Friday, July 21, 2017

Mke wa Mwakyembe afariki duniaLinah Mwakyembe enzi za uhai wake

Linah Mwakyembe enzi za uhai wake 

By Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Dar es Salaam .Mke wa Waziri wa Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe  amefariki usiku wa kuamkia leo  jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,  Wizara ya Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo Zawadi  Msalla  amesema Marehemu Linah Mwakyembe  amefariki  akipatiwa matibabu  hospitali ya Agha Khan.

Anasema shughuli za  msiba huo zinafanyika nyumbani kwa Waziri Mwakyembe, Kunduchi  Beach jirani na Chuo  cha  Mafunzo ya Kijeshi  jijini Dar  es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi mtoto wa Marehemu George amethibitisha kifo cha  mama yake  huku akisema taarifa zaidi zitatolewa na baba yake.

-->