Sunday, November 11, 2012

Chama cha makahaba chasajiliwa rasmiRais wa Malawi,Joyce Banda

Rais wa Malawi,Joyce Banda 

By Mwandishi Wetu

Malawi
ZAIDI ya makahaba 2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayoyapata na kuboresha mazingira ya afya, baada ya kuzindua rasmi chama cha kuwatetea juzi.

Kundi hilo linaundwa na vyama visivyo vya kiserikali vya ndani na nje ya nchi hiyo, ikiwa ni la kwanza kutambuliwa rasmi na kupewa usajili katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo biashara ya ukahaba inaharamishwa.

“Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri za kulinda afya zenu na afya ya uzazi bila kipingamizi,” alisema mwanasheria wa haki za binadamu, Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi la wateja wake wapatao 50 ambao ni makahaba.
Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo pia huambatana na kutozwa faini.

Miaka mitatu iliyopita, makahaba 14 walikamatwa na Polisi na kulazimishw akupimwa Virusi vua Ukimwi (VVU) na wote kukutwa wakiwa wameathirika, ambapo walishtakiwa mahakamani kwa kufanya biashara ya ngono huku wakijua kuwa wana maradhi hayo ya kuambikiza, ambapo walichajiwa Dola7 kila mmoja na kuachiwa huru.
Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa katika mahakama kuu.

Wataalamu wa afya nchini humo wanasema maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa makahaba hao yanafikia asilimia 70. Mawakili wao wanasema kuw awanatumiani umoja wao utawasaidia pia katika kuwaelimisha kuepuka maambukizi hayo.

-->