Mahakama yaombwa kuharakisha kesi za ugaidi

Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Rajab Katimba akizungumza na waandishi wa habari. Picha ya maktaba

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari leo, msemaji wa jumuiya hiyo, Sheikh Rajab Katimba amesema taasisi hiyo inapinga vitendo vya ughaidi ila wote walioshikiliwa wanatakiwa uchunguzi ukamilike ifahamike kama wamehusika au la.

Dar es Salaam. Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania imezitaka mahakama kuharakisha kesi za ugaidi zinazowakabili waislamu mbalimbali nchini kwasababu wamekaa zaidi ya miaka mitatu jela.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, msemaji wa jumuiya hiyo, Sheikh Rajab Katimba amesema taasisi hiyo inapinga vitendo vya ughaidi ila wote walioshikiliwa wanatakiwa uchunguzi ukamilike ifahamike kama wamehusika au la.

"Masheikh na waumini mbalimbali wamekamatwa karibu kila mkoa nchini, inadaiwa uchunguzi unaendelea na miaka inaenda. Mahakama iharakishe kesi hizo," amesema Sheikh Katimba.