DC Rombo amsweka rumande mwalimu

Muktasari:

  • Hokororo amesema tukio hilo limetokea (leo Jumatatu saa 12 asubuhi) baada ya mwalimu huyo kuwekewa mitego na wazazi wa mwanafunzi huyo  ambapo mwanafunzi huyo alitoroka nyumbani usiku na kwenda kulala nyumbani kwa malimu huyo.

Rombo. Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amemweka rumande mwalimu wa Shule ya Sekodari Matolo baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo.

Hokororo amesema tukio hilo limetokea (leo Jumatatu saa 12 asubuhi) baada ya mwalimu huyo kuwekewa mitego na wazazi wa mwanafunzi huyo  ambapo mwanafunzi huyo alitoroka nyumbani usiku na kwenda kulala nyumbani kwa mwalimu huyo.

Amesema baada ya wazazi na baadhi ya majirani walizingira nyumba ya mwalimu huyo na kunipigia simu ili akashuhudie wakifanya kitendo hicho.

“Kwa kweli ni jambo la kusikitisha  nilifika katika nyumba ya mwalimu  asubuhi  majira ya saa 12:00 na kukuta akiwa na mwanafunzi huyo huku  mwanafunzi akikiri kuwa amekuwa akitoroka mara kwa mara  na kuja kulala kwa mwalimu wake,”amesema Hokororo.