.Niwakumbushe watanzania,kama vile haki za wengi zinavyokiukwa ndivyo na haki za wanajeshi zinavyokiukwa.Fikiri wanajeshi waliokufa kwa kujitoa mhanga kutetea nchi hii familia zao walizoziacha nyuma zinatunzwa? kama hawatunzwi,ni nani basi yuko tayari kuingia kwenye ghala la silaha kukagua kama huna uhakika wa maisha ya familia yako?Inawezekana hawakagui,na viongozi wao wako busy na siasa wanaacha kutetea maslahi ya wanaowaongoza wanatetea matumbo yao wenyewe.Nani anajua kama wanajeshi nao wana mgomo baridi kama waalimu ambao matokea ya mgomo wao unaoneshwa na matokeo ya mitihani.Naomba mamlaka husika ziangalie upya mafao ya wanajeshi.Polisi nanyi mko wapi? mbona jana hamkupeleka magari yenu ya maji ya kuwasha,mkayamw agie mabomu? Muda mwingi mnautumia kudhibiti raia wasio na hatia mnaacha majukumu yenu ya msingi,kila siku mnadai mnazuia uvunjifu wa amani mbona hili hamkuzuia.Tunataka mzingatie taaluma zenu na si mashinikizo ya kisiasa.Naishauri serikali ihamishe mabomu yote hatari yakae mbali na makazi ya watu.
Quote
 
 
+1 #104 2011-02-17 20:46
Ngugu zangu watanzania,mimi nadhani tupunguze kutaja mambo mabaya katika serikali yetu hii, kwani ni mengi na karibu wote tunayajua, mimi nadhani la msingi sasa hivi ni kujadili ni jinsi gani ya kupambana kwa lengo la kuundoa utawala huu, naomba tusipoteze mwelekeo, tafadhali tuone michango juu ya nini kifanyike ili tuulazimishe utawala huu kuondoka madarakani.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner