‘Mlinzi’ avamia kikao cha shule kudai deni lake

Muktasari:

Akizungumza kwenye mkutano huo juzi, Malimi alisema kampuni hiyo iliingia mkataba Septemba 2016 na walinzi wake walikuwa wakilipwa Sh130,000 kwa mwezi, lakini tangu Rais John Magufuli alipozuia michango shuleni hadi Januari 17 hawajalipwa ilipositisha ulinzi.

Meneja wa kampuni ya ulinzi la Kilumi Security tawi la Ushirombo mkoani Geita, Malingumu Malimi ameibuka kwenye kikao cha wazazi cha Shule ya Msingi Igulwa kudai Sh245,666 ambazo hazijalipwa tangu Novemba mwaka jana.

Akizungumza kwenye mkutano huo juzi, Malimi alisema kampuni hiyo iliingia mkataba Septemba 2016 na walinzi wake walikuwa wakilipwa Sh130,000 kwa mwezi, lakini tangu Rais John Magufuli alipozuia michango shuleni hadi Januari 17 hawajalipwa ilipositisha ulinzi.

“Niombe kamati ya shule ishirikishe serikali ya kijiji kuona namna wataweza kulipa deni hilo, ili kuepusha migogoro,” alisema Malimi.

Akizungumzia suala hilo, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Joseph Lucian alisema shule ina wanafunzi 859 inakabiliwa na madeni mbalimbali ambayo yatapelekwa kwenye serikali ya kijiji.

“Shule inakabiliwa na deni la maji tangu 2016 la Sh340,000 na kiwango lilichochagwa na wazazi ni Sh26,000, deni la mlinzi wa ni Sh245,666,” alisema.

Mmoja wa wazazi, Rehema Ally aliiomba kamati ya shule iwe inatoa taarifa haraka za madeni ili kuondoa changamoto hizo, lakini serikali ya kijiji na kamati ya shule iangalie namna ya kuajiri mlinzi ili kunusuru mali za shule.

NAye mwenyekiti wa maendeleo ya shule hiyo, James Chopa alisema kikao kilichofanyika Desemba 12 mwaka jana walikubaliana kuchanga kila mtoto Sh600 zitakazofanikisha kulipa deni la maji na mlinzi.

“Shule ina wanafunzi 859 kila mtoto alitakiwa kutoa Sh600 ambazo zingekuwa jumla ya Sh515,400 zingetosha kulipa mlinzi na maji,” alisema Chopa

Chopa alimuomba mlinzi mlinzi kuwa mvumilivu wakati deni lake likifishwa kwenye serikali ya kijiji kuona namna ya kumsaidia.

Ofisa mtendaji wa kata ya Katente, Pamba Mgabali alisema haja pata taarifa ya madeni ya shule hiyo nakwamba kutokana na ukosefu wa mlinzi kunawizi mudogo mdogo wa miundo mbinu ya shule umeaza kutokea ambapo amewataka watendaji wa vijiji na wenyeviti kuimarisha ulinzi.

Mwisho