Hatimaye bodi yapata mkandarasi

Muktasari:

Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Innocent Mlay akizungumza juzi mbele ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Nicodemus Tarmo na Mkurugenzi mtendaji, Hamis Mahinga alizitaja barabara hizo kuwa ni za tarafa ya Mbungwe na Godoa.

Babati. Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara, imepanga kutumia Sh216 milioni kuimarisha miundombinu ya barabara kwa kipindi cha miezi minne ijayo.

Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Innocent Mlay akizungumza juzi mbele ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Nicodemus Tarmo na Mkurugenzi mtendaji, Hamis Mahinga alizitaja barabara hizo kuwa ni za tarafa ya Mbungwe na Godoa.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Nicodemus Tarmo alisema vigezo vilivyotumika kuipata kampuni hiyo ni bodi ya zabuni iliyowashindanisha na makandarasi mbalimbali kwa kushirikiana na ofisi ya mwanasheria wa Serikali.

Mahinga akizungumza baada ya kutiwa saini mkataba huo, alisema wananchi wa maeneo hayo nao watafaidika kwa kupata ajira na kusafirisha mazao.