‘’Watakaohujumu mashine bandarini watimuliwe’’

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa

Muktasari:

Mashine hizo za ukaguzi zilizotolewa na serikali ya China,zimegharimu Sh20.2 bilioni.

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuwatimua kazi watumishi watakaohujumu mashine za kukagulia mizigo bandarini (scanner) ili kuzuia upotevu wa mapato.

Mashine hizo za ukaguzi zilizotolewa na serikali ya China,zimegharimu Sh20.2 bilioni.

Akizungumza leo  wakati wa uzinduzi wa mashine tatu za kukagulia mizigo katika makontena, Mbarawa alisema kama wafanyakazi hawatakuwa waaminifu uwepo wa mashine hizo hautakuwa na maana.

‘‘Leo tumezindua mashine hizi za kisasa za kukagulia mizigo kwenye makontena lakini kama watumishi wetu hawatakuwa waaminifu hazitatusaidia,’’alisema na kuongeza :

‘‘Mkurugenzi Mkuu wasimamie kwa karibu watalaam watakaokuwa wanazisimamia ‘scanner’ ili zifanye kazi iliyokusudiwa, wakikosa uaminifu waondolewe.’’ alisema.