MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Bei ya umeme juu mwakani
BOOKMARK THIS PAGE
Bei ya umeme juu mwakani  Send to a friend
Monday, 20 December 2010 20:49

Nora Damian na Pilly Hashimu  
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imeruhusu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.5 kuanzia Januari Mosi mwakani.  

Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa ongezeko hilo la bei ni chini ya mapendekezo ya Tanesco kwa asilimia 16.1.  Kwa mujibu wa Masebu, Tanesco ilipendekeza umeme upande bei kwa asilimia 34.6, lakini, baada ya uchambuzi wa kina, mamlaka imekubali kuruhusu nyongeza ya asilimia 18.5 kwenye nishati hiyo. 

"Shirika hilo liliomba kupandisha bei ya umeme kwa miaka mitatu mfulululizo na kwa viwango tofauti kuanzia 2011 hadi 2013, lakini, tumeona kuwa kuna hoja za msingi ambazo haziwezi kutufanya tukubali ombi hilo," alisema.  

Masebu alibainisha kuwa Tanesco iliomba kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 34.6 mwaka 2011, asilimia 13.8 mwaka 2012 na asilimia 13.9 ifikapo mwaka 2013.  “Najua kwa uamuzi huu tutakuwa tumewaumiza watumiaji umeme na hatutakuwa tumewaridhisha Tanesco, lakini tumefanya hivyo kwa vigezo ili kufanya sekta iwe endelevu,”alisema Masebu.  Mkurugenzi huyo wa Ewura alisema kuwa ili shirika hilo liweze kujiendesha, linahitaji zaidi ya Sh 691bilioni na uchambuzi walioufanya umeonyesha kuwa ongezeko hilo jipya la bei ya umeme, linaweza kukidhi hitaji hilo.  

Alisema  pia wameondoa mfumo wa shirika hilo uliokuwa unawapa nafuu wafanyakazi wake kulipia garama za umeme na kuanzia sasa wafanyakazi hao watalipa gharama hizo kama watumiaji wengine.  “Si sahihi wao kulipa pungufu, lazima walipe kama  watumiaji wengine na wasipolipa hata kwenye mahesabu itaonekana,”alisema.  Hata hivyo, alisema watumiaji wadogo wa umeme wasiozidisha kilowati 50 kwa mwezi, wataendelea kusaidiwa na watumiaji umeme mkubwa. 

Kwa mujibu wa Ewura, bei ya zamani kwa watumiaji hao wa umeme, ilikuwa Sh 49, lakini bei mpya itakuwa Sh60.  Kwa upande wa watumiaji umeme mkubwa zaidi bei ya zamani ilikuwa Sh 2,303 na Tanesco waliomba ipandishwe hadi Sh 3,109, lakini bei iliyokubaliwa ni Sh 2,738 kwa kilowati moja.  

"Tumeamua kuruhusu ongezeko hilo na kama Tanesco wanadhani gharama zao za uendeshaji zinapanda kwa sababu ya ongezeko la gharama za mafuta ya kuzalishia umeme, wanaweza kujenga hoja na tukabadilisha bei ya mafuta pia," alisema Masebu.  Alisema ili kuhakikisha kwamba fedha zitakazopatikana hazitatumika vibaya, wameiagiza Tanesco kufungua akaunti maalumu kwa ajili ya kuboresha huduma ya umeme.  

"Akaunti hizo zitakuwa zikikaguliwa na Ewura kila baada ya miezi mitatu na fedha zitakazokusanywa zitasaidia pia kununulia umeme mkubwa kwa wazalishaji wengine wa umeme," alisema Masebu na kuongeza:  “Tumewaagiza baada ya mwaka mmoja watueleze mabadiliko haya ya bei yameleta mafanikio gani katika kupunguza hasara.”  Masebu alisema pia kuwa wameiagiza Tanesco ndani ya siku 30 tangu kuanza kwa mabadiliko hayo ya bei, kuwapelekea mkataba ili kujiridhisha kama hautakuwa na madhara kwa watumiaji wa nishati hiyo.  

Mkurugenzi wa umeme katika mamlaka hiyo, Pius Mbawala aliitaka Tanesco kuangalia mifumo ya manunuzi ya vifaa ili kupunguza garama za kuunganisha umeme kwani garama kubwa ni kikwazo mojawapo cha watu kuunganisha umeme.  Alisema pia wameliagiza shirika hilo hadi kufikia mwaka 2011 wawe wameunganisha wateja wapya zaidi ya 100,000, kuwa na idadi ya wafanyakazi inayotosheleza na kuhakikisha umeme unarudishwa mapema baada ya kukatika.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #16 2010-12-22 08:56
Ni kweli maisha ya mtanzania yanakuwa magumu kila siku lakini mi nadhani TANESCO kama shirika linalojiendesha kibiashara kutokana na kwamba halijawa shirika la huduma kwa jamii tena kama ilivyokuwa zamani wanapaswa kufanya ongezeko hili ili kunusuru hali yake mbaya ya kiuchumi na kuendana na gharama halisi za uendeshaji wa shirika.kwani ni kweli mafuta yanapanda kila siku, gharama za mitambo na usimamizi.
Mi naamini wa kulaumiwa ni serikali ambayo ndio yenye jukumu la kuelewa kuwa TANESCO si taasisi ya watu fulani bali ni shirika lililopewa dhamana na umma kuhudumia wananchi.sasa serikari inapolitelekeza shirika hili na kuliacha lijiendeshe kiushindani ni lazima gharama zitapanda kulingana na hali halisi ya uchumi wenyewe..serikali ya Tanzania imelichakachua shirika hili kama mpira usio kuwa na mwenyewe, wamelifilisi na kulibakiza kama skeleton(mifupa tupu) halafu litajiendeshaje ktk uchumi wa leo wa Tanzania ambapo kila kukicha gharama za bidhaa muhimu zinapanda bei...tuwalaumu wenye dola na sio Tanesco.
Quote
 
 
0 #15 2010-12-21 20:22
Hatari lakini salama!
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!
EWURA inaongozwa kisiasa katika kutoa maamuzi yake, yaani wahusika wa EWURA wapo pale kufanya kazi ya wale waliowaweka pale.
TANESCO waliomba muda mrefu kuongeza gharama za upatikanaji huduma ya umeme lakini kipindi chote hicho hawakuweza kuwaruhusu wapandishe gharama wakidai ni kubwa sana. Lakini leo hii baada ya kusikia deni kubwa la Dowans na Richmond, EWURA imetugeuka watanzania na kuamua kukubali ongezeko la bei ili zipatikane pesa za kulipa deni hewa la Dowans.
Inasikitisha sana lakini kinachosikitish a zaidi ni umbumbumbu tuliokuwa nao watanzania wengi wa kuweza kudanganyika na viongozi wachache kuwachagua kwa kigezo cha kuchagua chama.
Zama za kuchagua chama zimepitwa na wakati kwa sababu mafisadi wanajificha katika vyama vyetu. CCM ilikuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi, lazima tuhipiganie CCM yetu irudi kama ilivyokuwa zamani.
Hawa manyang'au inabidi wapigwe vita bila kujali kukosesha ushindi CCM, tuanze kufikiria kuwapa nafasi vyama vingine ili viongozi wetu wa CCM waanze kukumbuka maana halisi ya uadilifu ambao sasa wameamua kusahau au kuzarau kwa makusudi.
Na nchi kuifanya ya familia na marafiki!
Quote
 
 
0 #14 2010-12-21 16:39
Haruna unatudanganya Ewura na Tanesco lenu moja.....EWURA umeme ukiwa bei juu ninyi mnafaidika zaidi kwani asilimia moja ya mtumiaji wa kawaida kama ni Tshs.40 bei ikiwa juu asilimia moja ya mteja ni zaidi ya hiyo Tsh.40....ina maana EWURA mnafurahia/mnawashauri TANESCO wapandishe bei ili na nyie mchakachue hiyo asilimia moja yaani maslahi yenu yaongezeke..USHAURI.J.KIKWETE ivunje EWURA kama serikali yako haiwezi kuwalipa watumishi wake (EWURA)badala ya kututwisha mzigo wa kuwalipa EWURA mishahara na posho sisi wananchi tunaotumia umeme wa Tanesco kwani hali zetu za maisha ni duni sana!HARUNA MASEBO acha u[NENO BAYA] wa kutudanganya watanzania...hao wafanyakazi wa Tanesco ndio vishoka wa kucheza mita za umeme...iwejeunatudanga nya kuwa watalipa bill?Hilo umeliona leo?huo niu[NENO BAYA] ambao wewe na wenzako wa EWURA mmetunga...kuwadanganya watanzania....JK tumia busara kama unazo ivunjilie mbali hiyo EWURA...na mwajibishe [NENO BAYA] yako WILLIAMU NGEJLEJA alidanganya kuwa mgao wa umeme umeisha juma moja lilopita...KIKWETE UTKUWA MAKINI LINI?AU BADO MATATIZO YA KUANGUANGUKA YANAKUSUMBUA?....ugua pole!!
Quote
 
 
0 #13 2010-12-21 14:13
haya yote yanatokea na yalishatokea na yataendelea kutokea kwasababu watanzania hadi leo tumekuwa ni washabiki wa maisha yetu nasi wachezaji katika hayo maisha,nilichoj ifunza kipindi cha uchaguzi ilikuwa watu wanachukulia kama kipindi cha sherehe kinachoambatana na kuvaa khanga mpya na t-shirt na kupewa hela ya kutembelea siku ya sikukuu kama ambavyo mzazi anavyompa mtoto wake kipindi cha sikukuu,kama tulishindwa kujifunza miaka 5 iliyopita hatuwezi kujifunza tena na tutaendelea kuburuzwa na kuchubuka ngozi mwishowe mpaka mifupa itaonekana,tanz ania ya leo wale wenye nafuu ya maisha kidogo hawaipendi CCM,lakini cha kushangaza wale waliopigika vibaya ndio huwaambii kitu kuhusu CCM,mwishowe wanatusumbua na hicho kidogo tunachopata makazini kwetu ili tule nao.
Quote
 
 
0 #12 2010-12-21 13:50
imeamini kuna kundi dogo linalo control nchi hii, hivi kweli ndio mnamaanisha kuwa watanzania tuanze kulipa kwa njia ya mgogo wa nyumba, fidia ya dowans ama ni nini? na je kuna miundombinu gani mbadala ya nishati mbadala mliyoiandaa, mnadhan ni wote wataweza kumudu gharama hizi? na je mnapotukataza tusikate miti na kuchoma mkaa, mnadhani itawezekana????
Haya nyinyi mmeshika makali, sisi mpini, lakini tutakaposhika makali?? mtakipata.
shame on you!
Quote
 
 
+2 #11 2010-12-21 13:27
Ni mwanzo wa uchungu. Tutaendelea kushuhudia ugumu wa maisha ukiongezeka kwa nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi. Haya ndiyo tuliyoyachagua watanzania kwa gharama na u[NENO BAYA] wetu wenyewe. Tulibebwa kwenye magari tukavishwa nguo za kijani na njano, tukawachagua na kupoteza utu wetu kwa kodi zetu wenyewe!.
Quote
 
 
+2 #10 2010-12-21 12:52
Kama bei ya umeme inapanda pia bei ya gesi kwa sasa ndio usiseme, utakuwa na uwezo wa kumwambia mwananchi aache kupikia kwa kutumia kuni au Mkaa???
Quote
 
 
0 #9 2010-12-21 12:19
Serikali haiwezi kutoa ruzuku kwasababu hizo pesa zilizo ongezwa nikwaajili ya kulipia madeni ya makampuni hewa. Dawa ni kuleta ushindani katika soko la nishati hili TANESCO wasibweteke kama ambavyo tumepata afueni katika gharama za simu. INAWEZEKANA.
Quote
 
 
+1 #8 2010-12-21 12:17
DA!! KILA KUNAPOKUCHA HALI YA MAISHA INAZIDI KUWA NGUMU HIVI WATANZANIA TUTAENDA KUISHI WAPI!! HIVI KUSEMA UKEWELI WATAWALA WETU WA NCHI HII HAMLIONI HILI? MNAZIDI KURUHUSU BEI ZA UMEME KUPANDA ILI MJILIPE NA DOWANS YENU AMBAYO MMILIKI HAJULIKANI!! JK NA BARAZA LAKO KUWENI TAYARI KWA KUHUKUMIWA NA HISTORIA YA NCHI HII... SIJUI MTAISHI WAPI MTAKAPOTOKA MADARAKANI.
Quote
 
 
0 #7 2010-12-21 12:15
So,we thought the Kilimanjaro Stars victory was a big deal and we were proud as Tanzanians living abroad. However, that has prompted a new debate on www.zwapa.com (the Africans living abroad communication board) and we need some clarity from people who follows African soccer closely! Be the first to contribute at www.zwapa.com as soon as you can. Thanks
Quote
 
 
-1 #6 2010-12-21 11:28
Tunaomba serikali itoe ruzuku kwenye mafuta ya kuendeshea mitambo ya TANESCO ili kunususru watu wa kipato cha chini.
Quote
 
 
+5 #5 2010-12-21 10:42
MIMI NASHANGAA KUONA WATANZANIA HASA WALE AMBAO WALIKUWA NA SIFA ZA KUPIGA KURA LAKINI HAWAKUJITOKEZA KUPIGA KURA NA WALE AMBAO WALIPIGA KURA LAKINI WAKAAMUA KUICHAGUA CCM WANALALAMIKA.
WEWE KAMA ULIIPIGIA CCM KURA HATA HAKI YA KULALAMIKA HUNA MAANA UMEWACHAGUA MWENYEWE. KWAHIYO WE TULIA TU! UPATE KILE KILICHO HAKI YAKO KWA UCHAGUZI WAKO MBAYA HILI WAKATI MWINGINE UKISIKIA KUNA UCHAGUZI USIRUDIE MAKOSA KAMA HAYO.
Quote
 
 
+2 #4 2010-12-21 09:58
ivi ili shirika la umeme mna matatizo gani sisi wa kipato cha chini na tunahitaji umeme tataendelea kuangalia kwa majirani mpaka lini?me nadhani kuna uzembe unaofanyika na hivyo kutubebesha mzigo sisi wananchi ile hali mkijua hakuna tutakapo kimbilia lazima tutatumia huduma yenu hivyo ndo kama hivi mmepandisha bei ya umeme!!!!!!!!!! !
Quote
 
 
+4 #3 2010-12-21 09:16
Mimi nazani watanzania kasi mpya na nguvu mpya iliyo pamba moto, kwa sasa Tanzania ni nchi inayo ongoza kwa garama afrika mashariki ila serikali yetu inaona hiyo aitoshi na inataka sasa kuongoza dunia
Quote
 
 
+5 #2 2010-12-21 07:58
HAYA YOTE KWASABABU YA RICHMOND, DOWANS, IPTL NA SONGAS KWANINI SERIKALI ISIWEKEZE KWENYE UMEME ILI IACHANE NA HAWA WATU BINAFSI WANAOWALIPA PESA HATA WASIPOTOA UMEME HII NI SERKALI GANI ISIYOKUWA NA HURUMA KWA WANANCHI WAKE. WANATUINGIZA KWENYE MIKATABA MIBOVU LAKINI WANANCHI BADO TUMEKAA KIMYA NI WAKTI SASA WA WANANCHI KUANDAMANA NA KUKATAA HIZI BEI ILI SERIKALI IJIFUNZE. WAO HATA UMEME IPANDE VIPI HAWAJALI KWANI BILL ZAO TUNAZILIPA SISI. WATANZANIA BILA KUGANGAMALA TUTAONEWA KILA SIKU NA HII SERIKALI YA CCM. NI MUDA WA KUJIANDAA NA KUSEMEA HILI KWA MANENO, KWA VITENDO KAMA MAANDAMANO NA KUGOMA. TUSIBURUZWE. WAO WANAINGIA KWENYE MIKATABA MIBOVU WAKIJUA WATANZANIA WAPOLE WATALIPA TU. UKIWAAMBIA BASI PANDISHENI MISHAHARA WACHUNGU.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner