Kiongozi mbio za Mwenge ashtukia ‘wakomba sufuria’

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, George Mbijima .

Muktasari:

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye nyumba hiyo, alikemea tabia ya baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kufuja fedha.

Kigoma. Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, George Mbijima amehoji uhalali wa Sh6.2 milioni kutumika kwa ufuatiliaji mradi wa ujenzi wa nyumba ya mganga wa Zahanati ya Rusimbi mjini Kigoma.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye nyumba hiyo, alikemea tabia ya baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kufuja fedha.

Pia, alihoji kwa nini kiasi hicho kikubwa kitumike kufuatilia utekelezaji mradi huo unaogharimu Sh58.6 milioni.

Mwenyekiti wa mradi, Amrani Muhende alisema uliibuliwa na wakazi wa Kata ya Rusimbi na kufadhiliwa na fedha ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) ili kupunguza adha ya mganga kuishi mbali na zahanati.