MwanzoContactsEmail
Home
BOOKMARK THIS PAGE
CCM waitaka dola iwadhibiti Chadema  Send to a friend
Saturday, 05 March 2011 08:45

WANAZUONI, WANASIASA WAPINGA
Na Waandishi Wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema nyendo za chama cha upinzani cha Chadema, zina agenda ya siri ya kuking’oa madarakani kwa kutumia nguvu kinyume cha katiba, hivyo kikaitaka serikali pamoja na vyombo vyake vya dola kuchukua hatua za kisheria haraka.

“CCM inaviomba vyombo vya dola viwe imara kuchukua hatua za kisheria…, wanachofanya Chadema ni kutuchonganisha na wananchi, kutoa kauli hatari za kujaribu kughilibu akili za watu ili kuchochea machafuko, umwagaji wa damu na uasi," alisema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati kwenye mkutano na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam na kuongeza:

“Wanachochea wanachi wakisema, peoples’ power! (nguvu ya umma). Je, mpo tayari kufanya kama Tunisia, Misri? (ambako serikali zilipinduliwa kwa nguvu ya umma).”  

Tamko la CCM limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa, kukitahadharisha Chadema kwamba mikutano na maandamano ambayo waliyafanya kanda ya ziwa yanachochea uasi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kikatiba kinyume cha sheria, hivyo akawaomba waache mtindo huo.

Chiligati jana alisema kwamba viongozi wa Chadema wameonekana kudharau ushauri huo wa mkuu wa nchi wakisisitiza kuwa “wembe ni ule ule hadi kieleweke.”

Kwa sababu hiyo Chiligati alisema wanachofanya viongozi wa Chadema ni kinyume cha sheria za nchi hivyo wakaitaka serikali na vyombo vya dola vichukue hatua za haraka.

Kinachoitisha CCM
Chiligati alisema tangu Chadema waanze ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameshuhudia viongozi wa chama hicho cha upinzani wakitoa kauli za kuupotosha umma na zenye kuchochea uasi na machafuko.

“Kauli za kuwafanya wananchi wafanye fujo ili nchi isitawalike, kauli za kuhamasisha wafanye vurugu kama zile za Misri na Tunisia ili kushinikiza Rais aondoke madarakani kwa mabavu. Kwa hakika ni kauli za hatari mno na zinazoashiria umwagikaji wa damu mkubwa hapa nchini”.

“Mkuu wa nchi ameonya kauli hizi zikome… lakini cha kushangaza, tumesikia majibu ya Dk (Willbrod) Slaa (Katibu Mkuu wa Chadema), Mheshimiwa (Freeman) Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa) wakisema: Wembe ni ule ule hadi kieleweke.”

Chiligati alifafanua kauli ya viongozi hao kuwa ina maana wataendelea na kauli za kuchochea vurugu na nchi isitawalike jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Chiligati ambaye ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, aliweka bayana kwamba tatizo la CCM siyo Chadema kufanya maandamano wala mikutano, bali kauli za viongozi hao.

“Tatizo siyo maandamano. Tatizo ni lugha na kauli za upotoshaji na za kuchochea vurugu, ghasia na uvunjaji wa sheria. Mambo hayo ndiyo Mheshimiwa Rais Kikwete amewaonya na kuyakemea wayaache,” alionya Chiligati.

Chiligati alisema kwamba kauli hizo zingetolewa na Chadema kwenye kampeni za uchaguzi, CCM isingeona ajabu kwa sababu wakati huo kila chama kinajaribu kuvuta hisia za wapigakura... “Sasa kipindi cha uchaguzi kimekwisha, lakini wenzetu bado wanaendelea na yale yale… Ni lini nchi itatulia, tuache malumbano na tufanye kazi ya kutatua matatizo ya wananchi?”

Chiligati alimfananisha Dk Slaa na kiongozi wa upinzani wa Angola, marehemu Jonas Savimbi kwa kile alichosema tafsiri yake ya kuendelea na malumbano baada ya uchaguzi ambao alishindwa kwenye nafasi ya urais akisema kila aliposhindwa hakumtambua aliyeshinda na badala yake kuhamasisha uasi.

Alisema CCM haipingi kukosolewa kwani hiyo ni kazi ya vyama vya upinzani hivyo baada ya uchaguzi, walitegemea Chadema kutumia wabunge wake 48 bungeni kuweka bayana kasoro za serikali ya chama hicho tawala ili zirekebishwe.

“Hapa tunapenda tueleweke kwamba hatusemi vyama vya upinzani visiikosoe serikali, hapana! Uhuru upo wa kutosha kwa Chadema na vyama vingine kukosoa lakini iwe kwa lugha ya kiungwana, siyo matusi, kudhalilishana wala ya uchochezi,” alionya Chiligati.

Chiligati ambaye ni Kapteni mstaafu wa jeshi, aliyataja matukio ambayo Chadema imekuwa ikiyatumia katika kuwapotosha wananchi ili kujipatia umaarufu kuwa ni milipuko ya mabomu katika Kambi ya Jeshi Gongo la Mboto, sakata la Dowans kuidai mabilioni serikali na kupanda kwa gharama za maisha.

Milipuko Gongo la Mboto
Chiligati alisema Dk Slaa amekuwa akitangaza kwenye mikutano yake kwamba baada ya milipuko ya mabomu Mbagala mwaka 2009, serikali ililinyima jeshi fedha za kuteketeza mabomu yaliyokwisha muda wake katika Kambi ya Gongo la Mboto hadi yalipolipuka hivi karibuni na kuua watu 25 kujeruhi 512.

Lakini akasema CCM inaamini kuwa kauli hiyo ni ya uongo na ya uchochezi kwa sababu tume mbili, ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na ya wataalamu wa nje, zinafanya uchunguzi wake na bado hazijatoa matokeo yake.

“Uchunguzi haujatolewa, sasa Dk Slaa amepata wapi matokeo hayo anayoyatangaza kama siyo kuendeleza hulka yake ya uzushi?” Alihoji Chiligati huku akiwataka wananchi wapuuze kauli hizo kwa kuwa ni za uzushi.

Sakata la Dowans
Chiligati alisema kwamba CCM imekuwa ikiwapotosha wananchi kwamba serikali na “CCM tayari wameamua tena kwa furaha kuilipa Dowans Sh 94 bilioni” kutokana na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara.

Alisema huo ni uzushi na uchochezi kwa sababu suala hilo serikali pamoja na CCM wamekuwa wakisisitiza lisilipwe na ifanyike mikakakti ya kisheria ya ama kuliondosha kabisa au kupunguza mzigo. Alielezea hatua zilizochukuliwa na CCM pamoja na serikali kwa nyakati tofauti na kwamba zimewezesha suala hilo kuanza kufanyiwa kazi Mahakama Kuu ya Tanzania.

Isitoshe, alisema wamejaribu kuwatumia hata baadhi ya makada na wabunge wa CCM wenye umaarufu wa sheria kama vile Nimrod Mkono ili kuongeza nguvu ya kupambana na Dowans.

Aliitetea msimamo uliotolewa na Kamati Kuu ya CCM akisema iligundua mambo matatu makuu kuhusu malipo ya Dowans, kuwa ni suala la hukumu, ni jambo la kisheria na kwamba wakati kesi ipo mahakamani serikali isiilipe Dowans.

“Huu ni ukweli kuhusu suala hili, viongozi wa Chadema wanaelewa lakini wameamua kupotosha umma kwa makusudi ili kujenga chuki dhidi ya serikali na CCM,” alilalamika Chiligati.

Matatizo yanayolikabili Taifa
Chiligati alisema matatizo yanayolikabili Taifa ni upungufu wa nishati ya umeme na kupanda kwa gharama za maisha na upungufu wa chakula uliotokana na ukame kwa baadhi ya wilaya nchini.  Alisema matatizo hayo yote Rais Kikwete aliyaelezea katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari pamoja na mikakati ambayo inachukuliwa na serikali yake.

Alirejea hotuba hiyo akisema kwamba Rais Kikwete alisema suala la njaa katika wilaya 23 nchini tayari limeshughulikiwa na vyakula vimepelekwa ili kusambazwa.

Kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, Chiligati alisema kuwa Rais Kikwete alisema ni kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, hivyo vitu mbalimbali nchini navyo bei yake imepaa.

Alisema suala la kupanda kwa sukari serikali imechukua hatua za kuingiza sukari bila kulipiwa ushuru wa forodha na kwamba watahakikisha bei inashuka kutoka Sh 2,200 kwa kilo hadi 1,700.

Hata hivyo, baadhi ya waandishi wa habari walikosoa wakisema bado wafanyabiashara wa Dar es Salaam wanakiuka agizo hilo la Rais na wanauza kwa bei ya kati ya Sh 2,000 na 2,200.

Wasomi, wanasiasa wapinga
Wasomi na wanasiasa wamepinga msimamo huo wa CCM wakisema kauli yake na ile ya Serikali ni hofu isiyokuwa na msingi dhidi ya chama hicho na ndiyo inayovunja Katiba kwa kubana uhuru wa kujieleza.

Wakizungumza na gazeti hili jana, walisema kwa kauli hiyo, Serikali ndiyo inayotaka kuvunja amani na siyo Chadema kwani maandamano yao yamefanywa kwa vibali maalumu vya mamlaka husika.

Chama cha NCCR-Mageuzi na Chama cha Kijamii (CCK) vimeyaunga mkono maandamano hayo vikisema ni sahihi kufanywa kwa kuwa hiyo ndiyo kazi ya vyama vya siasa. Kauli za vyama hivyo zimetolewa siku moja baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wassira kukitisha Chadema na kukionya kisije kikailaumu serikali itakapokosa uvumilivu na kutumia dola kupambana nacho.

Wassira alisema chama hicho kinapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali na kuandaa mpango wa kuiondoa kwa nguvu serikali iliyoko madarakani.

Kauli hiyo ya Wassira iliungwa mkono na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango ambaye alidai kuwa maandamano hayo ya Chadema hayana nia ya kushinikiza Dowans isilipwe, bali kuhamasisha vurugu nchini.

Mwenyekiti wa CCK, Costantine Akitanda alisema serikali ndiyo inayoweza kuvuruga amani kwa kuogopa kivuli cha Chadema ambayo ina wabunge 47 tu bungeni.

“Nchi hii itabaki kuwa tulivu……, labda serikali iamue kwa kuogopa kivuli cha Chadema, kama tulivyoweza kuwaondoa wakoloni bila kumwaga damu, ndivyo hivyo hivyo tutakavyoweza kuiondoa CCM madarakani,” alisema Akitanda.

Alisema Rais Kikwete kujitokeza hadharani na kuilaumu Chadema si jambo sahihi badala yake alitakiwa  atoe msimamo wa serikali kuhusu maandamano yanayofanywa na chama hicho.

Naye Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Uenezi wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura alisema lingekuwa jambo jema kama Wassira angefafanua ni kauli zipi zinazohatarisha amani ambazo Chadema wamezitoa na asipofanya hivyo atakuwa anaitia aibu Serikali.

“Serikali lazima watoe ushahidi unaoonyesha Chadema wamevunjaje amani, kisheria ukipeleka kesi mahakamani ni lazima uwe na ushahidi wa kutosha, watuonyeshe ushahidi wao," alisema Sungura.

Alisema ziara inayofanywa na Chadema ni ya kisiasa na imepewa baraka zote na Jeshi la Polisi: “Kama kuna mtu ndani ya Chadema katoa kauli za uchochezi achukuliwe hatua na si serikali kutoa vitisho kuwa itasitisha maandamano, kosa la mtu mmoja haliwezi kukigharimu chama.”

Sungura alisema CCM kinatakiwa kujiuliza kwa nini hivi sasa Watanzania wakiambiwa waandamane wanakubali kirahisi? “Ukiona watu wanashabikia maandamano tambua kuwa wamechoshwa na yale yanayofanywa na viongozi wao, siku zote imani kutoka kwa wananchi ndiyo kipimo cha mazuri ya Serikali,” alisema na kuongeza:

“Mwaka 2005 wakati Rais Kikwete anaingia madarakani bei ya petroli ilikuwa kati ya Sh950 na 1,050 lakini mwaka huu bei imepanda na kufikia Sh1,800 mpaka 1,890, kipindi hicho hicho sukari ilikuwa Sh600 kwa kilo na leo hii bei ni Sh2,000, sasa hapo wananchi wataendelea kuipenda CCM?”

Alikitaka Chadema kutumia maandamano hayo kuwaelimisha wananchi ili wawe na ufahamu juu ya haki zao za msingi katika kuchagua kiongozi bora.

Wakili wa kujitegemea, Barnaba Luguwa alisema migogoro inayotokea nchini ambayo inaambatana na maandamano inatokana na serikali kushindwa kutekeleza ahadi zake. Alisema hali hiyo inatoa mwanya  kwa raia na vyama vya kisiasa kuingia katika maandamano yanayosababisha madhara mbalimbali kijamii na kiuchumi.

Alisema maandamano yanayofanywa na Chadema ni halali kwa mujibu wa sheria na kuitaka serikali  kupunguza kauli za mabavu zinazotolewa na baadhi ya viongozi wake.

“Chama chochote au mtu binafsi ana haki ya kufanya maandamano ya amani ilimradi tu isivunjwe sheria,” alisema na kuongeza kuwa vyama vya siasa vikifanya maandamano ya amani ni msaada kwa serikali kwani vinaikumbusha wajibu wake katika jamii ili kuzifanyia kazi.

Imeandaliwa na Leon Bahati, Fredy Azzah, Edom Mwasamya na Alphey Athanas

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Sunday, 06 March 2011 09:22
 

Comments 

 
+1 #102 2011-03-06 19:09
chadema hawachochei vurugu bali ccm wakikosa uvumilivu wa kuelezwa u[NENO BAYA] wao wakaamuru vyombo vya usalama kuzuia maandamano au kuwabugudhi waandamanaji ndipo noma litaanzia hapo ccm na rais wao watambue kuwa wananchi ni ngumi mkononi. acheni chadema wafanye kaz yao kama chama cha upinzani.people"s power mtindo mmoja.
Quote
 
 
+2 #101 2011-03-06 09:12
PIPOOOOOOOOOOOO Z PAWA? Neno ili lilikuwepo toka zamani ndani ya CHADEMA. kwanini sasa watu wanaogopa. CCM wala msiogope Fanya kile wananchi watu wanataka. Pia mtu akishinda kwenye uchaguzi mpe haki yake. Yote haya ni dhambi mlizofanya wakati wa uchaguzi. Malipo ni hapa bongo. Mtaondoka tu..
Quote
 
 
+1 #100 2011-03-06 09:06
CCM WANAOGOPA KUANGUKA VIBAYA KATIKA UCHAGUZI UNAOKUJA WA 2015. Cha kufanya sasa wafanye kile wananchi wanachopenda na si kuanza kukisakama CHADEMA. CCM KUANGUKA NI LAZIMA ILI NCHI YETU IWEZE KUPIGA HATUA MBELE. UNAPOSEMA CCM NI SAWA NA KUSEMA TUTAWALIWE NA UFISADI.
Quote
 
 
+1 #99 2011-03-06 08:37
"Peopleeee's.......POWER!" Ama kweli Watanzania tumeamka na sasa tunaweza kutenganisha kilio na kelele; ufisadi na uzalendo; mwanga na giza; haki na msaada na vitu vingi venye tabia kama hivi. Wakati umefika wasisi zote kuwa wamoja kupampana na "DULI ID-CCM".Huyu nduli hana tofauti na yule aliyeng'olewa na Mwalimu Nyerere kwani mporaji wa mali za watanzania, ni dictator, muuaji, mzembe na m[NENO BAYA]! Watanzania wenzangu tuwaunga wakombozi wetu (CHADEMA) mkono ili tung'owe Duli Id-CCM madarakani na ili mwishowe tuijenge Tanzania mpya!
Quote
 
 
+1 #98 2011-03-06 08:15
chiligati katibu mwenezi wangu na wenzio pamoja na mwenyekiti wangu inaonekana dhahiri hamjui siasa na mkiendelea na kauli zenu hizi za ki[NENO BAYA] mtaendelea kukosa dila na utashi wa kuiongoza nchi.nchi ilipo sasa haina kiongozi na ndio maana ya haya yote kwa msingi tumeshindwa kuongoza kabisa tumekalia porojo tuamke watanzania watatuhukumu vibaya.
Quote
 
 
+1 #97 2011-03-06 08:05
ni vigumu kusoma msg za mtanzania tena mwenye umri wa zaidi ya 18 halafu ana analse vitu kama mtotomdogo tena wa miaka 5 wa enzi zile za miaka ya 80 coz hawa ndio walikuwa wamefunikwa, leo hii hata mtoto wa miaka mitatu anaongea poit kuliko huyo anyesema suala la udini amani na julian anayepinga maandamano. Unajua wakati mwingine usipende comment kitu kama huna takwimu... unajua wizara zinafanyaje kazi sasa hivi,, ni u[NENO BAYA] kuunga mkono watendaji wa CCM, CCm kama chama hakina tatizo bali Hawa wanao ongoza Mh rais, na mafisadi wengine ndio waliotufikisha hapa tulipo. Kaka Ben alituachia pesa ya kutosha, anayebisha na abishe bt ukweki ndio huo , huyu baada ya kuingia madarakani akataka aanze na kiwanja chake mwenyewe wakati mwenazke amesha jenga msingi..akamaliza akiba yote kwa madai ya kutafuta wawekezaji , ona sasa kila kitu juu,
Quote
 
 
+1 #96 2011-03-06 08:01
'...Mwaka 2005 wakati Rais Kikwete anaingia madarakani bei ya petroli ilikuwa kati ya Sh950 na 1,050 lakini mwaka huu bei imepanda na kufikia Sh1,800 mpaka 1,890.'

Hivi aneyapanga bei ya mafuta ni serikali? hii sio inategemea hali ikoje duniani kote haswa uko nchi za uarabuni?
Quote
 
 
+1 #95 2011-03-06 04:32
Quoting Julian:
Jengeni hoja bungeni kwenye bajeti,na vikao vingine vya bunge,badala ya maandamano nchi nzima... CHADEMA kuweni realistic,you folk should put forward the targets which are achievable.!!

Even pro-Mubarak regime were sound like you are! Lakini pandora-box ilipofunguliwa ukweli umejulikana kuhusu uozo wa Mubarak-regime.

Kikwete et. al., wanataka CHADEMA wakashindane Bungeni baada ya kubadili kanuni kupunguza nguvu ya CHADEMA. Walidhani ndio mwisho, kumbe "wewe ukijua huku wengine wanajua kule"! Dawa ya ufisadi unaosababisha ugumu wa maisha sio tena njia zinazopendekezw a na CCM, lazima ipatikane tiba mbadala, na ndio hii ambayo inatumiwa na CHADEMA -- kuwaelewesha wananchi madudu ya CCM.
Quote
 
 
+2 #94 2011-03-05 23:43
MIMI NAOMBA CHONDE SANA NDUGU YANGU, RAISI WANGU KIKWETE UJIHUDHURU, SEMA KWELI NINA MZUKA WA MTUTU WA BUNDUKI, MAANA NAONA HERI KUFA KULIKO KUISHI MAISHA YA KUONEWA NA KUTESWA MFANO WA MTU ANAYE KATWA KIUNGO KIMOJAKIMOJA. NDUGU YANGU KAMA NI KUSHINDWA KUONGOZA UMEFAULU MTIHANI.ONA MDA HUU UMEINGIZA NCHI GIZANI, WANAFUNZI WANAFERI, AJIRA HAMNA, WAJAWAZITO WANAKUFA,HUDUMA ZA AFYA FEKI,UFISADI JUU, RUSHA NDIO KAULIMBIU YA CCM,MIKATABA FEKI NDIO CHAKULABORA CHA CCM. JAMANI TUMEVUMILIA TUMESHINDWA BORA KUFA KULIKO KUISHI TANZANIA. HUWIIIIIIIIIIII IIIIIIIIII
Quote
 
 
+2 #93 2011-03-05 23:03
Quoting elibariki yerald:
Quoting lapa:
Quoting Omary Rajab:
Quoting HOMANGO:
mbona hamsemi uislam unaimaliza tanzania CCM na viongozi wakuu katika idara nyingi na nyeti wote ni waislamu naona nyinyi ndio mnataka kulet mauji kama ya wayahudi suala la maisha ya watanzania na ukatoliki limetoka wapi tuongee hoja mbona wakatoliki hawasemi uislam wenu nyinyi wasadiki wa CCM UISLAM


Hii ni sera ya JK na watu wake baada ya kuchakachua kura, sisi waislamu wengine hatumo humo jamani. Msituhukumu bure "PEOPLES POWER"



hoja ya udini imefeli vibaya sana, sasa hivi hoja mpya ni chadema kuchochea machafuko. Waambie hawa rajab mfano ukisoma magazeti fulani ya fisadi mkuu ndio yanayoongoza kuwaponda viongozi wa dini ya kikristo na ukristo na ukisoma jina mwandishi utakuta ni mkristo hawamtumii mwandishi wa kiislamu. fungukeni wandugu sisiemu inawatumia vibaya watanzania wasiofikiri ili wabaki madarakani



CCM WOTE NGAAMONGO TU WASUBIRI TU WANAENDELEA KUBWAYABWAYA NA KUBWATUKA TUUU, NA WATAPIGWA JAMBA JAMBA MPAKA WFUNWE..PIA HILO LA HOJA WA KUWASHAMBULIA HOJA ZA MIGANDO DINI FULANI NI UHUNI.,,SI KILA EMMANUEL NI MKRISTO NA SI KILA MOHAMED NI MUISLAMU,, ACHENI KUHUKUMU KWA MUONEKANO BALI FIKIRINI TATIZO NI NINI? "MARUHANI NI WENGI KATIKA SIASA...........SI WOTE WAENDAO KANISANI WANAMINI KANISA NA SIO WOTE WAENDAO MSIKITINI WANAMINI MSIKITI..WANAFIKI WENGI SIKU HIZI JIFUNZENI..
'MAKUPE WENGI WANAJIFICHA MAKNISANI NA MISIKITI NA KUWAAWANYA WATU KATIKA HISIA KULIKO HOJA................TUWE MACHO!!..

NTASIMAMIA UKWELI DAIMAAAAAAAAAAA AAAAAA.

Haingii akilini kuzungumzia udini kwa nchi yetu ya Tanzania kwani hakuna kitu kama hicho. kinachofanyika ni kupoteza malengo tuache kujadili masuala muhimu yanayotusibu eti udini! hakuna kitu kama hicho. acheni tujadili mambo muhimu zaidi chondechonde!
Quote
 
 
+5 #92 2011-03-05 23:01
Naomba tuunge mkono chadema hawa wanaona mbali sio kama ccm wanaofikilia kila siku kuongeza ugumu wa maisha kwa ufisadi, kudumaza elimu kwa kuzidi kuongeza idadi ya wanafunzi wanaomaliza la saba hawajui kuoma na kuandika,kuingi a mikataba mibovu kama wa Dowans hali wasomi tupo wengi tungeweza kuwasaidia na sio kukurupuka. Kama ni damu imemwagika sana tunachotaka kufanya sasa ni kupunguza umwagaji damu utokanao na vifo vya watoto na wamama wajawazito, wagonjwa ambao huduma zingekuwepo wangepona n.k,. CCM achieni madaraka chadema wachukue hatamu. MIMI NI MWANA CCM
Quote
 
 
-6 #91 2011-03-05 22:57
sikubahatisha nilipoandika 'MASKINI UKATOLIKI UNAINYEMELEA TANZANIA' nina kila sababu ya kusimamia katika kauli yangu, na wala haihitajiki kuwa na PHD kulitambua hili ni strategy ambayo ilianzia katika waraka wa uchaguzi, ikafua[NENO BAYA] nakusimamishwa kwa padri SLAA kugombea nafasi ya urais, jaribu kuangalia safu ya uongozi wa CHADEMA, angalia tukio la zito kabwe kunyimwa asigombee nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA,angalia baraza la mawaziri la kambi ya CHADEMA bungeni (ni makosa kuita kambi ya upinzani)na KAKOBE KUAMRISHA WAKRISTU WAFUNGE MAKANISA WAKAMCHAGUE PADRI SLAA ALITUMWA NA CCM PIA? Tena hapo hata uzinzi ulionekana si kosa tena katika makanisa.
katika hili CCM HAIHUSIKI NA WALA MIMI SI MWANA CCM ila palipo ukweli lazima kusema. jaribuni kuangalia mfano wa RWANDA waliosimama ICTR wengi wao walikuwa ni mapadri wa KIKATOLIKI mlishawahi kujiuliza ni kwa nini....ndo km hv inaanza katika waraka, halafu tumtafute mwenzetu...... then tudominate kumbukeni kuna kundi kubwa halitakubaliana na hilo ndo hapo sasa machafuko yanapoanzia. That is the reality.
UFISADI haukuanza leo tanzania enzi ya nyerere ilijulikana km UHUJUMU UCHUMI, mbona watu hawakuandamana? haimaanishi kuwa natetea ufisadi bt itumike njia sahihi ktk kuutokomeza (tunazo sheria) na si kikundi cha watu wachache watake kutumia kama daraja la kuwatawala wengine.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI AFRICA.
NAKUPENDA TANZANIA NCHI YANGU YA AMANI.
Quote
 
 
+3 #90 2011-03-05 22:57
Ni ajabu kuona akina chiligati wanafikiri watanzania wa mwaka 47 ndiyo waliopo sasa hivi! Anasema muda wa kampeni umeisha inabidi nchi itulie? utulivu gani anaouzungumzia Mr Chiligati? Utulivu ili wale nchi yetu bila bugudha! Pia najaribu kufikiri chiligati ni nani hadi aanze kuzungumzia masuala ya gongo la mboto, dowans,ugumu wa maisha? haya ni masuala yaliyotakiwa kuzungumziwa na rais ambaye ameshindwa kuturidhisha sisi wananchi! yeye ilibidi alalamike kama chadema imekikashifu chama chake na siyo suala la serikali kwani chama chao kilishinda kimeunda serikali basi waiachie serikali ifanyekazi na siyo chama tena. Wananchi tukiambiwa ukweli mnadai wanaotwambia wanasababisha uchochezi!! kumbukeni tunataka mabadiliko ya kweli kama ccm hamuwezi pisheni njia waje wengine.
Quote
 
 
-4 #89 2011-03-05 22:52
jamani washkaji itabidi tuanze maandalizi ya nguvu masela anzeni mazoezi ktk kambi endapo fujo wakiaznzisha awa jamaa basi wajue Mungu ni Mkubwa na ndio mfalme,naona mashabiki ni wengi sasa nawanataka vita ya wenyewe kwa wenyewe.Wao wanaongea ya Tunisia,Egypt,L ibya awajui ata sababu wakatu sababu jubwa ni pambano kati ya Palestina na Wayaudi.Poa tu ikibidi basi itabidi kila mtu ashike siraha wenda itakua njia nyepesi kuraisishiwa kwenda peponi.Na hatutokubali nchi kupinuliwa kwa fujo.Km Ubaya ubaya tu
Quote
 
 
0 #88 2011-03-05 22:36
Quoting dina:
Quoting mikwaju-kuwait:
Ee mungu iepushe nchiyangu na machafuko ya siasa.
Wanaosababisha watu wanguwamwage damu wachukue haraka watutangulie ahera.

toa uchuro hapa huna aibu kuomba watu wafe...au unamwomba shetani

kufa ni uchuro,vipi Mabadiliko bila kufa,kwanza huyo kamuomba, Mungu si Asuman ukimwombe mtu ubaya hali ya kuwa huyo mtu ana nia ya kweli basi ndo umempiga chura teke, kubwa mungu anaangalia nyoyo zetu kama ni njaa zetu binafisi hata shetani akiomba atakubaliwa sababu mungu hataki ubinafsi Quoting Mkenya:
Kenya kwetu iliaanza hivyo-hivo siku baada ya siku, maneno baada ya maneno hatimaye LIKALIPUKA na MACHAFUKO kusamba nchi nzima." nduguzangu nina TOA ONYO ONYO na HADHARI ZOTE muchukuwe " musije dumbukia katika MTEGO HUU. ooh OOh poor TANZANIA mlicho jenga miaka 48 yote itakwenda teketea na kwisha kwa siku moja baadaye majuto majuto .take care!!

huyu jamaa mmempa point hasi 17,lakini anasema hivyo kwa huruma tu lakini gazeti nina lina-chembechembe za ukenya
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner