CCM yampa kibarua kigumu RC

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela .

Muktasari:

Kimesema kimeamua kumuomba Shigela kuingilia kati kwa madai kwamba, baadhi ya uongozi wa kata na tarafa umefanya njama za kuwalinda wahusika wa uuzaji mahindi hayo, yaliyopelekwa tangu Mei Mosi, mwaka huu.

Kilindi. Chama cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Ngobole, Kata ya Saunyi wilayani hapa, kimemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela kuingilia kati sakata la kuuzwa kwa mahindi ya msaada waliyopelekewa wanakijijini.

Kimesema kimeamua kumuomba Shigela kuingilia kati kwa madai kwamba, baadhi ya uongozi wa kata na tarafa umefanya njama za kuwalinda wahusika wa uuzaji mahindi hayo, yaliyopelekwa tangu Mei Mosi, mwaka huu.

Katibu wa CCM wa kijiji hicho, William Lazaro alisema siku hiyo Serikali ilipeleka magunia 27 ya mahindi ya msaada kwa wananchi wanaokabiliwa na njaa kijijini Ngobole na kwamba, baada ya kufikishwa tisa hayakuonekana.

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo alisema hajafikishiwa malalamiko hayo na kuahidi kufuatilia.