CAG mstaafu ataka sera ya viwanda iende na uwajibikaji

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Ludovic Utouh.

Muktasari:

  • Akizungumza katika warsha ya siku moja ya kukuza uwajibikaji na utawala bora Utouh alisema ni vyema Serikali kuweka mkakati imara ili historia isije ikajirudia.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Ludovic Utouh amesema sera ya kukuza viwanda iende sambamba na kusisitiza uwajibikaji kwa viongozi.

Akizungumza katika warsha ya siku moja ya kukuza uwajibikaji na utawala bora Utouh alisema ni vyema Serikali kuweka mkakati imara ili historia isije ikajirudia.

Utouh alisema miongoni mwa sababu zilizochangia kuua  viwanda na mashariki ya umma ni ukosefu wa uwajibikaji kwa walikuwa wasimamizi wake.

"Tusingependa historia ikajirudia...tukajenga viwanda vikafa kama mwanzo  lazima kuwe na mkakati wa kusisitiza uwajibikaji kwa viongozi."