Magufuli amteua Sanga bosi PSSSF

Muktasari:

  • Kabla ya uteuzi Sanga alikuwa mfuko wa LAFP

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ameendelea kuteua viongozi wa mashirika ya umma baada ya kumteua Eliud Sanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Uteuzi wa Sanga ulitangazwa jana usiku Julai 21, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliono ya Rais-Ikulu Gerson Msigwa kupitia taarifa kwa umma.

Kabla ya uteuzi huo, Sanga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pension wa LAPF.

Rais Magufuli amemteua Sanga ikiwa zimepita siku nane tangu alipomteua William Erio kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Julai 14, 2018.

Erio aliteuliwa baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara.