MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Saini ya Pinda yaghushiwa bungeni
BOOKMARK THIS PAGE
Saini ya Pinda yaghushiwa bungeni  Send to a friend
Wednesday, 27 July 2011 21:32

Neville Meena na Habel Chidawali
VITUKO vya wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimezidi kuongezekana; sasa baadhi ya wabunge wanadaiwa kugushi sahihi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa malengo ambayo bado hayajafahamika.
 
Kitendo cha kugushi sahihi ya Waziri Mkuu ndani ya ukumbi huo kunawaathiri zaidi wabunge wa upinzani, hasa wa Chadema ambao wamekuwa wakipelekewa ‘meseji’ za kuwadanganywa kuwa wanaitwa na Waziri Mkuu.
 
Juzi jioni kabla ya kikao cha Bunge kuahirishwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alialazimika kuomba mwongozo wa Mwenyekiti kukemea kitendo hicho alichokiita kuwa ni cha kihuni.
 
Lukuvi asimama mara tu baada ya Bunge kumaliza kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ambayo yalikuwa yalijadiliwa kwa siku mbili mfululizo.
 
“Naomba mwongozo wako kwamba, humu ndani imejitokeza tabia ambayo naona imezoeleka kidogo. “Kuna watu wanawaandikia wenzao meseji za kuwasumbua kwamba wanaitwa na mtu fulani halafu wanaweka sahihi na wakati mwingine haitokei,” alisema Lukuvi na kuongeza:
 
“ Nimeisikia hayo wiki iliyopita, lakini leo Mheshimiwa Joseph Selasini (Chadema) ameitwa kwa meseji inayodaiwa kuwa imesainiwa na Waziri Mkuu na hii nyingine ameitwa Mheshimiwa Leticia Nyerere (Chadema) kwamba anaitwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wakazungumze maneno ya maana, lakini Waziri Mkuu hana habari na wamegushi sahihi yake,’’ alisema Lukuvi.
 
Waziri huyo wa Sera, Uratibu na Bunge alitaka mwongozo wa Mwenyekiti kama jambo hilo linaweza kufanywa na Wabunge, ndani ya Bunge kwa wabunge kugushi taarifa ambazo alisema nyingine na zinatisha.
 
Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alikiri kuwepo kwa tabia hiyo ndani ya ukumbi wa bunge ambayo imekuwa ikifanywa na baadhi yao na kamba inaonekana kuota mizizi.
 
“Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri, ni kweli kuna mtu amefanya hivyo na karatasi aliyoiandika ipo hapa, Kwa kweli siyo nzuri haionyeshi kama tupo serious (makini) na kazi,” alisema Simbachawene na kuisoma:

“Amemwandikia hivi, Mheshimiwa Joseph Selasini Mbunge, samahani nakuomba mara moja tuje tujadili suala moja muhimu ambalo ningependa kujua kutoka kwako. Ahsante. Mizengo Peter Pinda na sahihi”.
 
Simbachawene alisema Selasini alipokwenda kwa Waziri Mkuu alishindwa kusaidiwa kwa kuwa wakati huo Waziri Mkuu alikuwa makini kusikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika majumuisho yake.
 
Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema uongozi wa Bunge utafanya kila liwezekanalo kubaini ni nani mwenye tabia hiyo na kwamba ili kukomesha vitendo hivyo.
 

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #37 2011-07-28 23:08
Kama ni messages wasiliana na kampuni za simu kumjua mhusika wala haichukui muda. Tulisajili simu kwa madhumuni gani kama hata hili limeshindikana tunabaki kulalamika tu. Wananchi tupewe taarifa tuwajue hao wabunge ambao simu zao zimetumika kufanya mambo ya kitoto ili uchaguzi ujao tuwape dawa yao.
Quote
 
 
0 #36 2011-07-28 19:38
Quoting MSEMA KWELI:
WALA SISHANGAI HATA KIDOGO, WATOTO WENGI WALEVI,WASANII WA KIZAZI KIPYA WALIOGOMBANA NA AFANDE SELE KWA AJILI YA TUZO YA MUZIKI,WAHU.NI, WATOTO AMBAO NDIO MARA YAO YA KWANZA KUINGIA BUNGENI. SIONI LA AJABU KUFOJI SAHIHI YA MUHESHIMIWA KWA KUWA WALIFOJI VYETI NA HATA TAALUMA ZAO MUSHIKELI.
NA NDIO KWANZA 2011 MBONA TUTASHUHUDIA MENGI SANA HADI 2015?
HUU NI MWANZO TUU. HAIWEZEKANI UKAWACHAGUA WANAUME WAVAA HERENI KISHA UTEGEMEE BUNGE LENYE HOJA.

Kweli upo sahihi kidogo, maana nakumbuka kuna orodha ya viongozi wa CCM wenye degree feki. Pia kuna mwenyekiti wa UVCCM alitemeshwa kwa kufoji muda wa kuzaliwa na sasa ni mbunge.
Kuhusu kuvaa heleni, soma history ya Tanzania uone jinsi makabila fulani, wanaume walifanya hivyo. Tunaambiwa "history repeats itself" sawa na Dr. Nchimbi kuwa na Afro
Quote
 
 
0 #35 2011-07-28 16:54
Haya sasa wabunge wazima wameanza michezo ya watoto wa shule ya msingi embu kuweni watu wazima jamani nyie ndio kioo cha jamii kama nyie mnafanya hivi jee sisi wapiga kura wenu tufanyajeeeeeee eeeeee?
Quote
 
 
0 #34 2011-07-28 16:42
Waziri Lukuvi na Mwenyekiti wa Bunge wanakiri kuwapo kwa mchezo huo mchafu na bado wanasema 'kamchezo haka kameanza kuzoeleka'. Hii inamaana ni wazembe, toka walivyoanza kujua mbona hawakuchukua hatua mapema? Au kwa sababu njama zao (CCM)zimegundul ika za kutaka kuwaghilibu Wabunge wa upinzani kutoibana Serikali?
Quote
 
 
0 #33 2011-07-28 15:19
Ni bora hilo bunge liaahirishwe sioni kama kuna cha maana hapo! Na hizo posho zenu ziende zikafanye mambo mengine ya maendeleo. Huyo ni mbunge eti watu wanemchagua wanasubiri awawakikilshe vyema bungeni! Hana tofauti na mwanafunzi wa form two kwani wengi wao wapo kwenye rika bovu (foolish age. Hata kama wewe mbunge uliyefanya huo u j inga ni mbunge wa kuteuliwa bado una hadhi na unastaili kuheshimiwa kama mbunge. JIHESHIMUNI ILI MUHESHIMIWE. Nendeni shule mkajiendeleze kwa wengi wenu bado elimu ni duni! Hamjui nini maana ya kuwa kiongozi!
Quote
 
 
0 #32 2011-07-28 15:11
Tunaomba waziri mkuu Pinda atumie watalaam wake kujia maandishi ni ya nani ili wachuliwe hatua kali kwani kama mbunge anafanya mambo kama haya maake ukimkabithi majukumu atafanya ubadilifu, rushwa, ufisadi na kuandika barua kama za David Jairo ambaye alikuwa anatumia nembo ya Ikulu kwa usoefu wake ugushi barua za kuchangisha fedha za kutoa rushwa kwa wabunge. Kama hakuna watalaam tumia Scotalnd Yard ya UK, ili ijulikane kabisa kuwa baada ya miaka hamsini ya uhuru tunashindwa kufanya kazi ndogo kama hizo wakati India au Pakistani wametupita kwa miaka 10 tu tangu wapate uhuru wanarusha satellites angani na kutengeneza atomic bombs.
Quote
 
 
+1 #31 2011-07-28 13:57
utoto watu wazeeeee hao??? wajifunze kuwa makini na kazi bwana tumewachagua wanapaswa kutekeleza yale tulio watuma na sio mambo ya kitoto sehemu ya kazi, kama wanataka cheza wakacheze na wake zao nyumbani au watoto wao.. hapo ni sehemu ya kazi watambue hivyo. na huyo mtu akipatikana achukuliwe hatua ya kisheria kwani kughushi sahihi ya Mr. pinda ( au ya mtu ni kosa kubwa)
Quote
 
 
0 #30 2011-07-28 13:37
Hadhi y bunge letu imeshuka. wabunge wa ccm hawajui watendalo, hii ni aibu.
Quote
 
 
+1 #29 2011-07-28 13:30
wapelekeni mahakamani hao wabunge wenu wa ccm km sheria n msumeno ila wangekuwa wapinzani hata mimi ningeomba mwongozo toka kwa spika km ilivyo kawaida yenu ya kushabikia u[NENO BAYA] na kuacha ku suport mambo ya maendeleo na wananchi kwa ujumla.
mwisho wenu umefka.
Quote
 
 
0 #28 2011-07-28 13:03
Hivi kweli sio tunawabunge kweli?????????????????????mbona wanafanya mambo ya kitoto
Quote
 
 
+1 #27 2011-07-28 12:55
teknologia ytu ni fupi sana haiwezikani bungeni kokote duniani kitendo kama hiki kifanyike ni aibu sana hata nchi nyingine kusikia jambo hili,alama za vidole ni muhimu kwa kila mtu anae ingia bungeni hivyo ni rahisi sana kumjua mualifu JAH BLAZ TZ AMEN
Quote
 
 
+1 #26 2011-07-28 12:55
wabunge wanatuwakilisha sisi..na pia wanawakilisha vijitabia vyetu vya mtaani..
Quote
 
 
0 #25 2011-07-28 12:53
Bila kumsahau Mh. Selasini nae anapokea maoni yenu hapa tathmini.com/.../... kuhusu utendaji wake wa kazi bungeni
Quote
 
 
+1 #24 2011-07-28 12:52
yaani kama wako shuleni, ndio shida ya kuchagua viongozi kwa mkumbo,jazba bila kufikiria na bado. wala hakuna hata mbunge mmoja sio wa upinzani wala wa chama tawala anayejali shida zetu ndio maana wanafikia hatua ya kufanya u[NENO BAYA] kama huo, mbunge? kufoji sahihi? yaani ni utoto kwisha kazi mnatia aibu, lakini mbona ni bunge hili tu ndio kuna vituko vya ajabu ajabu? kuna nini ndani yake.
Quote
 
 
0 #23 2011-07-28 12:52
Mh. Simbachawene anapokea maoni na ushauri wenu hapa tathmini.com/.../... kuhusu tendaji wake wa kazi bungeni
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner