Majaliwa ataka maelezo matumizi ya Sh340milioni

Muktasari:

Ametoa kauli hiyo leo Februari 18, 2018 wakati akizungumza  na watumishi wa halmashauri hiyo na kubaini kiasi hicho cha fedha hakijulikani kilipo.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe, Frank Bahati na mhasibu wa Halmshauri hiyo, Peter Mollel kumpatia taarifa ya matumizi ya Sh340milioni zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo Februari 18, 2018 wakati akizungumza  na watumishi wa halmashauri hiyo na kubaini kiasi hicho cha fedha hakijulikani kilipo.

Amesema hadi Februari 21, 2018 anataka kupata taarifa ya fedha hizo, kwamba hatima ya viongozi hao itajulikana baada ya kupokea taarifa hiyo.

"Halmashauri hii imekuwa mchwa, kuna fedha nyingi za maendeleo zinaletwa lakini zinatafunwa jambo hili halikubaliki hata kidogo lazima tushughulike na watendaji wa namna hii,” amesema Majaliwa,

“Lazima nipate taarifa ya fedha hizi, mmezipeleka wapi? Hatima yenu ni tarehe 21 mtakaponiletea taarifa kamili lazima kwanza tujiridhishe na haya alafu tuchukue hatua.”