MO atajwa kusaidia maskini

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohammed Dewji.

Muktasari:

Jarida la Forbes linakadiria utajiri wa Mo Dewji ni zaidi ya Dola 1.1 bilioni za Marekani (Sh2.42 trilioni).

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohammed Dewji maarufu Mo Dewji ametajwa kuwa miongoni mwa matajiri vijana ambao nusu ya utajiri wao wameamua kuutumia kusaidia maskini.

Jarida la Forbes linakadiria utajiri wa Mo Dewji ni zaidi ya Dola 1.1 bilioni za Marekani (Sh2.42 trilioni).

Mo Dewji amejiunga katika kundi linalojulikana ‘Giving Pledge’ na kuahidi kutoa angalau nusu ya utajiri wake kusaidia maskini duniani.

Wengine waliotoa ahadi hiyo ni Eli Broad na mke wake, Edythe; John Doerr na mke wake, Ann na mwanzilishi wa mtandao wa facebook, Mark Zuckerbery na mkewe, Priscilla Chan.