Polisi yakamata 130 kwa tuhuma za ugaidi, 36 kortini Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema limewakamata watu 130 katika mikoa mbalimbali kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu vinavyohusishwa na ugaidi.
Sh111 bilioni kutumika upimaji ardhi kidijitali Zanzibar Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kesho anatarajia kuzindua mradi wa upimaji ardhi kidijitali wenye thamani ya Euro 37 milioni (Sh111.187 bilioni).
Rais Faye wa Senegal aanzisha chama chake Rais wa Senegal, Bassirou Faye, ameanzisha rasmi chama kipya cha kisiasa, hatua inayothibitisha kuvunjika kwa ushirikiano wake wa kisiasa na kiongozi wa chama tawala cha Pastef, Ousmane Sonko.
Tanzania yaorodhesha hatifungani katika Soko la Hisa la London Tanzania imefanikiwa kuorodhesha hatifungani yake ya kwanza ya kimataifa iliyotolewa kwa Shilingi ya Tanzania na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) katika Soko la Hisa la London (LSE).
Uwanja AFCON Arusha wafikia asilimia 88 Mradi wa ujenzi wa Uwanja utakaotumika kwa Fainali za AFCON 2026 umefikia asilimia 88 na utakamilika rasmi mwezi ujao.
Ubabe wa Zuchu katika tuzo, digital streaming Ikiwa ni miaka zaidi ya sita tangu Zuchu alipotoka kimuziki chini ya WCB Wasafi, mwanamuziki huyo wa Bongofleva ameendelea kuonyesha ukubwa wake ndani na nje akiweka rekodi mbalimbali kupitia...
Dawa ya moto masokoni ni kuweka mifumo ya kinga Julai 5, 2026, lilitokea tukio la kuhuzunisha ambapo maduka zaidi ya 54 yaliteketea kwa moto na mengine 23 kuokolewa katika eneo la Lumumba jijini Mwanza.