
| CCM Arumeru waanza kuvurugana | Send to a friend |
| Tuesday, 21 February 2012 20:52 |
Moses Mashalla, Mussa Juma, ArumeruSIKU moja baada ya wanachama wa CCM, Jimbo la Arumeru Mashariki kumpendekeza Sioi Sumari kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo ujao, baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilayani humo, wamepinga uteuzi huo wakidai kuwa uchaguzi uligubikwa na mizengwe. Juzi, mkutano Mkuu wa Jimbo hilo ulimchagua Sioi, mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari kwa kura 361 akifuatiwa na William Sarakikya aliyepata kura 259, Elishilia Kaaya (176), Elirehema Kaaya (205), Anthony Musari (22) na Moses Urio (11). Lakini jana, baadhi ya wajumbe hao wa UVCCM wakiongozwa na Mjumbe wa Baraza la Umoja Mkoani wa Arusha, Kennedy Mpumilwa walidai kwamba uchaguzi huo ni batili kwa kuwa ulitawaliwa na misingi ya rushwa. Mpumilwa alidai kwamba uchaguzi huo ulijaa rushwa kila kona. Hata hivyo, hakuweka bayana kama walihongwa ili wamchague nani kati ya wagombea hao sita. Alidai kwamba kigogo mmoja wa UVCCM ngazi ya mkoa aliyeongozana na kada mmoja wa jumuiya hiyo, walikuwa ndani ya gari karibu na eneo la uchaguzi wakigawa rushwa kwa wajumbe. “Huu uchaguzi haufai kabisa baadhi ya wajumbe walihongwa. Ilikuwa ikitolewa 150,000 kwa kila mjumbe atakayekubali. Sasa hii CCM gani kama uteuzi tu hadi ufuate rushwa,” alidai Mpumilwa. Alisema kwa jinsi mchakato wa uchaguzi huo ulivyofanyika, ni dhahiri chama hicho kimeingia katika mpasuko mkubwa ambao kama usipoangaliwa kwa makini, unaweza kukiathiri. Mpumilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, alisema baadhi ya wanachama wa umoja huo wilayani humo wamechukizwa na mambo yaliyojitokeza katika uchaguzi huo huku wengine wakitishia kuhamia upinzani wakati wowote. “Nakwambia vijana wamechukizwa kabisa na kilichofanyika katika mchakato wa uchaguzi, sasa wengine wametishia kwenda upinzani wakati wowote,” alieleza Mpumilwa. Aliutaka uongozi wa CCM taifa kuingilia kati suala hilo na kulipa uzito akidai kwamba lisipoangaliwa huenda likazua mpasuko mkubwa ndani ya CCM wilayani humo na kusababisha kulipoteza jimbo hilo wakati wa uchaguzi. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi ya wa CCM Mkoa wa Arusha, Loota Sanare alisema hadi jana hakuna mgombea yoyote kati ya hao sita ambaye alikuwa amepinga matokeo ya uchaguzi huo. Alisema ushindi wa Sumari katika uchaguzi wa ngazi ya jimbo, siyo mwisho wa uteuzi na kwamba kuna vikao vya kamati ya siasa ya Wilaya ya Arumeru na baadaye vikao vya mkoa na Kamati Kuu (CC) ya CCM Taifa, ambayo ndiyo itakayomtangaza mgombea. “Tumezipokea hisia za wana-CCM, Sioi ameongoza ni nafasi nzuri kwake lakini siyo mwisho wa uteuzi wake. Bado kuna mchakato mrefu mbele yake,” alisema Sanare. Vigogo watimua mbio Katika hatua nyingine, kushindwa kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) wa Mkoa wa Arusha, Elishilia Kaaya katika kura hizo za maoni juzi, kuliibua huzuni kubwa kwa vigogo wa chama hicho huku baadhi yao wakiondoka ukumbini kabla ya matokeo. Kaaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), alikuwa anaungwa mkono na kundi la viongozi wa juu wa CCM na Serikali ambao wamejipambanua kuwa wanapambana na vitendo vya ufisadi. Mjumbe huyo wa Nec alishika nafasi ya nne baada ya kupata kura 176, nyuma ya Sumari, Sarakikya na Elirehema Kaaya. Dalili za kubwagwa kwa kigogo huyo, zilianza kuonekana mapema nje ya ukumbi ambako baadhi ya madiwani na wana-CCM vijana, walikuwa wakiendesha kampeni nzito ya kutaka mgombea kijana ambaye ataweza kupambana na mgombea machachari wa Chadema, Joshua Nasari endapo atapitishwa na chama chake. Pia, katika ukumbi wa kupigia kura, mara baada ya wagombea wote sita kujieleza, Sumari alikuwa akishangiliwa zaidi na kundi la vijana hali ambayo iliwasukuma baadhi ya vigogo kuanza kuondoka mapema ukumbini. Chadema wachekelea Akizungumzia uchaguzi wa jana, Nasari alisema amefurahishwa na uamuzi CCM kumpitisha Sumari kugombea akidai kwamba sasa anaamini kuwa ushindi wa chama chake utajulikana saa nne asubuhi Aprili Mosi. “Nimesikia Sioi kaongoza wamlete tu huyo tena nilikuwa namtaka sana. Chadema tulikuwa hatuna hofu na mgombea yoyote na sasa tuna uhakika wa kushinda saa nne asubuhi,” alitamba Nasari. Nasari alichukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo juzi. Katika uchaguzi wa mwaka 2010, mgombea huyo kijana aligombea pia kwa tiketi ya Chadema na kushindwa na Baba yake Sioi. |
| Last Updated on Wednesday, 22 February 2012 11:36 |



Moses Mashalla, Mussa Juma, Arumeru












Comments
isitoshe kila panapo tumika pesa basi ukweli hunyamaza .kwamaana pesa huweza kufanya uongo ukawa kweli na kweli ikawa uongo .sioi kama kweli alipita kwa rushwa basi bado wananchi wana nafasi ya
kumuondo kupita kura maana mtuanapotumia njia haramu ili kupata uongozi ni wazi kwamba hata kuwa na uchungu na kero za wananchi bali kujinufaisha mwenyewe
tuiji ulize kuwa nilazima mtu awe mbunge hata kwanjia zisizo halali .
1. Tz ni ndogo tuelemishe wachache wanaoweza soma mitandao hatua kabambe za kuwaelemisha watu 10 tu na hao kumi kila mmoja aelemishe 10 tena mara 10 days tuna kundi la Ushindi kwa CHADEMA. Kmbuka mimi na wewe hatuna ridhaa ya kwenda Meru kupiga kura ila tutoe elimu by any means.
2. Vijana kanisani, misikitini ni mahali pa kushauriana kubadilika kiroho na Kimwili why tusihauriane kumchagua kiongozi safi na atakayetutetea. Hivi huyo Sioi ametumia rushwa kubwa hivyo atasema nini bungeni in 5 years kama sio kuongozwa kama boya
Shangwe hizo zimetokana na Sioi Sumari, mtoto wa aliekua mbunge wa jimbo hilo kuingia katika kinyangayiro cha kuwania nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi na baba yake aliefariki dunia mapema mwezi huu. Sumari alipata kura 361 sawasawa na asilimia 34.91% na kuwashinda wenzake watano katika kura za maoni kupitia Chama cha Mapinduzi zilizopigwa jana na wajumbe wapatao elfu moja na thelathini na nne (1034) waliotokana na wajumbe wa halmashauri ya Arumeru.
Aliemfuata Sumari ni William Sarakikya alipata kura 259 au asilimia 25%, Elirehema Kaaya kura 205 au asilimia 19.82%, Elishilia Kaaya kura 176 au asilimia 17.02%, Antony Musani kura 22 au asilimia 2.12% na Rishiankira Urio kura 11 au asilimia 1.06%.
Ushindi wa kijana huyu umepokelewa kwa mshangao mkubwa na kuzua gumzo na maswali mengi katika makundi tofauti kutoka ndani na nje ya chama chake, wazee, wakina mama na vijana kutokana na mazingira yaliopelekea ushindi huo. Huku upande wa upinzani ushindi ukianza kushangilia ushindi kwa kuona uteuzi huo utahakikisha chama chao kitachukua jimbo kwenye uchaguzi mkuu kama waandishi wetu wanavyotutaarif u kutoka Arumeru.
Baada ya matokeo hayo kutangazwa, wagombea wenza walionekana kuondoka kwa hasira bila kumpongeza Sioi na kuacha kikao kabla ya kufungwa rasmi huku wakilalamikia TAKUKURU na uongozi kushindwa au kulipa kisogo swala la rushwa lilikiwa linafanyika hadharani bila hatua kuchukuliwa.
Nje ya ukumbi vijana wakereketwa waliokua wakisubiri matokeo kwa hamu kubwa walionyesha kushtuka na kukasirishwaa kwa matokeo yalipatikana wakisema wanahamia CHADEMA na kuanza kuimba “CHADEMA, CHADEMA!”.
Yaliyo washangaza watu ni Sioi kuwa mgeni kabisa katika siasa, bila wasifu wa uongozi, utumishi au uzoefu katika chama, mapungufu yalionekana alipokua akijinadi; hata kuleta walakini wa uanachama wake. Inasemekana hali hiyo ya ugeni ni pamoja na kwamba kijana huyo hana mizizi ya kutosha ikiwa na kutokua na ufahamu yakinifu au uhusiano au upendo wa kweli na Arumeru kuweza kuiendeleza.
Lingine ni la kuwania kukrithi kiti cha marehemu baba yake ambalo wananchi wamekuwa wakipinga vikali umangi kwani Arumeru inayo hazina kubwa ya viongozi. Dhana kwamba Sioi amepachikwa na Mhe. Lowassa kama vile Marehemu J. Sumari imetanda na watu wakiwa na hasira iweje Lowassa awachagulie na kusimika viongozi Arumeru kana kwamba wameru ni watoto na hawawezi kujifanyia maamuzi wenyewe na mpaka lini?
Kutoa suala la kupeleka na kufanya jitihada ya kujenga halmashauri ya Arumeru jimboni, marehemu sumari hakuwa na mengine yaliyowafurahis ha Wananchi na wengine kudiriki hata kusema aliwaacha na mengi zaidi ya kuwakwaza. Kwa mantiki hiyo wanasema isinge kuwa rahisi kumpa mtoto mtu dhamana ya kudendeleza mapungufu ya babae kama sio kwa nguvu ya ziada ya pesa kwani maelezo yake hayakua ya ajabu na wala hakuwa na haiba wala mvuto wa ziada.
Inasemekana kwamba Lowasa aliulizwa mapema na wazee tofauti wa Arumeru kuhusu ushiriki wa Sioi akakana kumsaidia hata kusema kuwa hana baraka zake kwani amekaidi ushauri wake wa kusubiri. Kwa kile kinachoonekana kudhihirisha hilo, kipindi chote cha mchakato Mhe. Lowasa na familia yake ikiwa ni pamoja na mke wa Sioi mwenyewe, Pamela Lowasa hawakuonekana hadharani kumuunga mkono au kujihusisha katika juhudi zake. Hii ni pamoja na kwamba inasemekana Pamela alikua Meru kuhudhuria ibada ya shukurani ya kumuombea marehemu Sumari Jumapili iliyopita.
Baada ya mkutano, tuhuma za wajumbe kugaiwa bahasha na anaesemekana kuwa ni mwenyekiti wa vijana wa Arusha James Millya (ambae ni shabiki mkubwa wa Lowasa) ili kushawishi Sioi apigiwe kura na hatimae ushindi wake wa kushangaza jana, hali ya hewa ilichafuka na chuki kuibuka juu ya Mhe. Lowasa baada ya wazee kubaini mkono wake katika kumpachika mkwe wake na kutambua kukana kwake kulikua ni mkakati kiini macho cha kuwapumbaza na kuwadanganya wazee na umma wa Arumeru kwamba hahusiki ili atimize azma yake ya kumuweka mtu wake.
Inasemekana James Millya, Robert na Fred Lowassa (ingawa Fred Lowassa alikua akijificha) ndio walileta pesa za kuwapa wapiga kura kwenye buti ya gari ya Millya Benzi ya rangi ya fedha. (tinted) Gari hilo lilipaki kwenye baa maarufu ijulikanayo kama Transit ya Leganga, Usa River. Sioi Nanyaro mfanyabiashara wa matofali wa Tengeru wakishirikiana na Mica Mwenyemali Isangya ambae alikua Katibu wa marehemu Sumari walikua wakifanya zoezi la kuwaita na kwenda kuwagaiya wajumbe huo mlungula ndani na nje ya ukumbi.
Zoezi hili lilikua likifanyika pamoja na TAKUKURU na vyombo vingine vya usalama kusema wameongeza nguvu kazi na umakini ili rushwa isitumike. Mbinu hii inasemekana ni chapa ya Lowassa na ilitumika tena katika kumpitisha mbunge wa viti maalum Mhe. Namelok Sokoine kwenye chaguzi zilizopita.
Pamoja na nguvu ya pesa kutumika inasemekana kuwa Sioi alipata ushirikiano mkubwa na nasaha kutoka kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika ngazi ya Wilaya na hata Mkoa. Siku Sioi alirudisha fomu yake ya uchaguzi alikaa takriban masaa matatu na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha ndugu Onesmo Nangole na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru Joseph Ole Saivoye (ambao ni watu wa karibu na MaLaigwanan wenza wa Lowasa na labda kwa niaba yake Lowasa) kwa kile kilichotafsiriw a kama semina ya kupigwa msasa kwani hakuna wagombea wengine waliopewa fursa hiyo maalum.
sisi atutamchagua sio.. chaguo letu ni Mr.Nassary