JPM amteua Alphayo Kidata Katibu Mkuu Ikulu

Alphayo Kidata

Muktasari:

  • Kidata anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Peter Ilomo ambaye amestaafu.
  • Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli, leo tarehe 23 Machi, 2017 amemteua Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Kidata anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Peter Ilomo ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Uteuzi wa Kidata unaanza mara moja na ataapishwa kesho tarehe 24 Machi, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.