
| Slaa awasilisha ushahidi kumbana Chenge | Send to a friend |
| Friday, 08 July 2011 21:32 |
|
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ameendelea kumkalia kooni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na sasa amewasilisha serikalini uchambuzi wa ushahidi utakaosaidia kumtia hatiani mwanasiasa huyo, dhidi ya tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa rada. Dk Slaa aliwasilisha waraka wa uchambuzi wa kisheria kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Nchini (DPP), Eliezar Feleshi, akiweka wazi kwamba Serikali ya Tanzania ina mamlaka ya kufanya uchunguzi dhidi ya uhalifu kwa watuhumiwa ambao ni raia wa Tanzania. Katika waraka huo ambao Mwananchi umeuona, Dk Slaa ameweka wazi kuwa kazi iliyofanywa na Ofisi ya Makosa ya Jinai ya Uingereza (SFO) ililenga kubaini makosa ya kuvunja sheria nchini Uingereza na kwamba Tanzania ilipaswa kufanya uchunguzi wake katika jambo hilo. “Kimsingi SFO ilikuwa inafanya upelelezi kuhusiana na uvunjifu wa sheria chini ya mamlaka yao yaani Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini. Makosa ya ufisadi wa rada yaliyofanywa na Watanzania (na mawakala wao) ni makosa dhidi ya Sheria za Tanzania,” inaeleza sehemu ya waraka huo na kuongeza:“Ni kwa msingi huo mimi niko “on record” ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuitaka Serikali ya Tanzania nayo kuanzisha upelelezi wa kwake kwa mujibu wa Sheria za Tanzania kwani walioibiwa ni Watanzania na fedha zilizoibiwa ni za Watanzania”. Dk Slaa alisema hakuna mantiki ya upelelezi wa ufisadi uliofanyika Tanzania kuachiwa mamlaka nyingine. Hatua hiyo ya Dk Slaa ni kuitika wito wa DPP ambaye juzi, alimtaka kuwasilisha nyaraka zenye ushahidi dhidi ya watuhumiwa wa rada serikalini ili ziweze kufanyiwa kazi, akieleza kuwa ushahidi alionao hautoshi kumtia Chenge hatiani kama atafikishwa mahakamani. Msimamo wa Feleshi unaungwa mkono na Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Fredrick Werema, ambaye pia alimtaka Dk Slaa asaidie kupelekea ushahidi kwa kuwa sheria inaruhusu.Kadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah pia alishaweka bayana kwamba taratibu za kuwasilisha ushahidi ofisini kwake ziko wazi, hivyo kumtaka Dk Slaa kutumia njia hizo ili ushahidi huo akaufanyie kazi. "Kama Chadema wanao (ushahidi), kama alivyoeleza Dk Slaa, walete tutaulinganisha na ushahidi tulionao ili tuone kama unatosha kuitetea kesi hiyo mahakamani," alisema Dk Hoseah Ambana Chikawe Na SPCO1/D/MC ya Machi 21, 2008, iliyosainiwa na msimamizi wa kesi hiyo, Mathew Cowie kuhusu suala la rada.“Attorney General (Mwansheria Mkuu wa Serikali), ndiye Mshauri Mkuu wa Serikali kwa masuala ya kisheria, na hivyo ni dhahiri barua hiyo Serikali inaifahamu. Kutokana na barua hiyo, ni dhahiri Chikawe alipotosha Bunge na Taifa kwa kusema kuwa Serikali haina ushahidi,” unasema waraka huo. Barua/Fax ya Mark Simpkins wa SPS ya tarehe 30 Agosti, 1997 ni ushahidi dhahiri wa ushiriki wa Andrew Chenge,”anaeleza DK Slaa katika barua yake na kuongeza:“DPP anao mkataba wenyewe wenye kuonyesha dhahiri “Financial Arrangement” na kama hana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inao.
Feleshi alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa na gazeti hili azungumzie kauli ya Dk Slaa aliyoitoa Jumatano wiki hii kuwa Serikali ina ushahidi dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wa rada ila imeamua kuwalinda. Sakata la Rada Jumatano wiki hii Dk Slaa alisambaza ripoti ya SFO yenye kurasa 11 na kusisitiza kuwa ushahidi huo unatosha kumtia Chenge hatiani.Dk Slaa alisambaraza ripoti hiyo kufuatia kauli ya Chikawe aliyedai Serikali haina ushahidi wa kuwafikisha watuhumiwa wa kashifa ya rada mahakamani. Kitendo cha Dk Slaa kukubali ombi hilo la Serikali kinabadili sura na msimamo waliokuwa nao yeye pamoja na chama chake wa kutowasilisha ushahidi na badala yake kufanya maandamano nchi nzima kuueleza umma kuhusu tuhuma hizo za rada. Dk Slaa alisema amefikia hatua ya kukubali kuandaa na kuwasilisha ushahidi huo kufuatia kauli ya DPP iliyotaka afanye hivyo kwa maelezo kuwa unaweza ukawa una tofauti na ule ambao Serikali inao. |



Geofrey Nyang’oro












Comments
Usifikirie hao waingereza wana wema na sisi, hiyo ni chambo ndugu yangu ya kutusambaratish a ili wao watimize fikra zao za kutuvuruga. Ndugu hilo ni kaa la moto toka uingereza jifanyeni kulishabikia muone kitakachotokea.
Wewe laiza unafikiri kwa kutumia kiungo gani? wakati watanzania tunapambana na kero la mafisadi wanaosababisha maisha yawe magumu kiasi hiki wewe unabeza. Inaonekana na wewe fisadi jingine linaibukia.
Kwa hili niseme tu kuwa Dokta Slaa na mwandishi mmetaka umaarufu wa kisiasa na wa gazeti ili liuzike lakini hakuna hoja yenye mashiko mliyotuletea. Bado hatudanganyiki
HATA MIMI KTK UJUMBE WANGU NAMBA 19 NIMEZUNGUMZIA KOSA LA MWANDISHI LKN NASHANGAA WATU WANANISHAMBULIA ! TUSIFANYE UWANJA WA MAONI KUWA KIJIWE CHA YANGA NA SIMBA. HAPA TUNAZUNGUMZIA MAMBO MUHIMU YA KUJENGA TAIFA. MWANDISHI AKIKOSEA LAZIMA TUSEME