MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Mattaka ang'oka ATCL
BOOKMARK THIS PAGE
Mattaka ang'oka ATCL  Send to a friend
Monday, 23 May 2011 21:56

Fredy Azzah
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka ametangaza kustaafu kazi huku akijivunia kubadilisha nembo, ingawa ameliacha likiwa halina hata ndege moja inayoruka.

Mattaka aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa alistaafu rasmi Mei 11, mwaka huu baada ya kufika umri wa miaka 60 na kwamba alishindwa kulifufua shirika hilo la umma kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa menejimenti. Alitaja moja ya sababu hizo kuwa ni mzigo wa madeni.

“Naondoka lakini najivunia kuiondoa ATCL chini ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) waliokuwa wameingia ubia, pia najivunia kuleta nembo mpya ambayo inatumika sasa,” alisema Mattaka.

Desemba 2002, Shirika la Ndege Tanzania (ATC), lilibinafsishwa kwa kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) na kubadilisha jina lake kuwa “Air Tanzania Company Limited” (ATCL). “Wanasema najiuzulu.

Hii siyo kweli, nastaafu kwa mujibu wa sheria, ingetakiwa nistaafu kuanzia Mei 11, lakini ni barua tu ndiyo ilichelewa kuja, nimeomba kustaafu na nimekubaliwa,” alisema Mattaka. Mattaka alisema tangu kuteuliwa kwake kuliendesha shirika hilo mwaka 2007, walikuwa na nia ya kulifufua lakini sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao zilikuwa kikwazo.

“Shirika lolote la ndege linahitaji mtaji ili liweze kujiendesha, sisi tumechukua shirika likiwa na mtaji hasi wa Sh43 bilioni na madeni yaliyofikia Sh23 bilioni,” alisema Mattaka.

Alisema katika kujitahidi kulifufua shirika hilo, kuanzia mwaka 2007 mpaka mwishoni mwa 2008, walifanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kununua ndege moja yenye uwezo wa kubeba abiria 50 na kukodi nyingine aina ya Air Bus, shughuli ambayo alisema waliifanya katika mazingira magumu.

Alisema baada ya mwaka huo, mafuta ya ndege yalipanda kwa zaidi ya asilimia 50, jambo lililoyafanya mashirika mengi ya ndege yaliyokuwa yakiendeshwa bila ruzuku ya serikali kuanguka.

“Mwishoni mwa 2009 ndipo serikali ikaanza kutoa fedha kidogo kidogo ambazo hata hivyo, ilizielekeza kwenye kulipa madeni. Napenda tu kusema kuwa sasa serikali inatakiwa kuwa na shirika lake la ndege,” alisema Mattaka na kuongeza: “Unapokuwa katika shirika la umma ukastaafu bila matatizo ni jambo la kumshukuru Mungu, kwa hiyo kwa sasa napenda tu kumshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa.”

Amlaumu Mkapa
Awali, Mattaka alisema katika uongozi wake ndani ya mashirika ya umma, kamwe hatamsahau Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alimsimamisha alipokuwa Mkurugunzi wa Mfuko wa Jamii wa (PPF) kutokana na kashfa mbalimbali, ikiwamo ya rushwa na ubadhirifu wa fedha.

Anasema kitendo cha kusimamishwa kwake ghafla kilimuumiza sana, ingawa anadai kuwa baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Usalama wa Taifa kuchunguza, walibaini kuwa hapakuwa na ukweli wowote wa kashfa zilizomfanya asimamishwe kazi.

“Unajua bwana siku zote mti wenye matunda ndiyo hurushiwa mawe, waliona majengo yanaibuka tu, mara PPF House, PPF Tower na kile Kijiji cha PPF kule Arusha, wakasema lazima hizi ni 10 percent.” “Walichunguza wakakuta yote yale hayana ukweli wowote na wakanilipa stahili zangu ambazo ndizo zilinifanya nikae takribani miaka ninne mpaka nilivyokuja tena huku ATCL.”

Alisema ameondoka ATCL na kuliacha likiwa halina hata ndege moja inayoruka akidokeza kwamba moja ipo Afrika Kusini ikifanyiwa matengenezo ambayo anasema yamekamilika na kinachosubiriwa ni Serikali kulipa fedha za matengenezo.
Alisema ndege nyingine ipo nchini lakini haifanyi kazi kutokana na kuhitaji matengenezo ya lazima. Mattaka alisema, serikali imemteua William Haji, kukaimu nafasi anayoiacha.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Monday, 23 May 2011 23:28
 
Comments 

+1 #35 2011-05-24 23:53
ANA HAKI YA KUSEMA DAVID MATTAKA SIO SHIRIKA LA NDEGE TU MH BENJAMINI MKAPA NA SWAHIBA SUMAYE WAMEUZA NCHI SIKU NYINGI WATANZANIA HAMJIJUI TU,MADINI ASILIMIA TISINI YA MAKAMPUNI WALISAINI MIKATABA WAO MASHIRIKA YA UMMA KAMA VILE NBC,TTCL,ATC,TA NESCO NA MENGINE MENGI WALIWAPA MAKABURU MPAKA MAREHEMU BABA WA TAIFA ALIANZA KUWAPIGIA KELELE MNAUZA NCHI,NA AKASEMA MTAUZA MPAKA MAGEREZA NYIE KWA UCHU WENU NA KWELI MH.MAGUFULI AKAANZA KUZIGAWA NYUMBA ZA SERIKALI NI BAHATI NZURI JK AKASIMAMISHA U[NENO BAYA] HUU.MATTAKA ALIFANYA KAZI NZURI SANA PPF NA KUONGEZA VIWANGO VYA MALIPO KWA WASTAAFU WAKAONA ANAWANUFAISHA WANANCHI WAKAMSIMAMISHA HAO AKINA MKAPA NA SUMAYE.
Quoting Mchukia majungu:
Quoting HUSNA:
Akina mataka ni moja ya aina ya watendaji wakuu waliowengi katika serikali ya awamu hii, Anamshutumu Mkapa kwa lipisasa huyo swahiba wake aliyemteua ona anavyo mwaibisha. Utendaji mbovu wa serikali ya awamu hii hauhitaji semina elekezi ya aina yeyote ni Kuwaondoa katika utendaji hawa akina mattaka. Jk unaziona hizi aibu au nasisi raia unataka kutupatia semina elekezi ili tukubaliane na huu u[NENO BAYA] ha ha haa! aibu embu tuwafanyie wt kazi jamani! Mattaka Uende salama nadhani hata Familia yako inapata shida sana.

Anapaswa kufilisiwa na uso wake usionekane tena mbele ya watu, mitu mingine hasara kweli.
Quote
 
+1 #34 2011-05-24 22:10
Nafikiri shirika hili limehujumiwampa ka likafa. Mbona mashirika ya ndege ya Kenya Uganda na Rwanda yanadunda! Hata nchi ndogo kama Rwanda iliyokuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe miaka 16 iliyopita inatupita kwenye ufanisi wa usafiri wa anga? Tujivunie nini? Tunahitaji kiongozi kama Kagame asiyeendekeza ufisadi. Dola moja ni faranga 600 za Rwanda. Kwetu ni karibu sh 1500 kwa dola moja.Hela yao ni stable haiyumbi kama ya kwetu. Sisi kila kukicha ni kupambana na Chadema badala ya kuibuka na mbinu za kuijenga nchi. Shirika liloanzishwa majuzi la Precision air bado linatamba. Mwanzoni walilisuta eti la wachaga. Tunakimbilia ukabila badala ya kujenga nchi. Sasa bila shirika hili tungekuwa wapi! Shirika la taifa la usafiri wa anga linapaswa kuongozwa na watu makini na kudhibi[NENO BAYA] na serikali. Shirika la usafiri wa anga la kenya linasifiwa kwa kuwa na viwango vya kimataifa na kutengeneza faida kubwa! Tatizo letu ni ufisadi!
Quote
 
+1 #33 2011-05-24 18:31
NEMBO UMEANZISHA LAKINI NDEGE ZENYEWE ZA KUWEKA HII NEMBO YAKO ZIKO WAPI?JAMANI KTK NCHI HII KUNA WATU WA AJABU.KAMA WASEMAVYO WENGINE KUWA WEWE MATAKA UMELETA MATAKATA KATIKA SHIRIKA HILI NI KWELI KABISA,NI AFADHALI HIZI TAKATAKA ZAKO ULIZOANZISHA ATCL ZAKULETA NEMBO UONDOKE NAZO.
Quote
 
+1 #32 2011-05-24 18:01
Huyu kweli ni Mataka, nasema huyu ni matakataka. Ameshindwa kulifufua shirika, ni kama Dakitari anayemmalizia mgonjwa badala ya kumsaidia
Quote
 
+5 #31 2011-05-24 16:22
KQ-KENYA WAMEAGIZA BOEING 787 ZINGINE 8,WATANZANIA HATUKO SERIOUS NA MAENDELEO TUMEWEKA SIASA NA NGOMA ZA UTAMADUNI MBELE WAKATI WENZETU WANAJENGA UCHUMI.
INASIKITISHA SANA KUA SASA HAKUNA NDEGE HATA MOJA, LAZMA TUJIULIZE ZILIKUA NANE, IKAANZA KUPOTEA MOJAMOJA.....NINI SABABU?
INAMAANA KILA MWAKA KUNA RIPOTI NA MAPENDEKEZO MAPYA, JE NI NANI HAKUTEKELEZA?
JE MNAJUA NDEGE NDIYO BENDERA INAYOLITANGAZA TAIFA NA UTALII NJE YA NCHI? MBONA KQ YA KENYA NA AIR UGANDA WANASHAMIRI?
NA KWA AIBEU KUBWA HATA RWANDA WAMETUSHINDA WANATUA NAIROBI MARA4 KWA SIKU. SISI HAPO MTWARA NA KIGOMA TUMESHINDWA.
SERIKALI IACHE SIASA NA LONGOLONGO ATCL IUZWE KWA WATANZANIA KAM PRECISION AU MZEE MENGI MUONE. ACHENI MAWAZO YA KUUZIA WAZUNGU.....KUMBUKENI FAIDA ZITAPELEKWA KUANZISHA MAKAMPUNI MENGINE ULAYA AMBAPO WATOTO WENU HAWATAPATA KAZI, MPENI MZARENDO ILI AKIPATA FAIDA AFUNGUE MAKAMPUNI NDANI YATAKAYOAJIRI VIJANA WAKITANZANIA
Quote
 
0 #30 2011-05-24 15:48
Bwabna Mataka, tumeambia Mkapa alikusimamisha PPF ili amweke pale mpwa wake, mtoto wa dada yake, kuwa mkurugenzi, na kwamba huyo ndie mkurugenzi hadi leo. Je ni kweli?
Quote
 
-2 #29 2011-05-24 15:39
Nenda ukampunmzike ule mapesa yako kwa raha zako.Abirae ndie mwenye ashindawe ni Uzuzuwe..
Hata mimi wakiniweka nitaiba,,,,
Quote
 
-2 #28 2011-05-24 14:58
Angalieni mazuri na mabaya ya Mataka, msibobebee kwenye mabaya tu wajemeni
Quote
 
+1 #27 2011-05-24 14:23
sina koment kwa kuwa Matakataka anajua kuwa ATC aliiua yeye na swahiba wake. In fakti huyu jamaa hakuwa na ujuzi wa kuendesha hata shirika la mikokoteni achilia mbali ndege......siwezi ongelea laizi uozo unaoendelea kuteu watendaji muhimu kwa kujuana. Sasa huyu aliyeteuliwa anaenda kufanya nini wakati hakuna hata kipepeo kimoja hewani. Hebu Mwananchi tupoatie sifa na uzoefu wake.
Quote
 
+2 #26 2011-05-24 14:19
Quoting Ibrahim Ali:
RAISI WA NCHI ANATEMBEA NCHI ZA NJE NA NDEGE YA AINA YA GULF-STREAM EXECUTIVE JET yenye thamani ya $.75,000,000 wakati nchi ni masikini, na walipa kodi ni masikini sana hata chakula hawana, Hayati Mwalimu alikuwa akipanda ndege za kiraia kwenda nchi za nje,katika miaka 23 ya utawala wa mwalimu safari zake hazijazidi 25.Raisi kikwete muda wa miaka 5 safari zake na hiyo ndege zinakaribia 100 na kila safari ndege hiyo inatumia mafuta na sio maji, kila ikiruka inatumia dola 50,000-75,000. mlipaji ni masikini wananchi. Angalia jirani wetu Rais Kibaki wa kenya safari zake kwa mwaka ni chache kuliko limbukeni rais wetu.inaonekana JK hana uchungu na nchi, mfano anaoonyesha kwa umma sio mzuri lakini hakuna wa kumweleza ukweli, kwa sababu hata hili bunge la nchi limejaa wanafiki watupu.PUNDA NI PUNDA tu.

Kheri mbaya wa sura kuliko roho na fikira. Akina mama walikuwa wanasema ni K tu eti handsome. Na bado miaka 4 tu[NENO BAYA]ma.
Quote
 
+1 #25 2011-05-24 14:15
Quoting HUSNA:
Akina mataka ni moja ya aina ya watendaji wakuu waliowengi katika serikali ya awamu hii, Anamshutumu Mkapa kwa lipisasa huyo swahiba wake aliyemteua ona anavyo mwaibisha. Utendaji mbovu wa serikali ya awamu hii hauhitaji semina elekezi ya aina yeyote ni Kuwaondoa katika utendaji hawa akina mattaka. Jk unaziona hizi aibu au nasisi raia unataka kutupatia semina elekezi ili tukubaliane na huu u[NENO BAYA] ha ha haa! aibu embu tuwafanyie wt kazi jamani! Mattaka Uende salama nadhani hata Familia yako inapata shida sana.

Anapaswa kufilisiwa na uso wake usionekane tena mbele ya watu, mitu mingine hasara kweli.
Quote
 
+2 #24 2011-05-24 14:11
Quoting Ibrahim Ali:
Mkurugenzi David Muttaka ni mmoja kati ya viongozi waliofilisika sera kichwani.
sidhani kama mtu aliye soma baada ya kushindwa na kazi aliyopewa na serikali anaweza kujisifu ya kuwa kabadilisha nembo, huu ni u[NENO BAYA] mkubwa sana. tatizo kubwa la viongozi wote wa serikali wanapopewa kazi ya umma ni sawa na kupewa leseni ya kuwa wizi na fisadi wakubwa bila ya kujali UZALENDO, na kwa sababu serikali haiwachukulii hatua za kisheria kiongozi anapo iba mali ya umma , sana sana serikali itamfukuza kazi huyo kiongozi,mwizi hawezi kumshitaki mwizi mwenzie. miaka 50 ya UHURU shirika letu la ndege halina hata kidege kimoja,AIBU iliyo baki bora tuirudishi nchi kwa wakoloni waje kututawala tena na watufundishe jinsi ya kuwa WAZALENDO. kenya iko mbele kwa miaka 50 na sisi tuko nyuma kwa miaka 50. UHURU SIO BENDERA TU UHURU NI WANANCHI KUWA WAZALENDO wapendao nchi na mali za umma.

Mkuu umesema vyema. Ni kheri kutawaliwa na mwingine kuliko na mzawa mwenzako. Hivi aliyemteua huyu [NENO BAYA] kuwa mkuu wa shirika hili alifikiriaje, ni wale wale. Kachukua kila cha shirika anaenda kula na [NENO BAYA] zake.
Quote
 
+2 #23 2011-05-24 14:04
mi naenda mbali zaid sio kila kiongozi mkuu akifa apigiwe wimbo wa taifa na bendera iwe nusu mlingoti!!mabab u zetu tuliwaona matahira kipindi cha biashara ya utumwa ila sisi ndo mazuzu zaidi,kweli unaita PRESS na kuwaambia kuhusu NEMBO kweli unatuheshimu lakini? pamoja madeni na ulikua huna mtaji je kuna mkakati gani ulioucha kuona kama shirika linafufuka?mmhh haya bwana utakumbukwa kwa hio NEMBO kama hilo ndo umeona lilimfanya rais akuteue au ndo lililokosekna hapa nchini
Quote
 
+3 #22 2011-05-24 13:22
there is no more embty-head man in this world like mattaka. this man is real bogus ,, and a purely great sabotage. IT`S BETTER THIS MAN TO HANG HIMSELF
Quote
 
+2 #21 2011-05-24 12:47
RAISI WA NCHI ANATEMBEA NCHI ZA NJE NA NDEGE YA AINA YA GULF-STREAM EXECUTIVE JET yenye thamani ya $.75,000,000 wakati nchi ni masikini, na walipa kodi ni masikini sana hata chakula hawana, Hayati Mwalimu alikuwa akipanda ndege za kiraia kwenda nchi za nje,katika miaka 23 ya utawala wa mwalimu safari zake hazijazidi 25.Raisi kikwete muda wa miaka 5 safari zake na hiyo ndege zinakaribia 100 na kila safari ndege hiyo inatumia mafuta na sio maji, kila ikiruka inatumia dola 50,000-75,000. mlipaji ni masikini wananchi. Angalia jirani wetu Rais Kibaki wa kenya safari zake kwa mwaka ni chache kuliko limbukeni rais wetu.inaonekana JK hana uchungu na nchi, mfano anaoonyesha kwa umma sio mzuri lakini hakuna wa kumweleza ukweli, kwa sababu hata hili bunge la nchi limejaa wanafiki watupu.PUNDA NI PUNDA tu.
Quote
 
Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!

Banner
Banner
Banner