|
Mahakama yafuta hati ya kumkamata Chenge |
Send to a friend |
|
Wednesday, 29 September 2010 09:08 |
|
Ummy Muya
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Kinondoni imefuta hati yake ya kuruhusu kukamatwa kwa mwanasheria mkuu wa zamani, Andrew Chenge iliyotolewa juzi kutokana na mshtakiwa huyo kushindwa kutokea mahakamani.
Hakimu Sundi Fimbo alitoa hati hiyo juzi wakati Chenge, ambaye anatetea kiti chake cha ubunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki akiwa kwenye mkutano wa kampeni ambako alipigiwa debe na mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye kwa sasa yuko mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Lakini mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, David Mwafwimbo aliiambia Mwananchi jana kuwa mdhamini wa Chenge aliibuka juzi akiwa amechelewa na akamuomba hakimu afute hati hiyo na ombi lake likakubaliwa.
"Mdhamini wake anayeitwa Masanja alimrudisha Hakimu Fimbo mahakamani ili kuomba kufutwa kwa kibali cha kumkamata mshtakiwa... ingawa mdhamini huyo alifika mahakamani hapo akiwa amechelewa, alienda kumuomba hakimu afute hati hiyo na akakubaliwa" alisema Mwafwimbo.
Mwafwimbo alisema baada ya mdhamini huyo kufika, hakimu aliitisha tena jalada hilo na kuifuta amri hiyo ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo.
Chenge alitakiwa kuanza kujitetea jana katika kesi inayomkabili ya kuendesha gari kizembe na kufanya makosa mawili ya kusababisha vifo vya watu wawili na jingine la kuendesha gari bila bima halali.
Chenge anadaiwa kugonga pikipiki ya maguruduma matatu, maarufu kama Bajaj iliyowabeba wasichana wawili na kusababisha vifo vyao ambavyo kisheria huchukuliwa kama makosa mawili tofauti.
Kutokuwepo kwake kulimfanya Hakimu Fimbo kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 5. Lakini Zulfa Mfinanga na Herman Meza wanaripoti kutoka Shinyanga kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo lilikuwa halijapokea hati ya kumkamata.
Afisa upelelezi mkoani humo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi((SSP), Adam Nyakipande alikiri kusikia habari hiyo, lakini akasema walishindwa kuitekeleza kwa kuwa hawakupata kibali cha mahakama hiyo.
"Ninachoweza kusema ni kwamba sisi tunasubiri hati ya kumtia nguvuni... kwa ufupi bado hatujapewa kibali cha kumkamata lakini tukipata tutalifanyia kazi," alisema.
|
|
Last Updated on Wednesday, 29 September 2010 10:25 |
Comments
SIKU HIYO HATA WASIOONA HAWAHITAJI KUFUMBULIWA MACHO NDIPO WAIFANYIE KUFURU CCM!!!!!!!!!!!! !!!!!!
NAFASI YA PEKEE KWA TAWZ KUREJESHA HAKI NA UADILIFU, UKOMBOZI HALISI WA MTANZANIA, KUREJESHA HADHI YA MAHAKAMA KWA KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI KWA MAFISADI NI KUIPELEKA CHADEMA IKULU.
TUKIFANYA KOSA LA KUIRUDISHA CCM IKULU, TUTAKUWA WASHIRIKA WA MAFISADI KATIKA KULIANGAMIZA TAIFA LETU NA LAANA ITAKUWA JUU YETU.
LET'S SHOUT, "WE ARE THE LIBERATORS OF TANZANIA, AND WE SHALL LIBERATE IT BY VOTING IN DR. SLAA FOR PRESIDENT".
Uchakachuaji!
Uchunguzi unaendelea!
Upembuzi yakinifu!
Tathmini inafanyika!
kesi inaendelea!
Mkandarasi anatafutwa!
YOOOOTE Haya ni UCHAKACHUAJI NA BLAAAH BLAAAH za Mafisadi
Believe Me!
Justice Delayed is Justice Denied!!
WAO WANABEBANA sisi TUTAAMUA 31/10/2010
VIVA Dr Slaa