Bundi aliyemuondoa Mavunde ang’ang’ania

Meya waDodoma Jafari Mwanyemba

Muktasari:

  • Shinikizo la kumtaka kufanya hivyo lilifikiwa juzi kwa madiwani 43 kati ya 52 kujiorodhesha kumpinga.
  • Miaka 90, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Dodoma, Peter Mavunde na Mkurugenzi wake, Badru Bushako waliondolewa kutokana na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu.

Dodoma/Kyela. Bundi anayewanyemelea mameya wa Manispaa ya Dodoma, ametua tena na kusababisha Meya wa sasa, Jafari Mwanyemba kujiengua kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Shinikizo la kumtaka kufanya hivyo lilifikiwa juzi kwa madiwani 43 kati ya 52 kujiorodhesha kumpinga.

Miaka 90, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Dodoma, Peter Mavunde na Mkurugenzi wake, Badru Bushako waliondolewa kutokana na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu.

Mwanyemba alichukua hatua hiyo baada ya jana, madiwani kuendelea kulumbana kwa zaidi ya saa mbili kuhusu kuongoza kikao kabla ya kusalimu amri na kumpisha Naibu Meya, Jumanne Ngede kuendelea hadi atakapojibu tuhuma zinazomkabili.

“Nimeamua kwa hiari yangu na hasa baada ya kelele  nyingi,” alisema Mwanyemba akizungumzia uamuzi wake huo.

Madiwani wanamtuhumu kwa ubadhirifu wa Sh30 milioni za mradi wa maji wa Zuzu uliofadhiliwa na ubalozi wa Japan nchini na matumizi mabaya ya madaraka madai ambayo aliyakanusha.