MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Kujivua gamba sasa mwisho Septemba
BOOKMARK THIS PAGE
Kujivua gamba sasa mwisho Septemba  Send to a friend
Monday, 01 August 2011 21:03

Habel Chidawali, Dodoma
KAMATI Kuu ya CCM (CC) imewataka wanachama wake wengine wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi kuwajibika kabla ya Septemba mwaka huu, vinginevyo wataumbuka.

Onyo hilo la CC linakuja baada ya kupitia kwa siku 90 zilizotangazwa Aprili mwaka huu na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), ikiwataka watuhumiwa hao kujiondoa wenyewe kabla ya siku hizo vinginevyo wataondolewa.

Hadi sasa, ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye amejizulu hatua ambayo imeridhiwa na kupongezwa na CC.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema chama kimeridhia uamuzi wa kujihudhulu kwa Rostam na kuongeza kwamba hiyo ni sehemu ya uamuzi wa chama ambao wengi wanatakiwa kuufuata.

“Ni heri kupoteza jimbo au kata halafu tukarudi kwenye uchaguzi maana ndiyo njia pakee ya kukisafisha CCM kuliko kuendelea kung’ang’ania wachafu kwenye chama chetu.”

Alisema CCM hakioni tabu ya kurudi kwenye mchakato wa uchaguzi katika majimbo na kata katika eneo lolote kama itabidi kwani wananchi wanatambua nini mustakabali wa chama chao na kutamba: “Tukirudi huko bado tutashinda.”

“Nasisitiza hata ninyi nendeni mkasome katika Biblia imeandikwa kuwa, kama kidole kitakukosesha amani ni bora kukikata ili mwili uwe salama kuliko kukiacha mwisho wa siku ikawa balaa. Hivyo nasi tuko tayari kuwatimulia mbali hao wanaotuhumiwa kwa mambo mbalimbali ili chama kibaki salama.’’

Nape alisema CCM kiko tayari kuwatimua muda wowote watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi na mambo mengine lakini, akatahadharisha kuwa hakiwezi kufanya hivyo kwa sasa bali kinasubiri kikao cha Nec ambacho kitakutana Septemba mwaka huu.

Alisema chama siku zote kimekuwa kikisitiza suala la maadili na kuongeza kwamba hiyo ni ajenda ya kudumu kwa kila kiongozi pamoja na wanachama wake.Alisema CCM hakipo tayari kuwaacha wanachama wake ambao wanalalamikiwa waendelee kutamba na kuonya kwamba kiama chao kinakuja Septemba Nec itakapokutana.

“Samaki ana nguvu akiwa ndani ya maji tu, ukimtoa hakuna kitu tena wala hana ujanja na hivyo hata hawa wanatusumbua wakiwa ndani ya chama lakini tukiwatimua hawana mahali pa kuegemea,’’ alisema na kuongeza:
“Hakuna maarufu kuliko chama. Wanaotaka tuwatimue tutafanya hivyo na chama kitabaki imara hivyo hivyo na huenda kikawa imara zaidi maana tunalenga kujijenga chama chetu wakati wote.’’

Malalamiko ya ziara za mikoani
Akijibu hoja kuhusu malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya wanaCCM na viongozi kuwa sekretaieti ya chama hicho imekuwa ikifanya mambo ambayo hayakuamuliwa kwenye vikao husika, Nape alisema huo ni uongo.Alisema CC imepongeza kazi nzuri inayofanywa na sekretarieti ikiwa ni pamoja na mikutano hiyo ambayo imekuwa ikifanya kwenye mikoa mbalimbali na kusema: “Kamati imeagiza wakaze buti bila ya kuyumba.”

Nape alisema kama sekretarieti ingekuwa hairidhishwi na mikutano inayofanyika sehemu mbalimbali isingekubali kuwapongeza na badala yake ingewazuia... “Kitendo cha kutaka mikutano iongezeke zaidi ni ishara ya kazi nzuri iliyofanywa.”

Mchakato wa uchaguzi Igunga
Nape alisema jambo jingine ambalo lilijadiliwa na CC ni pamoja na kuweka ratiba ya mchakato wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa ajili ya kumpata mgombea ubunge katika Jimbo la Igunga kupitia CCM.“Tulichokubaliana ni kwamba kule Igunga mchakato wote tutawachia wenyewe watu wa Mkoa wa Tabora pamoja na Wilaya ya Igunga lakini, sisi taifa tutakwenda kuongeza nguvu ya ushindi na tuna imani tutashirikiana na Rostam katika kufanikisha ushindi huo kwa kuwa alisema atabaki kuwa mwanachama wetu mwaminifu,” alifafanua Nape.

Umeme na migogoro ya ardhi

Katibu huyo mwenezi wa CCM alisema suala la migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini lilijadiliwa kwa kina na CC ambayo iliiagiza Serikali kushughulikia migogoro hiyo ikiwa ni pamoja na ile ya sehemu za migodini na kuimaliza kwa muda muafaka.

Alisema Kamati Kuu imeagiza kuwa migogoro hiyo ishughulikiwe katika ngazi ya mikoa kabla ya kupelekwa ngazi ya Taifa.Aidha, CC imeitaka Serikali kuja na majibu ya uhakika siku itakaporudisha tena bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kukidhi mahitaji ya Watanzania na kufufua matumaini yao yaliyoanza kutoweka.

Kamati ya maadili.
Kamati Kuu imefanya uteuzi wa wajumbe wa Kamati ya Maadili kwa kuwateua Abdulrahman Kinana na Pindi Chana. Wajumbe wengine kutoka Zanzibar hawakutaja mara moja.
 


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
+1 #30 2011-08-03 09:11
umakini wa ccm umepotea, hawana dira ndiyo maana hata sababu za umaskini hawazielewi, ni wakati wa mabadiliko ya mfumo mzima wa uongozi wa nchi
Quote
 
 
0 #29 2011-08-02 19:16
Naape Huna hoja mpya bali ni yale yale Viongozi wa CCM kuanzia mwenyekiti ,makamo mwenyekiti,kati bu mkuu
wanawaogopa Mafisadi kina Chenge na Lowassa,kwa sababu siri zao zajulikana na hao mafisadi, kwanini CCM sasa inangojea mwezi september????? hii ni danganya toto.enzi ya mwalimu kina Chenge wangekuwa jela.
Quote
 
 
-1 #28 2011-08-02 17:35
Haya yafanyikao sasa ndani ya chama yatatupeleka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Imeonesha kuna baadhi ya watu wanaunga mkono zambi za akina Lowassa, Rostam na Chenge na wapo watu wanalaani maovu yao. Nape anatumiwa kuzidi kuupotosha Umma. Huwezi kuzungumza kuwa tarehe ya kujivua Gamba imesogezwa mbele! Nape Tafadhali, usitumie elimu ya Kivukoni ya kudanganya umma wakati huu wa demokrasia. Nakuhakikishia utachukiwa na watu kuliko vile makamba alivyo bolonga.
Quote
 
 
+1 #27 2011-08-02 17:01
Hakuna asiye gamba ndani ya CCM the whole system is Rotten!Hii ndo sababu wanaogopana na Lowassa alisema..."wamwage ... na yeye atamwaga....."Hiyo kauli si nyepesi ina mambo mazito!1Tufikirie jinsi ya kutatua matatizo yetu ya ugumu wa maisha ulioletwa na mipango na sera mbovu za chama gamba!!Puuuu!
Quote
 
 
+1 #26 2011-08-02 16:22
MHH? JAMANI HIVI HUYO MZEE WA VIJISENTI AACHIE NGAZI KAMA ALIWEZA KUITA PESA ZA TANZANIA VIJISENT BASI AKATE WINGA ANADHARAU HATA PESA YETU YA MKULIMA MTU MWENYEWE HATA KWAO HAKUNA NYUMBA YA MAANA
Quote
 
 
-1 #25 2011-08-02 15:29
WASAFI WALISHAONDOKA CCM NA WALIONDOKA WAKIWA MASIKINI KWELI ATA LEO NI MASIKINI WAANGALIE WAASISI WENYEWE ANZA NA NYERERE, WARIOBA, BUTIKU NA WENGINEO WANAISHI MAISHA YA KAWAIDA TU, LAKINI WAANGALIE WA SASA NI VIBOPA WA KUTISHA WANAISHI KAMA WAPO PEPONI, NANI ATAKUBALI YAANI WENGINE WAJIVUE GAMBA WENGINE WAENDELEE KUVAA HAYO MAGAMBA, NDO MAANA MZEE WA VIJISENTI AMEGOMA KWANI KAMA NI MAGAMBA NI WOTE CHAMA HAKITABAKI NA MTU LABDA WALE WENZANGU NA MIMI WANAOSUBIRI POMBE NA KHANGA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI, WANA IGUNGA JIANDAENI KHANGA HIZO ZINAKUJA NDO MAANA WANASEMA LAZIMA WAMTUMIE R. A. KWANI YEYE NDIE MAHILI WA KUGAWA HIVYO VITU NDO MAANA ALIKUWA HANA MPINZANI, NAPE NENDA KAJIUNGE NA UPINZANI HAKUNA UTAKACHOFANYA HAPO HAO NI VIGOGO WALISHABOBEA
Quote
 
 
-1 #24 2011-08-02 15:15
NINYI FANYENI MSIHALA TU SI MNAONA SYRIA ILIVYO SASA.SASA NINYI ENDELEENI KUWAKUMBATIA HAO MAFISADI.PAKINUKA HAPA KILA MTU ATAKATAA KUWA AMKUWACHAGUA PINDI TUTAKAPOAMUA KUWATOA MADARAKANI KWA NGUVU YA UMMA ATA KAMA MNAWAPENDA HUKO MAJIMBONI KWENU.
Quote
 
 
-1 #23 2011-08-02 15:14
Magamba ya kujivua ni unafiki tu, CCM washatuchosha, achana nao, tafuta pa kukimbilia.
Quote
 
 
0 #22 2011-08-02 15:01
jamani mwacheni huyo k.u.m.a aneitwa nape kwa bahati mbaya yeye ni mtu aliye toka kwenye familia za kimaskini sana so yeye hayupo chama chochote ila anahaingaikia tu apate hela ya kula so ni shida zake zinamfanya awe hivyo.na sio mtu wa kumlaumu
Quote
 
 
-3 #21 2011-08-02 12:52
Quoting TARA:
Nape unahangaika bure tu! LOWWASA bado anakubalika na hata mkipiga chini sisi MONDULI tutamchagua tena!

Ajivue GAMBA kitu gani??????????? Kama kweli LOWWASA anahusika na richmond mbona hamumpeki mahakamani? Inamaana NEC imekuwa mahakama?


Haya ni majungu ya Nape na Sitta wake wanafanya kila njia ya kumfedhehesha na kumzalilisha Lowassa lakini wajue sisi wananchi tunaona. Hakuna mtu mbovu kama Sitta na hana sifa ya kuongoza nchi, ni mnafiki na mchonganishi wa hali ya juu. Mhe. Kikwete amekuwa msikilizaji na mtazamaji akishuhudia uhuni huu wa CCJ. NAPE achana na Lowassa na fanya kazi ya kujenga chama au urudi CCJ.
Quote
 
 
-4 #20 2011-08-02 12:44
Nape ni double face, double mouth and double ideology; namsihi dogo huyu aende kuimarisha CCJ. iweje anatelekeza chama chake anang'ang'ania chama cha wengine? Ajabu hii!
Quote
 
 
0 #19 2011-08-02 12:36
Nafikir NAPE hana uelewa wakutosha kuweza kupambanua na kuchangamanua mambo. Akumbuke kwamba bosi wake JK aliwanad hao anaowasema ni wachafu(mafisad i)kwenye kampen za uchaguzi mwakw jana akisema ni watu safi. Nape acha siasa za ushabiki na uzandiki. Mnatukanganya ss wana ccm
Quote
 
 
-1 #18 2011-08-02 12:21
HIVI HUYU JAMAA ANADHANI SEPTEMBER MBALI TUTAFANYA SUBIRA.HIVI HANA MAANA HADI KIKWETE MAANA SIJAMWONA AMBAYE MSAFI PALE AMA WADAU KUNA MNAOWAONA WASAFI
Quote
 
 
0 #17 2011-08-02 12:08
Quoting chibwaye:
Aaah CCM Mmetuchosha kabisa maana mnatuimbia ngonjera zisizo na mwisho fanyeni mambo yanayo eleweka sio sound kila siku. na siku mkitoka mjue hamta rudi tena

@Chibwaye, wewe bado unasikiliza hizi ngonjera sisi wengine tumaeshaacha, sasa tunatafuta msitakabali wa nchi yetu kupitia chama kingine! CCM wamepoteza uhalali wa kuingoza nchi yetu na nilazima tuwamwage, bila ajizi.
Quote
 
 
+3 #16 2011-08-02 10:25
Suala la kujivua gamba si la muhimu sana kama halitaenda sambamba na kurudisha mali na rasilimali za watanzania zilizoporwa na hao wajivuao gamba.Ni vizuri chama kinachotawala kijitafakari na kukubali kwamba sasa watanzania wengi wameelimika na hivyo kuwadanganya tena au kuwalazimisha chama wakipende kunaweza zua tafrani.Ushauri wangu ni kwamba,chama sasa kijipange upya,hata ikibidi kiwe chama cha upinzani hapo baadae.Hakuna chama kimeumbwa kutawala Tanzania milele.Hata Japan chama kilichotawala miaka hamsini kimeanguka.La msingi tukubali demokrasia itawale,hata kama mtaanguka kwenye chaguzi zijazo,mnaweza kujipanga upya na kurudi mkiwa wapya.Kujivua gamba kwa sasa hakuwezekani maana wengi walioserikalini wanaguswa na hilo.Chama tawala kubali sasa kupumzika.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner