IPTL wairuka benki ya Standard Chartered - Hong Kong

Picha na Omari Fungo.

Muktasari:

  • Kampuni hiyo inaunga mkono hatua ya Tanesco kukata rufaa katika màhakama ya ICSID kwasababu hukumu iliyotolewa ina mapungufu mengi kisheria.

Dar es Salaam. Kampuni ya kufua umeme ya IPTL imesema haiitambui benki ya Standard Chartered - Hong Kong kama mdai wao wala haina haki ya kupata malipo yoyote kwa niaba yao.

Kampuni hiyo inaunga mkono hatua ya Tanesco kukata rufaa katika màhakama ya ICSID kwasababu hukumu iliyotolewa ina mapungufu mengi kisheria.

Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege amesema watu wasifanye makosa kuilipa benki  hiyo Kwa sababu wanataka kutapeli.

"Hii benki ya Standard Chartered haistahili kulipwa fedha yoyote kwa niaba yetu. Hatuwatambui kama wadai wetu, ndiyo maana wanakimbia mahakama za ndani na kwenda nje."