Kubenea: Tumeokoa Sh 1.2 bilioni za ufuaji majoho ya madiwani

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea

Muktasari:

  • Kubenea ameyasema hayo leo wakati alipofanya mkutano wa hadhara uwanja wa Mabibo Farasi ikiwa ni ziara ya kwanza jimboni kwake tangu achaguliwe Oktoba 2015.
  • "Ubungo tumeokoa Sh 430 milioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho 18 ya madiwani, Kinondoni Sh 800 milioni kwa majoho 58 na tangu Aprili mwaka jana hatujafua na hatujatoka upele," amesema Kubenea.

Dar es Salaam. Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea amesema tangu Chadema ichukue halmashauri mbalimbali jijini hapa imefanikiwa kuokoa Sh 1.2 bilioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho ya madiwani Kinondoni na Ubungo kwa mwaka.

Kubenea ameyasema hayo leo wakati alipofanya mkutano wa hadhara uwanja wa Mabibo Farasi ikiwa ni ziara ya kwanza jimboni kwake tangu achaguliwe Oktoba 2015.

"Ubungo tumeokoa Sh 430 milioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho 18 ya madiwani, Kinondoni Sh 800 milioni kwa majoho 58 na tangu Aprili mwaka jana hatujafua na hatujatoka upele," amesema Kubenea.

Kubenea amefanya ziara hiyo na itakuwa muendelezo wa kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo la Ubungo.