Kazi ya kukinyanyua kivuko cha MV Nyerere kufanyika leo

Muktasari:

Meli yenye vifaa maalum vya kukinyanyua na kukigeuza kivuko cha MV Nyerere kurahisisha uokoaji imewasili katika kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe

Ukerewe. Meli yenye vifaa maalum vya kukinyanyua na kukigeuza kivuko cha MV Nyerere kurahisisha uokoaji imewasili katika kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameieleza MCL Digital leo Jumapili Septemba 23, 2018 leo kuwa kazi ya kunyanyua kivuko hicho itafanywa na wataalam wa masuala ya usafirishaji na uokoaji.

MCL Digital imeshuhudia baadhi ya wataalam wa uokoaji, wakiwemo wazamiaji wakishusha majini baadhi ya maboya yatakayotumika kukinyanyua kivuko hicho.

Kazi ya kukinyanyua kivuko hicho inatarajiwa kufanikisha upatikanji wa miili zaidi  kutokana na kile kilichoaminika kuwa ipo miili iliyokandamizwa, kulaliwa na mizigo ndani ya kivuko.

Meli malaum ya kampuni ya Nyehunge yenye winchi la kunyanyua vitu vizito, tayari imesogezwa hatua chake na kilipozama kivuko cha MV Nyerere.