Tuesday, March 14, 2017

Fox fake ‘walamba’ tisa TBC

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taarifa za uongo za mitandao ya kijamii maarufu kama ‘fake news’ imewaingiza matatani wafanyakazi tisa wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC), baada ya kurusha hewani taarifa ya uongo iliyosambazwa na mtandao wa Fox channel.com, kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu utendaji kazi wa Rais John Magufuli na kwamba ni mfano mzuri wa kuigwa barani Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dk Ayoub Rioba alithibitisha kuchukuliwa kwa hatua na kusema kwa kifupi: “Ni kweli watu kadhaa wamesimamishwa kutokana na suala hilo.”

Walisimamishwa ni Elizabeth Mramba, Gabriel Zacharia, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.

Pia, Mtandao Foxnews umewahi kuripoti kuwa Rais mpya wa Zambia ameuawa, ilhali taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.

-->