CCM yawashukuru wananchi kwa kura

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo amesema kura walizopata kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita unawapa ujasiri kuendelea kuwatumikia kwa kasi.

Muktasari:

Katika uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita Jimbo la Dimani, mgombea wa CCM, Juma Ali Juma alipata kura 4,860 dhidi ya mgombea wa CUF aliyepata kura 1,234 huku kati ya kata 20 ulikofanyika uchaguzi huo, madiwani 19 walioshinda ni wa CCM.

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewashukuru Watanzania kwa kukipigia kura kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar na kwenye kata 19 na kusema kitaendelea kuwatumikia kwa uadilifu na uaminifu.

Katika uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita Jimbo la Dimani, mgombea wa CCM, Juma Ali Juma alipata kura 4,860 dhidi ya mgombea wa CUF aliyepata kura 1,234 huku kati ya kata 20 ulikofanyika uchaguzi huo, madiwani 19 walioshinda ni wa CCM.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo amesema kura walizopata kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita unawapa ujasiri kuendelea kuwatumikia kwa kasi.

“Ushindi huu umezidi kutuimarisha kama chama na kupata nguvu ya kuendelea kuwatumikia wananchi,” amesema.”