Gereza la Iringa kuhamishwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba .

Muktasari:

  • Gereza hilo lililopo katika Kata ya Miomboni, lipo jirani na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na uwapo wake umelalamikiwa na wakazi wa mji huo wanaodai hushindwa kuwafikisha wagonjwa hospitalini kutokana na barabara hiyo kufungwa nyakati za usiku kwa sababu za kiusalama.

Iringa. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameuagiza uongozi wa Jeshi la Magereza mkoani Iringa kuanza mchakato wa kulhamisha gereza kuu la mkoa huo kutoka katikati ya mji na kwenda pembezoni mwa mji.

Gereza hilo lililopo katika Kata ya Miomboni, lipo jirani na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na uwapo wake umelalamikiwa na wakazi wa mji huo wanaodai hushindwa kuwafikisha wagonjwa hospitalini kutokana na barabara hiyo kufungwa nyakati za usiku kwa sababu za kiusalama.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya siku moja mkoani hapa na kutembelea eneo hilo kujionea hali halisi jana, Mwigulu aliuagiza uongozi wa gereza kuanza mchakato huo mara moja.

Mwigulu aliwataka viongozi hao kuanza mchakato wa ujenzi wa gereza jipya lilipo gereza dogo la Mlolo eneo la Kwa Kilosa.